PEPO NI WABAYA

nguruwe

Nguruwe

“USIZIDIWE AKILI NA NGURUWE”

Yesu Alipofika Nchi Ya Wagerasi, Na Kukutana Na Yule Ndugu Aliyekuwa Na MAPEPO WACHAFU, WABAYA NA WAKATILI Waliokuwa Wakivunja Kila Kamba Na Minyororo Aliyokuwa Akifungwa Na Waliokuwa Wakimfanya Yule Mtu Ajichanje Na Kujichanachana Kwa Mawe…. Walipomuona Yesu Akija Walipiga Kelele Wakisema, “TUNA NINI NAWE YESU KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI? JE UMEKUJA KUTUTESA KABLA YA WAKATI WETU?” Halafu WALE PEPO WACHAFU Wakaomba Na Kumsihi AKIWATOA AWARUHUSU WAINGIE NDANI YA NGURUWE!!

KITU CHA AJABU KILITOKEA


Alipowaruhusu Wale PEPO WAWAINGIE NGURUWE… Kitu Cha Ajabu Kilitokea…. NGURUWE WOTE WALIKWENDA KASI NA KUFA MAJI [KUJITOSA BAHARINI]!!!

KILICHOTOKEA HASA


1.Nguruwe Hawakuwa Tayari Kukaa Na PEPO WACHAFU NDANI YAO Wakaona BORA WAFE KULIKO KUWA CHINI YA UTAWALA NA UDHIBITI WA ROHO CHAFU.
Cha Kushangaza Kuna Watu Mnasoma Ujumbe Huu Lakini MMEKUBALI KUKAA NA “TABIA, MIENENDO NA MIFUMO YA MAISHA” Ambayo NI MIBAYA, MICHAFU NA MNAJUA KWAMBA KUNA “NGUVU INAWASUKUMA KUWA HIVYO” Lakini MMEAMUA “KUFA NA TAI SHINGONI” Yaani “MMEAMUA KUKAA NA PEPO NDANI YENU” Ilhali NGURUWE WALIGOMA NA KUONA BORA WAFE KULIKO “KUTESWA NA ROHO CHAFU” Kama Hizo Zinazokutesa na Kukutawala.
Cha Ajabu Ni Kwamba HAUFANYI BIDII YOYOTE YA MAKUSUDI KUTAFUTA MSAADA WA “KUFUNGULIWA” NA KUTOKA KWENYE “MATESO” HAYO UNAYOPITIA!

Inawezekana Umekuwa MUONGO NA MDANGANYIFU “MUDA MREFU” Lakini UMERIDHIKA TU KUKAA NA HIYO “ROHO YA UONGO” NA HAUFANYI BIDII KUJIKWAMUA AU KUTAFUTA MSAADA HIYO “NGUVU CHAFU IKUACHIE”
Ndugu USIZIDIWE AKILI NA NGURUWE WALIOKATAA KUKAA NA PEPO, WAKAONA BORA WAFE!!

Inawezekana Umekuwa MZINZI NA MUASHERATI, Na Kila UKIMALIZA KUFANYA HIYO DHAMBI UNAUMIA NA KUTUBU KWA MACHOZI Lakini BAADA YA MUDA “HAMU NA KIU YA KUFANYA HICHO KITU INARUDI” Na Haufanyi Bidii Kutafuta Msaada, Bali UMERIDHIKA KUKAA “NA PEPO” Wakati NGURUWE WALIGOMA NA KUKATAA, WAKAONA BORA WAFE…. Usizidiwe Akili Na Nguruwe, Usife Na Tai Shingoni Ndugu, TAFUTA MSAADA UFUNGULIWE!!

Dhambi Yoyote Ambayo UMEJARIBU NA KUFANYA BIDII KUIACHA LAKINI IMEKUWA NZITO KWAKO, Na UNARUDI HUKO HUKO Kiasi Kwamba SWALA LA UTAKATIFU Kwako Ni Kama UONGO, HIYO INA ROHO [PEPO MCHAFU] NYUMA YAKE ANAYEISHIKILIA IENDELEE KUKUTESA…. Usizidiwe Akili Na NGURUWE, Hawakukubali KUKAA NA PEPO, WALIONA BORA WAFE!!
Tafuta Msaada Kwa Watumishi Wa Mungu Unaojua Wana NGUVU ZA MUNGU ZA KUTOSHA NA NI WATAKATIFU PIA Watakusaidia [Maana Kuna Watu Wanaitwa WATUMISHI WA MUNGU Lakini WANA SKENDO CHAFU]…Hao Badala Ya Kukusaidia Watakupa Matatizo Zaidi.

Salamu Toka Mwanza,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “PEPO NI WABAYA
  1. underson says:

    nashukuru sana kwa maneno mazuri yatokayo kwa bwana ili tusomapo tuweze kuuvua utu wa kale na kuvaa mwili wa yesu kristo.naomba msichoke kufundisha mambo kama haya hasa kwa vijana kama mimi ambao mambo mabaya ni mengi sana yanayotuzingila hadi kushindwa kumjua mungu kwa undani.MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: