UKITAKA

Mathayo 8:3

Mathayo 8:3

“Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Na tazama, AKAJA MTU MWENYE UKOMA akamsujudia, akisema, Bwana, UKITAKA, WAWEZA KUNITAKASA. Yesu akanyoosha mkono, akamgusa, akisema, NATAKA; TAKASIKA. Na mara ukoma wake ukatakasika” (Mathayo 8:3).

TUNACHOJIFUNZA

Huyu mtu mwenye ukoma, aliamini na alijua ya kwamba “YESU ANAWEZA KUTATUA” shida ya ukoma aliyoteseka nayo, ila hakuwa na uhakika kama “YESU ANATAKA” kumponya au la!

Hivi ndivyo ilivyo kwa wengi wenu, mnajua Yesu Kristo anaweza kutatua changamoto mnazopitia, lakini MMEMRUHUSU SHETANI APANDE UONGO KWENYE AKILI NA MIOYO YENU kwamba HUENDA “YESU HATAKI” Maana umeliombea hilo swala sana, umefunga sana, umeombewa sana, umetoa sadaka maalum kwa ajili ya hilo lakini hujaona matokeo.
Kumbuka hata huyu mwenye ukoma ALIMSUJUDIA YESU lakini ukoma haukuondoka; Alimwabudu Yesu lakini alibaki vilevile.
Tatizo Lilikuwa kwenye AKILI, MTAZAMO NA FIKIRA ZAKE, Yeye Alidhani YESU HATAKI KUMPONYA Mpaka pale alipochukua hatua ya kumwambia kwa kubahatisha na kusema “UKITAKA, WAWEZA KUNITAKASA” Kwa lugha nyepesi alikuwa anasema, “NINAAMINI HILI TATIZO LANGU UNALIWEZA ILA SINA UHAKIKA KAMA UNATAKA KUNITAKASA HUU UKOMA AU LA”
Biblia inatuambia, “TUNAPOMWENDEA MUNGU, TUAMINI YA KWAMBA YUPO, NA YA KUWA ATATUPA HAKIKA KILE TUNACHOKIHITAJI KWAKE” (Waebrania 11:6).
Unaweza kusogea mbele za Mungu, kwa maombi, sadaka, kufunga, kuombewa, kusifu na kuabudu LAKINI Usipojua kwamba ANATAKA HAKIKA KUKUSAIDIA NA KUGEUZA HALI YAKO, HAUTAPATA MATOKEO NA UTAISHIA KUONA WENZIO WANASHUHUDIA MATENDO MAKUU YA MUNGU!
Badili Mtazamo Wako, Geuza Fikira zako; “YESU KRISTO ANATAKA SASA HIVI KUKUSAIDIA NA KUKUTENDEA HILO UNALOTAKA”
Ingia kwenye maombi kwa ujasiri na ukiwa na uhakika na utapata muujiza wako!
#Mfungo_Wa_Mathayo
Tafadhali wewe unayefaidika na mafundisho haya, Tuma sadaka yako kwa ajili ya HUDUMA TULIYONAYO MKOANI TABORA, MWEZI UJAO WA 4, TAR 16-21.
Tutakuwa na Timu Ya Watu 50 Na Inahitajika Milioni 8, Shirikiana nasi kwa hicho kidogo ulichopewa na Mungu.
Tuma Sadaka yako kwa Mhazini:
Eng Martha Shitindi
M-PESA: 0754 711 519

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: