KWA KILA ALIYEOKOKA:

Unapookoka, MAJIRA NA MUDA WAKO PIA Unageuka Na Kuwa Tofauti Na Wa WATU WENGINE Japo Unaendelea Kuwa Na Asubuhi Na Jioni, Usiku Na Mchana Ulio Sawa na Wa Watu Wengine WALIOKO NJE YA KRISTO YESU!

i)Unapookoka, Kuanzia Siku Ile Ni “MWANZO WA MIAKA KWAKO”

Wana Wa Israeli Walipokaribia Kukombolewa Toka UTUMWANI MISRI Ilimwagwa DAMU YA KONDOO AITWAYE “PASAKA” Na Musa Akatangaza Akasema, “USIKU HUU NI MWANZO WA SIKU, NA MIEZI NA MIAKA KWENU” (Kutoka 12) Akiwa Na Maana “NI MSIMU MPYA KWAO TANGU USIKU ULE WALIPOPAKA DAMU YA PASAKA”
Hiki Ndicho Kinachotokea Kwa Yeyote Anayeamua “kuikubali kazi damu ya Yesu na kazi ya msalaba” Maana Kwenye AGANO JIPYA, Yesu Kristo Anaitwa “PASAKA WETU”
Ghafla “KWENYE ULIMWENGU WA ROHO” Kunatokea Mabadiliko Ya MAJIRA NA MUDA WAKE…. Anaanza Kutembea Ndani Ya Muda WA MUNGU Ambao Ndani Yake Kuna MAMBO SABA Ambayo YESU KRISTO AMEPEWA KWA KUMWAGA DAMU YAKE KUTUNUNUA: UWEZA [POWER], UTAJIRI [RICHES], HEKIMA [WISDOM], NGUVU [STRENGTH], HESHIMA [HONOR], UTUKUFU [GLORY] Na BARAKA [BLESSINGS] (Ufunuo 5:8-13).
Hivi Vitu Saba ALIVYOPEWA YESU Amevipokea KWA AJILI YA “MWILI WAKE [KANISA- MIMI NA WEWE” Maana Sisi TULIOOKOKA TU VIUNGO VYA MWILI WA KRISTO NA KRISTO NI “KICHWA CHA KANISA” Na Kama Tujuavyo “YALIYO YA KICHWA NI YA MWILI PIA”
Mtu Anapookoka Anaingia Kwenye Miaka Ya UWEZA, UTAJIRI, HEKIMA YA KIMUNGU, NGUVU, HESHIMA, UTUKUFU NA BARAKA!
Wengi MLIOOKOKA HAMYAJUI HAYA Na Kwa Sababu Hiyo HAMNA MATARAJIO YA KUWA NA MAJIRA NA NYAKATI Zilizojaa Haya; Mnaishi Kwenye Majira Na Nyakati Ambazo Watu Wengine Wanaishi, MNAKWAMA!!!

ii) Unapookoka, “KILA MWAKA KWAKO UNAKUWA NI MWAKA ULIOKUBALIWA NA BWANA”

Yesu Aliposimama Kutangaza KAZI ILIYOMLETA DUNIANI Alisema AMEKUJA KUTANGAZA “MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIKA” (Luka 4:19).
Alisema “AMEKUJA ILI TUWE NA UZIMA KISHA TUWE NAO TELE” (Yohana 10:10b).
Kwa Lugha Nyepesi; YESU AMKUJA KUTANGAZA KWA KILA ALIYEMWAMINI NA KUMPOKEA KUWA “KILA MWAKA UMEJAA UTELE NA UMEKUBALIWA NA BWANA” Lakini Ili Tuweze Kuuona Huo UTELE Ndiyo Maana Anatangulia Kusema “AMEKUJA ILI VIPOFU WAPATE KUONA TENA” (Luka 4:18), Akiwa Ana Maana Kwamba “AMEKUJA KUYAFANYA MACHO YA NDANI YA KWETU YAPATE KUONA FURSA ZA KUPATA BARAKA NA MEMA NDANI YA KILA MWAKA ANAOTUPA KUISHI” Ili “TUYASIMULIE MATENDO YAKE MAKUU” Na “KUTANGAZA YA KUWA BWANA NI MWEMA NA AMEJAA ADILI”
Kwa Walio Ndani Ya Yesu Hakuna MWAKA MBAYA, MWAKA WA TABU, MWAKA WA SHETANI, MWAKA WA MAGUMU Na Mingine Ya Aina Hiyo Maana Kila MWAKA NI MWAKA TOKA MBINGUNI; NI MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA!!!

Nitoke Kwa Yesu Niende Kwa Nani?
Usiache Kutuma Sadaka Yako Kwa Ajili Ya Huduma Ya Injili Pasaka Mkoani Tabora, Tutakuwa Na Timu Ya Wainjilisti 50, Na Itakuwa Kwa Siku 6, Tunahitaji Sana SADAKA YAKO, TABORA KWA YESU.
Tuma Kwa Mhazini,
Eng Martha Shitindi
[M-PESA: 0754 711 519]

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: