KWA WALIOOLEWA NA WANA MPANGO WA KUTUNZA NDOA ZAO

https://i2.wp.com/www.bolegaindia.com/images/gossips/married_women_post_1326187601.jpg

waliolewa

1.Lazima Ujue Kwamba Wewe Ni MKE Na Ni Wajibu Wako KUSHUKA NA KUMTII MMEO
“Enyi Wake Watiini Waume Zenu Kama Kanisa Linavyomtii Kristo Yesu”

2.Lazima Ujue Kwamba MMEO NI KIONGOZI WAKO, Haijalishi Uko SMART KIASI GANI, Mme Anabaki Kuwa Mme… Hata Ukiwa Rais Wa Nchi, Ukirudi Nyumbani UNAKUWA MKE WA MTU; Hapo Elimu, Nafasi, Cheo, Umaarufu Havifanyi Kazi.
“Mme Ni Kichwa Cha Mkewe… Hata Kama Kichwa Hakina Akili Bado Ni Kichwa, Na Unadhirisha Usivyo Na Akili Zaidi Kwa Kukubali Kuolewa Na Mjinga… Umeshaolewa, Umegundua Ni Mjinga, Ishi Naye Kwa Akili Na Msaidie Kujua Nafasi Yake Na Muache Akae Kwenye Nafasi Yake”

3.Usiwe Mjinga Kiasi Cha Kutoka Nje Kwenda Kueleza Mapungufu Ya Mmeo; Midomo Ya Wanawake Wengi Imevunja Ndoa Zao… Hao Mashoga, Marafiki, Ndugu Zako Watakusikiliza Ila Hawatatatua Shida Zako Bali Watachangia Kuibomoa.
“Mwanamke Mpumbavu Huibomoa Nyumba Yake Kwa Mikono Yake Mwenyewe”

4.Simama Kidete Na Umlinde Mmeo Anaposhambuliwa… Chako Ni Chako Hata Kama Kina Mapungufu… Mtete Mmeo Mbele Za Watu Na mkosoe Mnapokuwa WAWILI CHUMBANI.
“Naye Abigaili Akamwangukia Daudi Akamfichia Mmewe Aibu Na Kumlinda Asiuawe”

5.Mmeo Akitoka Nje Ya Ndoa Kutafuta Nyumba Ndogo, Kabla Ya Kutafuta Pepo Aliyemwingia, Tafuta Mlango Ambao Huyo Pepo Ameutumia… Inawezekana Ulipokuwa Single Ulikuwa UNAJIPENDA, Unapiga PAMBA MPAKA BASI, Umeolewa UNAJIVALIA KIVYOVYOTE [shauri Yako]; Inawezekana Ulipokuwa Hujampata LUGHA YAKO ILIKUWA SUPER, Lakini Sasa Unajibu Unavyojisikia [Shauri Yako]; Inawezekana Ulipokuwa Hujavaa Pete ULIKUWA UNAWAPENDA NA KUWATHAMINI NDUGU NA WAZAZI WAKE, Lakini Ulipoingia Tu, Ndio Umeona KARAHA YA MAWIFI NA NDUGU WA MME [shauri yako]… INAWEZEKANA NI KITANDANI [Biblia Inasema MKE HANA UMILKI JUU YA MWILI WAKE ISIPOKUWA MMEWE] Usisahau Hii Ni Ya Muhimu Sana, UKISEMA ANAKUCHOSHA “KWA KUKUJIA MARA KWA MARA” [Shauri Yako]!
“Mungu amefanya jambo jipya duniani ya kwamba MWANAMKE ATAMLINDA MWANAUME”

6.Usisahau Kwamba Ni Wajibu Wa Mke KUAMKA KABLA USIKU HAUJAISHA NA KUPIGA KAZI ZOTE ZA MUHIMU NDANI… Biblia Imesema Hili, MITHALI 31 [BIBLIA HAISEMI NI KAZI YA HOUSE GIRL; UKIMPA HOUSE GIRL AZIPIGE UMEMPA NAFASI YA KUWA MKE BADALA YAKE, MAANA NI KAZI ZA MKE MWEMA HIZI]
“Mke Mwema Huamka Kabla Usiku Haujaisha Ili Kuweka Sawa Mambo Ya Nyumbani Mwake Kwa Siku Inayoanza Baada Ya Usiku Huo”

7.Ni Lazima MKE AWE NA KITU CHA KUFANYA… Ukiwa tu GOLIKIPA, Hakuna VIUNGO Wala MABEKI Kukulinda UTAFUNGWA MAGOLI.
Mke Ambaye ANA AKILI NZURI Lazima AWE NA KITU CHA KUINGIZA KIPATO…Afanye Kazi Kwa Mikono Yake Mwenyewe, Na Kutunza Watu Wa Nyumbani Kwake, MITHALI 31 IKO WAZI KAMA UNATAKA NDOA YAKO ISIMAME, UKIKWEPA IMEKULA KWAKO!
“Mke Mwema Hufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, na kuwapa chakula watu wa nyumbani kwake

8.Mke Mwenye Hekima ANAULINDA UHUSIANO NA MAMA MKWE [Hii Ni Zawadi Ya Pekee Kwa Mmeo], Moyo Wa mtoto Wa Kiume Humpenda Na Kumjali Mama, Usisahau Hii Itakusaidia, NI SILAHA MUHIMU YA VITA!
SOMA KITABU CHA RUTHU Utaona Ruthu Alivyocheza Kete Zake Vizuri Na Kuuteka Moyo Wa Mama Mkwe.
“Mke Mwenye Busara Huhakikisha Anauteka Moyo Wa Mmewe Kwa Kuwa Kipenzi Cha Mama Mkwe”

9.Mke Mwenye Busara Anajua Ya Kwamba Ni Jambo Moja Kuwa Mzazi [Mwanamke Aliyezaa] Na Ni Jambo Jingine Kuwa MAMA.
Kuzaa Ni Kuporomosha Kiumbe Baada Ya Miezi 9 Aliyoweka Mungu Lakini Kuwa Mama Kunategemea MALEZI SAHIHI NA BORA Yatakayoweka Msingi Mwema Na Bora Usiofutika Kwa Mwanao.
“Mke Mwema Humlea Mtoto Wake Katika Njia Impasayo Ambayo Hataiacha Hata Atakapokuwa Mzee”

10.Mke Mwenye Hekima HUUWEKA MOYO WAKE KWA MUNGU: Huku Ndiko Anakoeleza Mapungufu Yake, Mapungufu Ya Mme Wake, Na Kukabidhi Ndoa Yao KWENYE MIKONO SALAMA NA MAKINI YA MUNGU. Mungu Anaweza Kubadili Chochote Ambacho Wazazi, Washenga Au Washauri Wa Ndoa Hawawezi Kugeuza Au Kutatua.
“Mke Mwema Hufunga Na Kuomba Kwa Ajili Ya Mmewe, Ndoa Na Familia Yake… Ni Rafiki Wa Uwepo Wa Mungu”

*Kama Umeolewa Ichukue, Ichape Na Uanze Kuitendea Kazi,
*Kama Umeoa, Ichape Na Umpelekee Mkeo,
*Kama Ni Binti Mwenye Malengo Ya Kuja Kuwa Mke Mwenye Ndoa Iliyofanikiwa, Ichukue Na Uichape, Ibandike Chumbani Kwako, Na Uanze Kuitendea Kazi.

Tafadhali Usiache Kutuma Sadaka Yako Kwa Ajili Ya Kazi Ya Mungu Ya Injili Tabora, Wiki Ya Pasaka, APRIL 16 HADI 21, Tutakuwa Na TIMU YA WATU 50, BUDGET NI MIL 8.
Tuma Hiyo Sadaka Kidogo Mungu Aliyokupa Itafanya Kitu:
Tuma Kwa Mhazini,
Eng Martha Shitindi
M-PESA: 0754 711 519

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: