Imani: Salamu Kutoka Mwanza

Imani

Biblia Inaposema, “IMANI CHANZO CHAKE NI KUSIKIA, NA KUSIKIA HUJA KWA NENO LA KRISTO” (Warumi 10:17).
Ina Maana Kwamba, “NENO LA MUNGU NDILO LINALOLETA USIKIVU NDANI YA MOYO WA MTU, ILI KUJENGA IMANI… IMANI ITAKAYOTUMIKA KUKUSAIDIA KUUSHINDA ULIMWENGU NA CHANGAMOTO ZAKE” (1Yohana 5:1-4).
Unapokuja Kwa Mtumishi Wa Mungu Ili AFUNGE NA KUOMBA Kwa Ajili Ya MATATIZO Au CHANGAMOTO ZAKO Wakati Wewe UNAKULA NA UMEWEKA MGUU JUU YA MGUU Hakika WEWE NI MGONJWA [Unaumwa Roho, Akili Na Mwili]!!
Jizoeze KULISOMA NENO LA KRISTO [BIBLIA YAKO] Katika HALI YA UNYENYEKEVU NA UTIIFU KWA ROHO MTAKATIFU Halafu UTAPATA UFUNUO Ambao UTAKUKWAMUA WAKATI WA TAABU!
Kumbuka Hili, “AZIMIAYE SIKU YA TAABU, NGUVU ZAKE NI CHACHE” (Mithali 24:10).
Na Ni WAJIBU WA KILA MKRISTO “KUMTAKA BWANA NA NGUVU ZAKE, NA KUUTAFUTA USO WAKE SIKU ZOTE” (Zaburi 105:4).
Usipotafuta NGUVU ZA ROHONI Kupitia NENO Maana LINA NGUVU (Waebrania 4:12), Lakini Kupitia MAHUSIANO YAKO NA YESU KRISTO [MAOMBI NA KUFUNGA] Ambavyo HUZALISHA NGUVU TOKA KWA KRISTO (Wafilipi 4:13), Hakika Utakuwa LEGELEGE Na “MAFURIKO, UPEPO NA MVUA ZA MAISHA ZIKIJA HAKIKA ZITAKUBOMOA NA KUKUNG’OA” (Mathayo 7:24-27).
WEWE “KULAKULA TU” Tangu Jumatatu Mpaka Jumapili Au Mpaka Mchungaji Wako Atangaze MFUNGO NA MAOMBI, Halafu “ANGUKO LAKO LITAKUWA KUBWA SIKU YA MAJARIBU NA TAABU, MAANA NGUVU YAKO NI CHACHE”
Hakuna Askari Anayeandaa Silaha Na Kufanya Mazoezi Vitani, Maandalizi Yanafanyika WAKATI WA AMANI!
Biblia Inasema, “MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU BALI JAWABU LA ULIMI HUTOKA KWA BWANA” (Mithali 16:1).
Fanya Maandalizi WAKATI WA AMANI Halafu NYAKATI MBAYA Zitakapokuja UTAVUKA SALAMA; Ukizubaa Utajuta!!
Salamu Toka Mwanza,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: