Kwenye Injili Ya Mathayo Sura Ya Kwanza

Ruth na Naomi

**JANA YAKO HAIWEZI KUMZUIA MUNGU KUKUTUMIA KWA MAKUBWA**

“Kuna Wanawake Watatu Ambao Historia Yao [Jana Yao] Si Nzuri Na Ilikuwa Inawazuia Kwa Mazingira Ya Kawaida Kuja Kuwa Watu Muhimu Na Kujumuishwa Kwenye ORODHA YA UKOO WA YESU Lakini NEEMA YA MUNGU Na KUSUDI LA MUNGU [Lisilozuiwa Na Mtazamo Wa Wanadamu Wala Jana Yao] Viliwapa Nafasi Kuwa Sehemu Ya Kupitisha UKOO WA YESU; Wanawake Hawa Ni RAHABU [Aliyekuwa Kahaba Katika Mji Wa Yeriko], RUTHU [Aliyekuwa Mtu Wa Moabu, Asiyekuwa Mwisraeli], Na Beltsheba [Mke Wa Huria Mhiti, Mke Wa Ziada Wa Daudi Na Mama Yake Suleimani]” (Mathayo 1:5-6).

TUNACHOJIFUNZA HAPA:

1.Mungu Hazuiwi Na Jana Yako [Past] Wala Chimbuko Lako [Background] Anapotaka Kukutumia Kuwa Sehemu Ya Mipango Na Mambo Yake Makubwa Hapa Duniani.
-Rahabu Alikuwa Kahaba Maarufu Lakini Bado Mungu Alimtumia
-Ruthu Alikuwa Mtu Wa Moabu Lakini Mungu Alimtumia
-Beltsheba Alikuwa Mke Wa Huria, Mke Aliyepatikana Kwa Hila Kwa Kumuua Mmewe Huria Mhiti Lakini Mungu Alimtumia Kupitisha Vitu Vyake

2.Mungu Hutumia Vitu Vinyonge Ili Kuvipinga Na Kuviaibisha Vyenye Nguvu; Hutumia Vitu Vipumbavu Ili Kuviaibisha Vyenye Hekima

3.Mawazo Na Njia Za Mungu Ni Tofauti Na Mawazo Na Njia Za Mungu; Mungu Hatazami Kama Wanadamu Watazamavyo, Mungu Hutazama Ndani [Utu Wa Ndani Wa Mtu] Bali Wanadamu Huangalia Sifa Za Nje

4.Yasiyowezekana Kwa Wanadamu Yanawezekana Kwa Mungu; Inawezekana Rahabu Hakuwahi Kuwaza Kuwa Sehemu Ya Mpango Mkubwa Wa Mungu Na ALIONA HAIWEZEKANI Na Kadri MUDA ULIVYOZIDI AKIDIDIMIA KWENYE UKAHABA Ndoto Zake Zilianza Kufutika Au Kufa Lakini Mungu ALIMTENGENEZEA “APPOINTMENT” NA WAPELELEZI Ambao Walimuunganisha Na DESTINY YAKE
Mungu Anaweza Kufanya Hata Yale Uliyoyakatia Tamaa, Hata Zile Ndoto Ambazo Kwa Akili Yako Huoni Uwezekano Wa Kuzitimiza; Beltsheba Alipoolewa Na Huria Mhiti NDOTO YAKE YA KUWA “MALKIA [FIRST LADY]” ILIPOTEA KICHWANI MWAKE Lakini BADO MUNGU ALIMWONA AKIWA “MAMA WA MFALME SULEIMANI”
Mungu ANAWEZA KUFANYA YALE AMBAYO UMEYAKATIA TAMAA NA AKILI YAKO HAIKUBALI KWAMBA YANAWEZEKANA!

SIFA KUBWA WALIYOKUWA NAYO HAWA WANAWAKE:

-Walikuwa Ni Wanawake Wa IMANI

Walikuwa WANAMWAMINI MUNGU KIASI KWAMBA HAWAJALI KITU KINGINE CHOCHOTE, MAZINGIRA AU HALI WALIZOMO
*Rahabu Alimwamini Mungu Akiwa Bado Kahaba Na Kuamua Kumng’ang’ania MUNGU WA ISRAELI ALIYEKUWA ANASIKIA HABARI ZA MATENDO YAKE YA AJABU ALIYOWATENDEA HUKO NJIANI TOKA MISRI; NA ALISUBIRIA KWA HAMU WAJE ILI HUYO MUNGU AWE MUNGU WAKE.
*Ruthu Alikuwa Na Imani Kubwa Sana Kiasi Kwamba ALIMNG’ANG’ANIA MAMA MKWE WAKE [NAOMI] Akisema “NITAAMBATANA NA WEWE, MUNGU WAKO ATAKUWA MUNGU WANGU NA WATU WAKO WATAKUWA WATU WANGU” (Ruthu 1:16-17)

-Hawakuwa Wanawake WANAOYUMBISHWA NA HALI ZAO ZA WAKATI ULIOPO [They Where Not Moved By Their Current Situations]

*Rahabu Hakubabaishwa Na Ukahaba Wake Aliokuwa Anapitia Bali Kwa Imani Aliingia AGANO NA MUNGU WA WALE WAPELELEZI
*Ruthu Hakubabaishwa Na Ujane Wake, Hakubabaishwa Na Utaifa Wake [Mmoabu], Wala Hakubabaishwa Na Ukweli kwamba Hakuwa Na AGANO NA MUNGU WA ISRAELI; Bali Aliamua KULIWEKA AGANO Akisema, “MUNGU WAKO [NAOMI], MUNGU WA ISRAELI ATAKUWA MUNGU WANGU NA WATU WAKO [WAISRAELI] WATAKUWA WATU WANGU” (Ruthu 1:16).

Kama Ni Mwanafunzi Kweli, Naamini Mungu Amekupa Kitu Kikubwa Kupitia Ujumbe Huu; JENGA MAISHA YAKO KWENYE UKWELI HUU NA MUNGU ATAKUTOKEA NA KUKUTENDEA MEMA KAMA HAWA WANAWAKE TULIOJIFUNZA KWAO!

#Mfungo_Wa_Mathayo
Mwl D.C.K
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: