Je unapowapa watu vitu,unavitoa kwa jicho la sadaka???

Hivi Umewahi Kujiuliza Kama Mungu Akikupa VITU AMBAVYO TAYARI UNAVYO Badala Ya VILE UNAVYOHITAJI, Utafurahi Na Kupokea Kwa Furaha Kama Ambayo Akikupa VILE UVIHITAJIVYO SANA KWA WAKATI HUO???
Unapochukua Hatua Ya KUMPA MTU MWINGINE KITU [KWA JICHO AU MTAZAMO WA SADAKA] Hakikisha UNAMPA KILE AMBACHO “HATA MOYO WAKO UNAJUA UNAKIPENDA SANA NA KUKITHAMINI” Tofauti Na Hapo Ni KUPOTEZA BURE ULICHOTOA… Utaishia Kupata ASANTE YA MHITAJI Lakini Kwakweli HAUTAPATA MATOKEO KWENYE MADIRISHA YA MBINGUNI!!!
Mungu Anawapenda Wale WANAOTOA KWA “MOYO NA JICHO LA UPENDO”
Mtu Anayetoa KWA UPENDO Hawezi KUMPATIA ANAYEMPENDA “KITU AMBACHO YEYE MTOAJI HAKITHAMINI”
Hawezi Kuchukua Suruali Yake Ya KUMI KWA UBORA Kama SADAKA Ilhali YEYE MWENYEWE Anaelewa HATA AKIPEWA ZAWADI “KITU HICHOHICHO” WALA HAWEZI KUKIPOKEA KWA “FURAHA YA JUU” Maana Ni Kitu Ambacho “NI CHA KAWAIDA SANA KWAKE” Na “HAKINA THAMANI KUBWA KIVIILE KWAKE”
Mungu Alipoamua KUTOA… ALIMTOA “MWANAYE MPENDWA NA WA PEKEE” Anayemhitaji Na Kumjali Na Kumthamini Kuliko Chochote Kingine Mbinguni.
Yesu Alipoamua KUTOA… ALIUTOA UHAI WAKE [ZAWADI NA SADAKA KUBWA] KULIKO CHOCHOTE KINGINE ALICHOKUWA NACHO! Sikuambii UTOA MAISHA/ UHAI WAKO ILA NAKUONESHA “NAMNA SAHIHI YA UTOAJI”
Ibrahimu Alipoamua KUTOA… ALIMTOA “MWANAE WA PEKEE NA ALIYEMHITAJI KUWA MRITHI NA MWENDELEZA KIZAZI CHAKE”
Unapoamua KUTOA KITU KWA MTU KAMA ZAWADI [SADAKA] Hakikisha Unatoa KILE KINACHOUGUSA NA KUUMA MOYO WAKO… KILE KISICHO NA THAMANI MBELE YAKO HAKIWEZI KUWA NA THAMANI MBELE ZA MUNGU!
Usijefanya Kosa La Kudhani Anayepokea Hiyo ZAWADI/ SADAKA Ni Huyo Mtu, HAPANA… MUNGU ANAKUNJUA MIKONO KUIPOKEA KWANZA KABLA YA HUYO UNAYEMPATIA HUKU DUNIANI!!!
Kornelio Alikuwa ANAWAPA WATU SADAKA Huku DUNIANI Lakini ZILIKUWA ZINAPOKELEWA MBINGUNI Mpaka ZIKAWA UKUMBUSHO MBELE ZA MUNGU (Matendo 10:1-4).
KILE AMBACHO “HATA WEWE UKIPEWA HAKITAKUFURAHISHA KIVILE” Hakikisha Na Wewe HAUKITOI KWA MWINGINE… Kama Hakina Thamani Kwako, HAKIWEZI KUWA NA THAMANI KWA MUNGU!

Asomaye Na Afahamu,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “Je unapowapa watu vitu,unavitoa kwa jicho la sadaka???
 1. eliakim paul says:

  mtumishi hapo sijakuelewa?
  si kila kisichona thamani kwangu na kwa mwingine hakina thamani!!!!
  ni mara nyingi nimekuwa nikiacha kuvaa viatu ambavyo mimi nahisi vimepitwa na wakati angali vyenyewe havijachakaa, na jamaa zangu wa kijijini siku wakija home au nimeenda kuwatembelea nikiwapatia viatu hivyo kwao geuka shangweeeee

  wakati mwingine wananangu wanatupa chips na vyakula vingine vizuri ila siku watoto wa ndg zangu wakija vyakula hivyo ugeuka cha thamani.

  nachotaka kusema si kila kisicho cha thamani kwako , na kwa wengine hakina thamani.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: