NIMEIOMBEA WIKI YAKO

Siku NJema

Siku Njema

-Hautapoteza Ndugu Au Watu Wako Kwa Ajali, Magonjwa Au Vifo Visivyo Amriwa Na Serikali Ya Mbinguni.
MWIZI [IBILISI] HATACHINJA WATU WAKO WIKI HII (Yohana 10:10).

-Kila Changamoto Ya Kimaisha Uliyokuwa Unapitia HAITAVUKA WIKI HII NA WEWE, ITABAKI WIKI HII
“…MKIISHA KUTESWA KWA MUDA KIDOGO [HAITAZIDI KIDOGO], YEYE MWENYEWE [MUNGU NA SI MALAIKA] ATAWATENGENEZA, NA KUWATHIBITISHA, NA KUWATIA NGUVU” (1Petro 5:10).

-Kila Haki Yako Uliyocheleweshewa Au Kuzungushwa Kwa Muda Mrefu UTAIPATA NDANI YA WIKI HII
“UTATHIBITIKA KATIKA HAKI, UTAKUWA MBALI NA KUONEWA” (Isaya 54:14).

-Wewe Ambaye ULIKUWA UNASUASUA KIROHO [ULIRUDI NYUMA] NA UKAKOSA AMANI NA NGUVU YA KURUDI TENA NA KUSIMAMA, UTASIMAMA TENA NA KUIMARIKA
“MWENYE HAKI HUANGUKA MARA SABA AKAONDOKA TENA; BALI WASIO HAKI HUKWAZWA NA MABAYA” (Mithali 24:16).

-Wewe Unayewaza Aidha KUPANUA MRADI/ BIASHARA YAKO TOKA SEHEMU MOJA KWENDA NYINGINE, HII NI WIKI YAKO
“ZAENI MKAONGEZEKE [BE FRUITFUL AND MULTIPLY]” (Mwanzo 1:28)
“PANUA MAHALI PA HEMA YAKO, NA WAYATANDAZE MAPAZIA YA MASKANI YAKO; USIWAKATAZE; ONGEZA UREFU WA KAMBA ZAKO; VIKAZE VIGINGI VYA HEMA YAKO” (Isaya 54:2).

-Wewe Mwenye SHAUKU NA KIU YA KUTUMIWA NA MUNGU KWENYE HUDUMA NA UTUMISHI NA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU [WEWE ULIYEKUWA UNAMTAFUTA MUNGU KWA AJILI YA HAYA], WIKI HII UTAANZA KUONA MTEMBEO WAKE KWAKO
“YEYE ANIAMINIYE MIMI, KAZI ZOTE NIFANYAZO, YEYE NAYE ATAFANYA, NAAM KUBWA KULIKO HIZI ATAFANYA MAANA MIMI NAKWENDA KWA BABA [NA NATAMANI WABAKI WATU WA KUENDELEA KUUJENGA UFALME KATIKA UWEZA NA NGUVU ILEILE NILIYOTEMBEA NAYO]” (Yohana 14:12).

Itakuwa Amani Kwako, Mungu Atakupa Habari Njema [NENO LAKE] Kwenye Kila Habari Mbaya!
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “NIMEIOMBEA WIKI YAKO
  1. JOSEPH LUHIGA says:

    hakika neno hili ni la kwangu mimi ,na wote wa nyumbani kwangu .UINULIWE MUNGU ULIYEMTUMA MJUMBE WAKO KWA AJILI YANGU KTK JINA LA YESU .AMINA

  2. Elisha says:

    Hakika Mungu akuinue na kukuongeza, natamani sana kutumika ktk shamba la Bwana naomba maombi yenu

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: