KAMA UNA WAZAZI AMBAO BADO WANAISHI: AU WALEZI WALIOKULEA TANGU CHINI

 [SOMA HII ITAKUSAIDIA]!

wazazi/walezi

wazazi

1.Jitahidi Uwe Na Mawasiliano Nao Ya Uhakika; Walau Wapigie Simu Hata Mara Mbili Au Tatu Kwa Wiki… Ukiweza Kila Ukiamka Unaongea Nao Mara Baada Ya Kuongea Na MUNGU [Mzazi Namba Moja] Itapendeza Sana.
Wazazi Wako Wamekupa Upendo Kwa Miaka Mingi, Ni Wakati Wako Kuanza Kuwapa Upendo; Una Miaka 18 Na Kuendelea, Wazazi Watakuwa Na Miaka 40 Na Zaidi Na Kwakweli Wana Muda Mchache Wa Kuwa Na Wewe, WAPE UPENDO… Ukizungumza Nao Watie Moyo, Waambie, “NAMSHUKURU MUNGU KUNIPA MAMA/ BABA BORA KAMA WEWE”
HAIPENDEZI KUMPINGIA MCHUMBA WAKO AU MPENZI [KARIBU KILA SAA] AU UJUMBE WA MESEJI [KILA BAADA YA NUSU SAA] WAKATI MAMA YAKO NA BABA YAKO WALIOKUSOTEA NA KUKUVUMILIA KWA MIAKA MINGI UKIWA HUMJUI HUYU “SWEETHEART WAKO” ALIYECHUKUA NAFASI YA KILA KITU!
Kumbuka Ni Mawasiliano Kati Ya Yakobo Na Mama Yake Rebeka Yaliyoleta FURSA YA KUBARIKIWA KWAKE!
Kumbuka Ni Mawasiliano Kati Ya ISAKA NA ESAU Yaliyopelekea KUTAKA KUMBARIKI YEYE NA SI YAKOBO NDUGUYE JAPO WOTE WALIKUWA WATOTO WAKE!

2.Usikae Na Kutumia Kila Kila Unachokipata Wakati Unajua WAZAZI WAKO Hata Hicho Kwao Wakikipata Ni MUUJIZA; Kwa Kidogo Hichohicho JINYIME NA UGAWANE NA WAZAZI WAKO… BARAKA ZIMEFUNGWA KWENYE VITU VIDOGOVIDOGO IKIWEMO HII YA KUGAWANA NA WAZAZI WAKO!
UZOEFU WANGU:
Mwaka Jana Nilikwenda Kijijini Kwa Wazazi Wangu, Huko Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.
Nilikuta THAMANI YA PESA KWAO IKO JUU KULINGANISHA NA HUKU MJINI,
Kilo Ya Kiti Moto Ni Sh.2000 Ilhali Huku Town Mpaka Uwe Na Sh.8000 Hadi 10,000 Kuipata. [Mara 4 Hadi 5 Zaidi]
Maziwa Lita Moja Kule Sh. 500 Wakati Huku Mjini Ni Sh.1500 Na Kuendelea [Mara 3 Na Zaidi].
Kwa Kule, Mtu Ukimpa Sh. 2000 Anashukuru Na KUKUTAMKIA BARAKA ZA KUSHINDILIA Ilhali Pesa Hiyohiyo Kumpa Mgeni Aliyekutembelea Nyumbani Unaona Aibu Kabisa.
Nimetoa Mifano Hiyo Hapo Juu Ili Nikusaidie Wewe Uliyeko Mjini Ujue Kwamba UKIMTUMIA MZAZI WAKO/ MLEZI WAKO WALAU Sh.10,000 Hadi 50,000 Kila Mwezi Utakuwa UMETOA KITU KIKUBWA AMBACHO KWAKE ATAKIHESHIMU NA KUKICHUKULIA KWA UZITO MKUBWA!
Usisubiri Wazazi Wakutafute WAKIWA NA SHIDA INAYOHITAJI PESA; Jizoeze Kutenga Kiasi Cha Pesa Kila Mwezi “KAMA SADAKA YAKO KWA MUNGU” Kupitia “MADHABAHU YA WAZAZI WAKO/ WALEZI WAKO” Na Hata Wao Wasipokutamkia BARAKA; UKIWAPA KWA JICHO LA SADAKA [KWA IMANI] UWE NA UHAKIKA “MUNGU ATAKUSHANGAZA KWA MEMA” Lakini Pia “UHUSIANO WAKO NA WAZAZI/ WALEZI WAKO UTAKUA”
Usijitetee Kwamba Huna Kazi Ya Kuajiriwa Au Bado Uko Chuo: KAMA UNAWEZA KUPATA SADAKA YA KUTOA KILA JUMAPILI, UNAWEZA KUPANGILIA HELA YAKO INAYOBAKI NA “KUTOA SADAKA KUPITIA MADHABAHU YA WAZAZI/ WALEZI”
Wazazi Wetu Hawatakwambia Kama Isaka Alivyomwambia Esau Kwamba, “NILETEE CHAKULA KIZURI NIKIPENDACHO HALAFU NITAKUBARIKI” Lakini Kiukweli, “WANATAMANI WAONE MATUNDA YA UKIFANYACHO” Hata Kama Ni Kutoka Kwenye Hela Ya Kibarua, Au BOOM Kwa Walio Vyuoni.
USIPOWEZA KUWA MSAADA NA BARAKA KWAO UKIWA HAUNA UWEZO MKUBWA WA KIUCHUMI HAUTAWEZA KUFANYA UKIPATA PESA KUBWA; SIKU ZOTE PESA HUJA NA MATUMIZI, HAITATOSHA KAMWE!
Anzia Hapo Ulipo… Mimi Huwa Ninagawana nao kisha Nawaomba Watamke Kitu Kwangu; Na Najua Kwa Sababu Natimiza WAJIBU WANGU WA KIAGANO [KUWATUNZA WA NYUMBANI KWANGU]: Najua Kabisa, SIWEZI KUFA MAPEMA, SIWEZI KUSHINDWA MAISHA, SIWEZI KUKOSA CHAKULA [LABDA KAMA NIMEFUNGA]; MBINGU ZANGU ZIKO WAZI!

3.Kama Hauna Mahusiano Mazuri Na Wazazi Au Walezi Wako Waliokulea Tangu Wazazi Wako Walipokufa, UNAISHI NDANI YA LAANA Na MUDA WOWOTE UNAWEZA KUFA; UTAFANYA KAZI KAMA TEMBO NA KULA KAMA SISIMIZI, MAMBO YAKO HAYATAKWENDA!
Inawezekana WAZAZI/ WALEZI NDIO WALIKUKOSEA Na Wewe Ukaamua KUKATA MAWASILIANO NAO… Kama Kweli WALIKUANGAIKIA NA KUGUSA MAISHA YAKO, NDUGU KATENGENEZE NAO MAMBO YAKO Tofauti Na Hapo Hautaona Matokeo Ya UTOAJI WAKO [FUNGU LA KUMI NA SADAKA NYINGINE], HAUTAONA MATOKEO YA MAOMBI YAKO… LAANA ISIYO NA SABABU NDIYO HAIMPATI MTU; ILA KAMA INA SABABU ITAKUPATA NDUGU; HAUWEZI KUWA MJANJA KULIKO NENO LA MUNGU… YOTE YATAPITA LAKINI NENO MUNGU LINASIMAMA MILELE MBINGUNI!

NB: Usiache Kutuma Sadaka Yako Kwa Ajili Ya Huduma Ya Injili Pasaka Mkoani Tabora, Tutakuwa Na Timu Ya Wainjilisti 50, Na Itakuwa Kwa Siku 6, Tunahitaji Sana SADAKA YAKO, TABORA KWA YESU.
Tuma Kwa Mhazini, Eng Martha Shitindi [M-PESA: 0754 711 519]

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: