Kwanini siwezi kua Masikini???? [PART1]!

kwanini

kwanini

Lengo La Kuandika Ujumbe Huu Si Kujisifia Bali Kukusaidia Ujifunze KANUNI HII YA AJABU Ambayo Mungu Alinifundisha Ambayo Baada Ya Kuielewa Imenipa UHAKIKA WA KUTOKUWA MASIKINI MAISHANI… Ukipotezwa Na Kichwa Hapo Juu, Umekosa Siri Za Kukukwamua Kwenye HALI YAKO YA UCHUMI NA FEDHA!

ALICHONIFUNDISHA MUNGU
“FEDHA/PESA INAFUATA THAMANI YA MTU; IKIKUTA THAMANI NDANI YAKE INAKAA, IKIKOSA THAMANI NDANI YAKE, INAONDOKA”

Hivi Umewahi Kumwona MILIONEA AU BILIONEA Ambaye Ni MILIONEA AU BILIONEA LEO Ambaye Amepata Huo UMILIONEA AU UBILIONEA “KWA KUSHINDA BAHATI NASIBU [LOTTO/ JACKPOT]”???
Jibu Ni Rahisi, HAKUNA!
Unajua Ni Kwanini?
Ni Kwa Sababu WALIPATA PESA KWA BAHATI NASIBU [LOTTO/ JACKPOT] LAKINI PESA ILIPOKUJA KWAO, IKAKUTA “HAWANA THAMANI SAWA NA HIYO PESA AU ZAIDI” IKAONDOKA!
Namaanisha Nini?
PESA SI “ZILE KARATASI AU SARAFU ZA SHILINGI AU DOLLAR AU POUND” HAPANA!
PESA NI “THAMANI YA MFUMO WA KIMAWAZO NA KIAKILI WA KIUZALISHAJI NA KIUSIMAMIZI ALIONAO MTU”

Kuna Mtu UKIMPA LAKI MOJA LEO, WIKI MBILI ZIJAZO ATAKUWA NA MILIONI MKONONI, NA KUNA MTU AMBAYE UKIMPA MILIONI MOJA LEO, WIKI IJAYO ATAKUWA NA LAKI MOJA MKONONI…
UNAONA,
TATIZO SI YALE MAKARATASI YA SHILINGI, DOLLAR, EURO, POUND NAKADHALIKA; TATIZO NI “THAMANI HALISI ALIYONAYO MTU NDANI YAKE KWENYE ENEO LA UZALISHAJI, UWEKEZAJI, USIMAMIZI, UBUNIFU, MASOKO, MAHUSIANO NAKADHALIKA” NA HIKI NDICHO KINAMTOFAUTISHA MTU NA MTU!
Aliye Na Thamani Kubwa ATAVUTA PESA Na Asiye Na Thamani PESA ZITAMKIMBIA!

TUJIFUNZE KWA IBRAHIMU

Huyu Mzee Aliondoka HURU WA WAKALDAYO Katika NCHI YAKE NA KWENDA UGENINI [Abroad] KANAANI Sawasawa Na Maagizo Ya Mungu Akiwa Na Ndugu Yake LUTU NA MKEWE SARA!
Waliondoka MIKONO MITUPU Kule Wakiwa WATU WA KAWAIDA, Lakini Baada Ya MUDA MFUPI Walikuwa WAMETAJIRIKA KWENYE ENEO LA MIFUGO Kiasi Kwamba WACHUNGAJI WA IBRAHIMU NA WA LUTU WAKAWA WANAGOMBEA MALISHO! (Mwanzo 13:5-11).
Lakini Pia Biblia Inasema , “IBRAHIMU ALIKUWA TAJIRI SANA KATIKA MIFUGO, FEDHA NA DHAHABU” (Mwanzo 13:2).

NINI KILIMFANYA IBRAHIMU AWE TAJIRI???

Cha Kwanza Kabisa Tunajua Ya Kwamba “MUNGU ALIMPA NGUVU YA KUPATA UTAJIRI” (Kumbukumbu 8:18).
Hivyo ILITEGEMEA “MATUMIZI YA HIYO NGUVU” Ili KUUPATA UTAJIRI WENYEWE!
Nilichojifunza Kwa Ibrahimu Ni Hiki: “IBRAHIMU ALIJENGA THAMANI YAKE KWA KIWANGO CHA JUU SANA KIASI KWAMBA AKAIFANYA PESA NA MALI VIMFUATE”
Acha Nikurahisishie Kidogo:
“IBRAHIMU, ALIJIJENGEA THAMANI NDANI YAKE KATIKA MASWALA YA UFUGAJI, UWEKEZAJI, USIMAMIZI WA PESA, NA VYANZO VYA UCHUMI KIASI KWAMBA PESA ILIPOKUJA ILIMKUTA AKIWA NA THAMANI KUBWA, BADALA YA KUONDOKA KWAKE, IKAANZA KUITA PESA NYINGINE KUJA”
Wazungu Wanasema, “PESA INAZAA PESA [Money Begets Money]”
Ndani Ya IBRAHIMU Alikuwa Ameshafanya UCHUNGUZI Kuhusu Maswala Ya UFUGAJI Na Namna Ya Kustawi Katika Eneo Hilo [ALISHAJIJIENGEA THAMANI KWENYE MASWALA YA UFUGAJI], Lakini Pia Alishafanya UTAFITI Kuhusu MADINI YA FEDHA [Silver] Na MADINI YA DHAHABU [Gold] Hivyo PESA ILIPOKUJA, ILIKUTA TAYARI ANA “THAMANI KUBWA NDANI YAKE” Na Ameshaweka “MFUMO WA KUZIFANYA PESA ZIZAE PESA”
Hivyo ZILIPOKUJA “AKAZIWEKEZA KWENYE ARDHI” Maana Biblia Inasema, “HAKUKUBALI KUPEWA BURE HATA MAHALI PA KUZIKIA MKEWE SARA, BALI ALINUNUA KWA PESA YAKE, LENGO LIKIWA NI KUWA NA CHANZO CHA UCHUMI CHA KWAKE BINAFSI” Lakini Pia “ALIWEKEZA KWENYE MIFUGO” Na Ndiyo Maana Biblia Inasema “ALIKUWA TAJIRI SANA KWENYE MIFUGO” Kiais Kwamba “ENEO LA KULISHIA LIKAWA DOGO IKABIDI AACHANE/ ATENGANE NA NDUGU YAKE LUTU KUEPEUSHA UGOMVI KATI YA WACHUNGAJI WAO”
Lakini Pia “ALIWEKEZA KWENYE MADINI” Na Ndiyo Maana Biblia Inatwambia “ALIKUWA TAJIRI SANA KATIKA [MADINI YA] FEDHA NA DHAHABU”
Huyu Ndugu Alijua “THAMANI YA PESA HUWA INASHUKA KADRI MUDA UNAVYOKWENDA” Hivyo “AKAIBADILI PESA YAKE NA VITU VINAVYOPANDA BEI [MIFUGO, ARDHI, MADINI]”
Si Pesa Zilizomtajirisha IBRAHIMU Bali Ni “THAMANI YAKE” Iliyovuta UTAJIRI UJE KWAKE!

Je Hadi Hapo, Kwa Siri Hizi Naweza Kuwa Masikini?
Hata Kwa Dawa, Hata Kama Majeshi Yote Ya Kuzimu Yangeungana Kinyume Changu, HAYAWEZI KUVUNJA HIZI KANUNI ZA USHINDI ALIZONIPA MUNGU ZA KUNIFANYA TAJIRI!

Ulichosoma Hapa Kinatosha Kukufanya UWE TAJIRI, Kirudie Kukisoma Tena Na Tena Mpaka UELEWE SANA, Kisha Kifanye MFUMO WAKO WA MAISHA, Na PESA ITAKAPOKUJA KWAKO ITAKAA Maana Tayari THAMANI YAKO ITAKUWA KUBWA NA ITAVUTA PESA ZAIDI!!!

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: