Mambo Manne Muhimu sana

Mambo manne

Mambo Manne

MAMBO MANNE YA MUHIMU SANA YATAKAYOKUFANYA UWEZE KUTIMIZA NDOTO, MAONO AU JAMBO LOLOTE KWENYE MAISHA!

Kama Unataka Kufanya Chochote Kwenye Maisha Kiwe KIKUBWA AU KIDOGO Lazima Uzitumie Hatua Hizi Nne, Na Lazima Utapitia Hatua Hizi Nne.

Yaani Hizi Hatua Nne Ni MWONGOZO Wa Kukusaidia KUTIMIZA Chochote.

JAMBO LA KWANZA:
“JUA UNATAKA NINI/ UNATAKA KUFANYA NINI”

-Mtaji Wako Wa Kwanza Katika Kutimiza Au Kufanya Jambo Lolote Ni KUJUA NINI UNATAKA/ NINI UNATAKA KUFANYA
-Uwe Na PICHA YA NDANI [MENTAL PICTURE] Ya Kile Unataka Au Kile Unataka Kufanya
-Hakikisha Hicho Unachotaka Kufanya Au Unachotaka KISIISHIE KICHWANI MWAKO Bali Chukua HATUA YA KUKIANDIKA Kwenye DIARY, NOTEBOOK, DAFTARI Au Mahali Maana Ni Rahisi Kuanza Kupunguza Vitu Kwa Kusahahu Kama Hautakiandika Hicho Unachotaka/ Unachotaka Kufanya
-Haijalishi Hakuna Aliywahi Kukifanya Au Wewe Ndo Wa Kwanza Kupata Wazo La Namna Hiyo, ISIKUPE SHIDA, Maadamu UMEWEZA KUKIONA NDANI YAKO [VISUALIZE IT IN YOUR MIND] Huo Ni Ushahidi Tosha Kwamba UNAWEZA KUKIFANYA KITOKEE… Vitu Vingi Vinavyoonekana Leo HAVIKUWAHI KUWEPO, Lakini KUNA WATU WALIAMINI WANACHOONA NDANI YAO, WAKAKIANDIKA, WAKAAMUA KUKIFUATILIA KWA GHARAMA ZOTE MPAKA KIKATOKEA NA KUWA HALISI!
-Usipojua Unachotaka Kufanya Au Unachotaka UTAYUMBISHWA NA WATU, MAZINGIRA, HALI YA UCHUMI, Nakadhalika Na UTAPOTEZA NDOTO YAKO.
-Hakikisha Umekijua Vizuri Na Kwa Undani Kile Unachotaka AU Unachotaka Kufanya.
HII NI HATUA MUHIMU SANA YA KWANZA KABISA ITAKAYOKUPA CHOCHOTE MAISHANI MWAKO!

JAMBO LA PILI:
“NAMNA GANI UTALIPATA HILO JAMBO/ NAMNA GANI UTALIFANYA HILO JAMBO”

-Hii Ni Hatua Ya MIPANGO GANI Utaitumia Kupata Unachokitaka/ Kuweza Kufanya Unachotaka Kufanya?
-Hii Inasimama Kuwakilisha NJIA ZIPI Utazifuata Kuweza Kulifanya Hilo Jambo Kuwa Halisi?
-Hii Inahusisha MIKAKATI GANI Utaitumia Kufikia Lengo Lako?
-Hii Inahusisha MALENGO GANI Utayafuatilia Mpaka Yakufikishe Unapotaka Kufika?
-Hii Inahusisha MAMBO GANI UTAPASWA KUYAKWEPA Kama Unataka Kufikia Ndoto Yako?
-Hii Inajumuisha WATU GANI UNATAKIWA KUWAACHA/ KUWAKWEPA Kama Kweli Umeamua Kufikia Ndoto Yako?
-Hii Inajumuisha WATU GANI Itakupasa Uwe Karibu Nao Watakaokusaidia Kufikia Ndoto Yako?
-Hii Inahusisha AINA GANI YA VITABU Itakubidi USOME ILI KUPATA SIRI NA UJASIRI WA KUPAMBANA NA KUENDELEA MBELE?
-Hii Itahusisha MAZINGIRA YAPI UKAE NDANI YAKE NA YAPI UYAKWEPE KAMA UNATAKA KUFIKIA NDOTO YAKO?
HIKI KIPENGELE CHA PILI NI CHA MUHIMU SANA: Usipojua NAMNA YA KUKIPATA UNACHOKITAKA, HAKIKA HAUTAKIPATA!
Utakapokusanya Yote Haya YAANDIKE KWENYE DIARY, NOTEBOOK Au DAFTARI LAKO Maana Ni Rahisi Kusahahu Au Kupunguza Mambo Kadhaa Usipoandika… JITAHIDI KUANDIKA, USIJIDANGANYE KWAMBA YOTE YAKO KICHWANI, HUO NI UONGO WA SHETANI ILI AKUIBIE WAZO LAKO!

3.JAMBO LA TATU
“WEKA KWENYE MATENDO HIYO MIPANGO, MALENGO, MIKAKATI YA NAMNA YA KUKIPATA UNACHOKITAKA”

-Hii Ni Hatua Ya Muhimu Sana, KUWA NA WAZO PEKE YAKE HAITOSHI, Kuwa Na MAONO Peke Yake Haitoshi
-Kuwa Na NJIA, MIPANGO, MIKAKATI Peke Yake Haitoshi, Yote Yatatoa Matunda UKICHUKUA HATUA YA KUANZA KUTENDEA KAZI “JAMBO LA PILI”
Weka Kwenye Matendo Zile NJIA, MIPANGO NA MIKAKATI YAKO.
-Unapoweka Kwenye MATENDO Unaonesha Kwamba UMEMAANISHA NA UNATAKA KUPATA MATOKEO, Usipochukua Hatua Utaishia Kuwa Na Ndoto Nzuri Isiyoweza Kuwa Halisi.
-Unapoweka Kwenye Matendo UNAONESHA IMANI YAKO KWA MUNGU, Unaonesha IMANI YAKO KWAKO, Na Unaonesha IMANI YAKO KWA NDOTO YAKO.
-Usipochukua Hatua Ya Kuweka Kwenye Matendo Hakuna Mwingine Atakayefanya Chochote Kwa Niaba Yako.
-Watu Wengi Wameshindwa Kufikia Ndoto Zao Kwa Sababu Ya kutochukua Hatua Na Kuanza.
-Unapoweka Kwenye Matendo Inaonesha Uthubutu Wako; Na Usipothubutu Mungu Naye Hatafanya Miujiza Yake Kwako.
CHUKUA HATUA, ANZA KUTENDEA KAZI HIZO NJIA, MIPANGO, MIKAKATI NA MALENGO YAKO… HAKIKISHA KILE ULICHOANDIKA KINAKUWA HALISI KUPITIA UTENDAJI WAKO!

JAMBO LA NNE:
“FANYA MAREKEBISHO KADRI INAVYOTAKIWA MPAKA UTAKAPOONA UMEPATA NDOTO YAKO”

-Kadri Unavyochukua Hatua NA KUTENDEA KAZI MIPANGO, MIKAKATI, NJIA NA MALENGO YAKO, Utagundua Kuna MENGI YA KUONGEZA NA MENGI YA KUONDOA… Ya Kuongeza Ongeza Na Ya Kupunguza Punguza.
-Safari Ya Mafanikio Ni Safari Ya Makosa Mengi; Rekebisha Makosa Na Jifunze Tokana Na Makosa Halafu Endelea Mbele Mpaka Upate Matokeo Unayotaka.
-Kadri Unavyochukua Hatua Ya Kutenda, Utapata Maarifa, Ujuzi Na Mbinu Mpya Kwa Watu Waliofanikiwa, Vitabu Na Vyanzo Vingine Vya Taarifa Utagundua Wapi Yaliko Mapungufu Na Utayaweka Sawa Kuelekea Ndoto Yako.
-Mjenzi Hujenga Tofali Kwa Tofali Kila Siku, Hupanga Na Kupangua Pale Alipogundua Amekosea Mpaka Anapofikia Ukamilishaji Wa Jengo.
-Hii Ni Hatua Ya Kufumbua Macho Yako Na Cha Kuongeza Na Cha Kupunguza Mpaka Unapokamilisha Ndoto Yako.

HIZI NI HATUA NNE ZA MUHIMU KUWEZA KUFANYA LOLOTE LIWE HALISI,
ZIWEKE KWENYE MATENDO, HAKIKA HAZITAKUANGUSHA,
NAAMINI ALIYEKUSUDIWA NA MUNGU LEO, AMEPOKEA CHA KUMSAIDIA.
Usipofanikiwa Usimlaumu Yeyote, Jilaumu Wewe Kwa Kutozingatia Na Kutotumia Maarifa Uliyopewa Bure!

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “Mambo Manne Muhimu sana
  1. bertha says:

    kazi yako ni njema mtumishi endelea kutimiza kusudi la Mungu.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: