Mme wa Kweli mwenye Malengo ya kuwa na Ndoa Bora

Mme wa Kweli

1.Atajua Ya Kwamba MKE WAKE NDIYE MZAZI, NDUGU, RAFIKI NA MTU WAKE WA KARIBU Kabla Ya Mtu Mwingine Yeyote
“MKE WAKE NI KAMA MWILI WAKE MWENYEWE”

2.Atakuwa Tayari Kumshirikisha Mke Wake Kila Jambo Ambalo Hata Yeye Hawezi Kujificha: Kama Kuna Kitu Cha Kumficha Mkewe Ni Kile Ambacho Hata Yeye Amejificha Au Kile Alichoambiwa Na Mungu Asiseme Au Kumshirikisha Yeyote
“MME WA KWELI HANA SIRI KATI YAKE NA MKEWE”

3. Anajua Ameamua Kuchukua Hatua Ya Kumuoa Huyo Mwanamke Hivyo Analazimika KUACHANA NA WAZAZI WAKE NA KUAMBATANA NA MKEWE…. Yaani Lazima Ajue Msimu Wa Kuwa MTOTO WA MAM NA BABA UMEISHA NA MKE AMEKUJA PAHALA PAO
NB:Haimaanishi Wazazi Watelekezwe Au Wasiheshimiwe, Hapana! Ina Maana Mke Wake Anakuwa Na a Hadhi Na Haki Kibiblia Kabla Ya Wazazi, Japo Wazazi Watabaki Kuwa Wazazi

4.Anajua Kama Ndoa Itakwama Au Kuyumba, Mtu Wa Kwanza Kuwajibishwa Au Kulaumiwa Ni Yeye Mme Kama KICHWA
“MME NDIYE MBEBA MAONO NA ALIYEPOKEA WAZO LA KUANZISHA NDOA, NA AMEBEBA RAMANI NZIMA YA HIYO NDOA, HATUA NA KILA KINACHOPASWA KUWA AU KUTOKUWA KWENYE NDOA”

5.Anajua Swala La MALEZI Si La Mke Peke Yake Bali Ni La WAZAZI WOTE WAWILI: Hivyo Anajua KANUNI, TARATIBU NA NJIA ZIPASAZO KUMLEA MTOTO KIROHO, KIMWILI, KIUCHUMI Nakadhalika Na Hivyo ANASIMAMA NA MKEWE [Kwa Muda, Vitendo, Maneno, Gharama Na Uwajibikaji] KWENYE MALEZI
“MME WA KWELI HAWEZI KUACHA WATOTO WAKULIE MIKONONI MWA MTU YEYOTE KISA NI NDUGU AMA NI MFANYAKAZI WA NDANI BILA UHAKIKA WA MTAZAMO, HALI YAO YA KIROHO, LUGHA YAO KUHUSU MAISHA NA IMANI”
Mme Wa Kweli Hawezi Kusingizia Kazi Au Wingi Wa Majukumu Kama Kigezo Cha Kutopata Muda Na Watoto Wake.
“KWA MME WA KWELI FUTURE YA WATOTO WAKE NI YA MUHIMU KULIKO KAZI AU HUDUMA AU CHOCHOTE; ANAJUA HUO NDO WAJIBU WAKE WA KWANZA”

6. Anajua Kwamba NI WAJIBU WAKE KUMPENDA MKE WAKE Na KUENDELEA KUMPENDA SIKU ZOTE “Kama Siku Ya Harusi” Kwa Kubeba MSAMAHA, UVUMILIVU, KUUCHUKULIA UDHAIFU WA MKEWE, KUPINGA WAZO AU CHOCHOTE KINACHOZUNGUMZIA AU KUTISHIA KUVUNJIKA KWA NDOA YAKE, KUMWOMBEA MKE WAKE ADUMU KUFANYA SEHEMU YAKE KILA SIKU
“MME WA KWELI ANAJUA ANAMWOA MWANADAMU MWENZIE NA SI MTU WA SAYARI NYINGINE, HIVYO ANAPASWA KUMPENDA KAMA YESU KRISTO ANAVYOLIPENDA KANISA SIKU ZOTE NA KWA KIWANGO KILEKILE BILA KUJALI SISI [KANISA] TUMEPATIA AU TUMEKOSEA”

7.Anajua Kwamba NI WAJIBU WAKE KUMTUNZA MKEWE NA KUMTIMIZIA KILA MAHITAJI YAKE KAMA MWILI WAKE MWENYEWE
NI WAJIBU WA MME KUMFANYA MKEWE AONEKANE MALKIA
“HATA KAMA MKE ANA UWEZO KIFEDHA, BASI MME WA KWELI ATAMSAIDIA KUCHAGUA VITU BORA VYA KUMFANYA MKEWE AWE KIOO KWELI, WALAU ATAMSINDIKIZA DUKA LA NGUO NA KUMWAMBIA HII IMEKUTOA MKE WANGU, HII HAPANA MAMA”

8.Anajua Ya Kwamba Ni Wajibu Wake KUMLINDA MKEWE Dhidi Ya Wazazi, Ndugu, Marafiki, Au Chochote.
“MME WA KWELI ATAPANGUA KILA NENO, SHUTUMA NA SHAMBULIZI DHIDI YA MKE WAKE; ATALINDA HADHI NA HESHIMA YA MKEWE”
Hata Kama Kinachosemwa Ni Kweli, HATAUNGANA NA WENGINE KINYUME CHA MKEWE Bali ATAMLINDA MKEWE NA KUYAZUNGUMZA NA MKEWE NA KUYAREKEBISHA WAKIWA PEKE YAO CHUMBANI.

9.Anajua Ya Kwamba YEYE NI KIONGOZI-RAFIKI WA MKE WAKE Hivyo ANAMWONGOZA NA KUMWELEKEZA KWA UPENDO NA HALI YA URAFIKI WA KIWANGO CHA JUU.
“MME WA KWELI ANAJUA YA KWAMBA NI MBEBA MAONO NA MKEWE NI MSAIDIZI ANAYEPASWA KUPOKEA MAELEKEZO TOKA KWAKE MARA KWA MARA ILI WADUMU KWENYE MAONO ALIYOPEWA NA MUNGU”

10. Anajua Ya Kwamba Anapaswa Kujenga Msingi Wa Vizazi Vingi, Hivyo ANAKUWA MAKINI KUHAKIKISHA ANAKUWA KIOO KWA WANAE Kupitia TABIA ZAKE, MWENENDO, MANENO YAKE, MTAZAMO WAKE Nakadhalika Maana Anajua WANAE WANAJIFUNZA KWAKE… ATACHUNGA HALI YAKE YA KIROHO SANA NA KUWAUNGANISHA WANAE NA MUNGU WA KWELI NA KUWAHIMIZA KWENYE MASWALA YA UFALME WA MUNGU; ATAFANYA JUU CHINI WANAE WAMJUE MUNGU WAKE NA KUMTUMIKIA BILA KUSITASITA WALA KUGEUZWA NA CHOCHOTE AU YEYOTE, ILI ATAKAPOKUWA AMEONDOKA [AMETANGULIA] AWAACHIE MTAJI WA UHAKIKA KWA LEO NA KESHO YAO!

*Kama Umeoa, Chukua Hizi Uzichape Na Kuanza Kuzifanyia Kazi
*Kama Umeolewa, Zichape Na Umpelekee Mmeo Kama Zawadi
*Kama Haujaoa Kama Mimi, Zichukue Na Uzichape Uzibandike Chumbani Kwako, Uanze Kuzifanya Tabia Yako Na Mtazamo Wako Kama Mme Mtarajiwa Wa Kesho.

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo, ndoa

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: