Je kuna Dhambi ilikuwa inakutesa kwa siri :…..

: NA UNAHANGAIKA KUJIKWAMUA BILA MAFANIKIO??? UJUMBE HUU NI WAKO…

Dhambi Yoyote Ambayo UTAIFICHA Na Kutofanya BIDII [Kwenye Maombi Na Kufunga] Na Kumweleza ROHO MTAKATIFU Akusaidie KUJINASUA, Hakika ITAKUANGUSHA!
Wakristo Wengi WANAANGUKA DHAMBINI Na Kuacha MINONG’ONO MINGI NYUMA YAO Kwa Sababu WANAFUGA DHAMBI NDANI YAO Halafu Inafikia Wakati Ile DHAMBI INAZAA MAUTI [ANGUKO] Ambalo LINATIA AIBU ZAIDI NA LINA GHARAMA KUBWA Kuliko Gharama Ya Kwenda Kwa YESU AKUTUE HUO MZIGO NA KUMTWIKA HIYO FEDHEHA YAKO!
Biblia Inasema, “HATUJAFANYA VITA NA DHAMBI KIASI CHA KUMWAGA DAMU”…. Kama Kweli UMEDHAMIRIA KUWA MTAKATIFU NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, Hakikisha UNAFANYA VITA NA DHAMBI Inayokutesa Na Kukusumbua KWENYE MAOMBI Ukimsihi ROHO MTAKATIFU AKUPE NGUVU YA KUJIKWAMUA!
Yafuatayo Ni Mambo Yatakayokusaidia Kujinasua Kutoka Kwenye Dhambi Yoyote Inayokutesa:

1.USIIFICHE DHAMBI YAKO MBELE ZA MUNGU:

Mweleze Mungu Waziwazi [Kweney Maombi] Kwamba Unateswa Na Dhambi Fulani, Na Hauna Nguvu Yako Binafsi Ya Kujinasua
Wakristo Wengi Wanateswa Na Dhambi Kwakuwa HAWAKIRI DHAMBI NA MADHAIFU YAO MBELE ZA ROHO MTAKATIFU AMBAYE NI “MSAIDIZI” MWENYE NGUVU YA KUTUNASUA.
Biblia Inasema, “AFICHAYE DHAMBI ZAKE HATAFANIKIWA, BALI AZIUNGAMAYE NA KUZIACHA ATAPATA REHEMA” (Mithali 28:13).

2.AMINI NA KUBALI KWAMBA YESU HAKUFA KWA AJILI YA MSAMAHA WA DHAMBI TU, BALI ALIKUFA ILI AIHARIBU DHAMBI NA NGUVU YAKE INAYOKUTESA:

Wakristo Wengi Wanadhani Na Kuamini Kwamba YESU KRISTO Alikufa Ili Atupe MSAMAHA WA DHAMBI Na Pia Atupe UWEZO WA KUTUBU NA KUSAMEHEWA TENA ENDAPO TUTAKOSEA AU KUTENDA DHAMBI BAADA YA KUOKOKA… Hii Ni Sahihi Lakini Si Sahihi Sana!
YESU Amefanya Hayo Yote NDIYO Lakini Pia Amefanya Kitu Kikubwa Zaidi Ya Hicho, AMEUVUNJA UTI WA MGONGO NA UBONGO WA DHAMBI… Yesu AMEISHAMBULIA NA KUIANGUSHA DHAMBI… AMEISHINDA DHAMBI NA KUIPANGUA JUMLA KWA AJILI YETU Ili “TUKIWA HAI KWA MAMBO YA HAKI TUWE WAFU KWA MAMBO YA DHAMBI” (1Petro 2:24).
Biblia Inasema KUPITIA KRISTO YESU “TUMEIFIA DHAMBI NA KUUVUA UTU WA DHAMBI NA KUVAA UTU MPYA KWA KUFUFUKA KWAKE, ILI TUSIITUMIKIE DHAMBI TENA” (Warumi 6:4-6).
Bila KUAMINI KWAMBA “YESU ALIIVUNJA NGUVU YA DHAMBI NA KUIHARIBU” Hakika HAUTAWEZA “KUTEMBEA NJE YA UKANDA WA DHAMBI [SIN ZONE]”
Biblia Inasema, “YESU ALIDHIHIRISHWA ILI AZIONDOE DHAMBI [ZISIWEPO TENA]” (1Yohana 3:4-5).
BADILI MTAZAMO WAKO: “YESU ALIIVINJA NGUVU YA DHAMBI NA KUPATA SULUHISHO LA KUDUMU KUHUSU SWALA LA DHAMBI” Ukiamini Na KULIPOKEA MOYONI HILI, Na Kisha KULIOMBEA KWA MZIGO KWENYE MAOMBI YAKO, UTASHANGAA DHAMBI IMEPOTEZA NGUVU NA UTAWALA JUU YAKO NA NDANI YAKO!

3.NENO LA MUNGU LINA UWEZO WA KUKUFANYA KUWA MTAKATIFU NA KUZUIA USITENDE DHAMBI TENA; LISOME NA KULIAMINI, LITUMIE KAMA “STANDARD YA MAISHA YAKO” HALAFU DHAMBI ITAKUWA HISTORIA

“Na ya kuwa tangu utoto UMEYAJUA MAANDIKO MATAKATIFU, ambayo YAWEZA KUKUHEKIMISHA [KUKUFANYA MWENYE HEKIMA] HATA UPATE WOKOVU KWA IMANI ILIYO KATIKA KRISTO YESU… KILA ANDIKO LENYE PUMZI YA MUNGU [Lililovuviwa na ROHO MTAKATIFU] Lafaa KWA MAFUNDISHO, NA KWA KUWAONAYA WATU MAKOSA YAO, NA KUWAONGOZA, NA KWA KUWAADABISHA KATIKA HAKI ILI MTU WA MUNGU AWE KAMILI [PERFECT] AMEKAMILISHWA KA KILA TENDO JEMA” (2Timotheo 3:15-17).
Hii Mistari Hapo Juu Innaonyesha Waziwazi NGUVU NA UWEZO WA MUNGU WA KUMTOA MTU DHAMBINI NA NGUVU YA DHAMBI Kupitia MAANDIKO MATAKATIFU Pale ROHO MTAKATIFU Anapopewa NAFASI YA KUYAPA UHAI [PUMZI YA MUNGU]!

Lakini Pia Daudi Anatufundisha SIRI YA KUISHINDA DHAMBI, Naye Anatuambia NAMNA YA KUFANYA:
“MOYONI MWANGU NIMELIWEKA NENO LAKO ILI NISIJE NIKAKUTENDA DHAMBI” (Zaburi 119:11).
Unapoweka UAMUZI Wa Kulisoma NENO Na Kuliweka nafsini mwako [kwenye AKILI NA KUMBUKUMBU YAKO] Kisha Ukapata MUD WA KULITAFAKARI KWA IMANI NA SHAUKU, Litaingia MOYONI MWAKO Na Kukujengea MFUMO WA MAISHA MATAKATIFU Unaokataa Na Kupinga KILA NAMNA YA UASI NA UOVU.

Ukiufanyia Kazi Ujumbe Huu UTAJINASUA TOKA KWENYE DHAMBI YOYOTE, TABIA YA SIRINI INAYOKUTESA, Ila Usipoifanyia kazi Utaishia kusema WOKOVU NI MGUMU NA UTAKATIFU NI KAZI NGUMU… Weka Kwenye Matendo na UTAVUKA HAKIKA!!!

Salamu Toka Tabora,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
8 comments on “Je kuna Dhambi ilikuwa inakutesa kwa siri :…..
 1. underson says:

  hakika ni somo zuri sana,katika maisha yangu kuna dhambi ambayo imekuwa ngumu sana kuiacha lakini baada ya kusoma masomo haya na maandiko nimesali na kutubu,nachohitaji ni kuacha dhambi kwa maana shauku yangu ni kutaka kumuona mungu akitembea katika maisha yangu pamoja na familia yangu ndio shauku lililobaki ndani ya moyo wangu.MUNGU AKUBARIKI.

 2. Noah says:

  Ubarikiwe mtumishi wa Mungu.

 3. Theresia says:

  Mungu wa mbinguni akubariki…..ni kweli kuishinda dhambi kwahitaji maamuzi ya dhati na kujitoa wakfu ndipo upokee Neema ya msamaha….tusipojitoa kikamilifu na kuweka hiari kamwe hatutaweza.

  Na mbaya zaidi dhambi zinazotutesa sio dhambi mpya ni dhambi tulizozizoea kabisa na tunazitenda makusudi.

  TUMRUDIE MUNGU KIKAMILIFU TUACHE MAIGIZO

 4. JOYCE says:

  Napata faraja sana ktk mafundisho yenu, nimeokoka nampenda yesu ila kuna nguvu inanisumbua sana.

 5. Revocati Kimario says:

  Nafurahia sanaaaaa ujumbe wako

 6. Revocati Kimario says:

  Nafurahia sanaaaaa ujumbe wako mzuri. Natamani nifanye
  Vixuri katika maombi

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: