NDANI YAKE


Umewahi Kumwona Kuku Anayejaribu Kumdonoa Panzi Ndani Ya Chupa Ya Soda??
Yule Panzi Anakuwa Na Mashaka Na Hofu Kila Mara Kuku Anapochukua Hatua Ya Kuikaribia Chupa Na Kujaribu Kudonoa; Akili Ya Panzi Inadhani Kwamba ULE NI MWISHO WAKE…. Lakini Kwa Upande Wa Pili; Kuku Anapomuona Panzi Ndani Ya Chupa Anafurahi, Anadhani Tayari Amepata Kitoweo, Anaisogelea Ile Chupa Kwa Kiburi Na Uchu Halafu Anadonoa; Halafu Anashangaa Mdomo Wake Umegonga “KITU KIGUMU” Halafu Anarudi Nyuma ANAJIPANGA TENA NA KUCHUKUA HATUA YA KUJARIBU NA KUJARIBU Mpaka Pale ANAPOKUBALI KWAMBA HAIWEZEKANI KUMPATA “Yule Panzi Ndani Ya Chupa Japo Anamwona Na Anamtamani”

TUNACHOJIFUNZA HAPA:
JAMBO LA KWANZA:

Panzi Ni Mwanadamu Wa Kawaida [Kama Mimi Na Wewe] Ambaye Kutokana Na Dhambi AMEKUWA MNYONGE Kwa KUKU [IBILISI]!

Huyu Panzi [Mwanadamu Mwenye Udhaifu] Akiwa Nje Ya Chupa [YESU KRISTO] Anakuwa DHAIFU, MNYONGE NA WA KUONEWA NA ADUI YAKE KUKU [SHETANI]… Lakini Akichukua UAMUZI WA BUSARA WA KUINGIA KWENYE CHUPA [YESU KRISTO] Kupitia MLANGO MWEMBAMBA WA CHUPA [WOKOVU] Tayari Anakuwa Amepata UHAKIKA WA USALAMA WA MAISHA YAKE Ilimradi ASITOKE NDANI YA CHUPA [ASIUACHE WOKOVU NA KURUDI TENA DHAMBINI] Maana Akirudi Tu Nje ATAKUWA CHAKULA CHA KUKU [IBILISI]!

JAMBO LA PILI:

Chupa INAONESHA [TRANSPARENT] Hivyo Panzi Anamuona Kuku Na Kuku Anamuona Panzi; Wote Wanaonana!

Ndivyo Ilivyo KWA MTU ALIYEOKOKA NA KUINGIA NDANI YA YESU [CHUPA] Ataendelea KUMWONA ADUI YAKE SHETANI NA VITISHO VYAKE KUPITIA Majaribu, Changamoto, Matatizo Na Hila Zote Za Yule Adui! Na Pia ADUI Naye Ataendelea Kumwona Huyu MTU NDANI YA CHUPA Na ATAFANYA KILA HILA NA MBINU “Kumtisha, Kumtia Hofu, Kumwogopesha Na Ikiwezekana Huyu Mtu [PANZI] Aruke Na Kutoka Ndani Ya Chupa Halafu AMAKAMATE KWA URAHISI”
Usalama Wa Panzi Ni KUAMINI UBORA, UIMARA NA NGUVU YA UKUTA WA CHUPA Katika Kudhibiti Kila SHAMBULIO LA ADUI KUKU!
Kama Panzi HATAAMINI Bali Akayumbishwa Na HISIA ZAKE Badala Ya UHAKIKA ALIOPEWA NA NGUVU ZA UKUTA WA CHUPA Atajikuta Anapata HOFU Na Kuanza KURUKARUKA Na Mwishowe ATATOKA NDANI YA CHUPA NA KUWA CHAKULA CHA Adui Yake KUKU!!
Hiki Ndicho Kinachowakuta WALIOOKOKA WENGI Wanatishwa Na MNG’URUMO ZA SIMBA “AZUNGUKAYE AKITAFUTA MTU AMMEZE” Hivyo WANAINGIWA NA MASHAKA NA HOFU Wanasahau AHADI YA UKUTA WA CHUPA [NGUVU YA MUNGU NA NENO LAKE] Na Wanaanza KURUKARUKA KILA ADUI AKIJA KUDONOA Na Mwishowe WANAJIKUTA TAYARI WAMETOKA NJE YA CHUPA NA KUWA CHAKULA CHA ADUI YAO IBILISI!!!
Lakini KUNA PANZI WALIOELEWA [WALIOKOMAA] Hawa WANAAMINI UKUBWA NA NGUVU YA UKUTA WA CHUPA; Ndiyo WANAMUONA ADUI NA KILA ANALOJARIBU KUWATISHA NALO Lakini WANAJUA KWAMBA, “ILI AWAPATE LAZIMA AIVUNJE CHUPA” Kitu Ambacho Mdomo Wa Kuku HAUWEZI!
Hawa WANAZIAMINI AHADI ZA NENO LA MUNGU BILA KUJALI NINI ADUI ANALETA KINYUME CHAO… Wanajua Ya Kwamba, “BWANA NI NGOME NA MWAMBA WAO” Wanaelewa HAKUNA CHA KUWAANGUSHA WALA KUWADHURU MAADAMU WAMEDUMU KATIKA UTULIVU NA KUTOTOKA NDANI YA CHUPA!!!

Asomaye Na Afahamu.
“HATA IMEKUWA MTU AKIWA NDANI YA KRISTO YESU, YA KALE YAMEPITA; TAZAMA! YOTE YAMEKUWA MAPYA” (2Kor 5:17).
“NDANI YAKE TUNAISHI, TUNAKWENDA NA KUWA NA UZIMA WETU” (Matendo 17:28).
“NAYE ALITUOKOA TOKA NGUVU ZA GIZA; AKATUHAMISHA NA KUTUINGIZA KATIKA UFALME WA MWANA WA PENDO LAKE” (Wakolosai 1:13).

Usiache Kutuma Sadaka Yako Kwa Ajili Ya Huduma Ya Injili Pasaka Mkoani Tabora, Tutakuwa Na Timu Ya Wainjilisti 50, Na Itakuwa Kwa Siku 6, Tunahitaji Sana SADAKA YAKO, TABORA KWA YESU.
Tuma Kwa Mhazini,
Eng Martha Shitindi
[M-PESA: 0754 711 519]

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “NDANI YAKE
  1. Elisha says:

    Be blessed mwl.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: