USIJIDHARAU NA KUJISHUSHA

Hata Kama Haujasoma Hata Elimu Ya Sekondari, Yaani Hata Division Five Huna, Ama Haujatoka Familia Mambo Safi Au Huna Watu Ambao Wana Nafasi Au Vitengo Wa Kukusaidia… Haya Yote Si Kigezo Au Vigezo Vya Kukufanya UWE MNYONGE Na KUPOTEZA UJASIRI Hasa Pale Unapokutana Na Watu Ambao Wana Elimu Kubwa, Au Wametoka Familia “Mboga Saba” Au Wenye Ndugu “Walioshika Vitengo”
UKIJIDHARAU NA KUJISHUSHA WEWE “NAFSINI MWAKO” NA KUJIONA DUNI NA ASIYEFAA, HAKIKA HAKUNA ATAKAYEKUPOKEA!
Usiogope ELIMU YA MTU, Hata Yeye Amewahi Kuwa Mtu Asiye Na Elimu Huko Nyuma.
Usiogope PESA YA MTU AU FAMILIA, Hata Wao Wamewahi Kuwa Masikini Na Wahitaji Huko Nyuma.
Usiwaogope Watu Kwa Sababu Ya NDUGU AU JAMAA ZAO WENYE VITENGO Haya Yote Yanaweza Kubadilika Wakati Wowote [Wanaweza Kupoteza Nafasi Zao, Wanaweza Kufa, Wanaweza Kuugua Muda Mrefu Na Kushindwa Kurudi Kwenye Hivyo Vitengo].
ILE KWAMBA “UMEUMBWA NA MUNGU KWA SURA NA MFANO WAKE” Na Pia Ya Kwamba “UMEUMBWA KWA KUSUDI MAALUMU” Na Ile Kwamba, “UNAISHI SASA NDANI YA MUDA NA WAKATI HUU” Ni Ushahidi Tosha Kwamba, “MUNGU ANA KAZI NA WEWE NA HAJAMALIZANA NA WEWE, LOLOTE JEMA LINAWEZA KUTOKEA KWAKO” Hata Kama HUONI PA KUTOKEA Au HUONI NAMNA YA HILO KUWEZEKANA!!
Mungu Aliyegeuza Historia Ya MWANAMKE ALIYETOKWA NA DAMU KWA MIAKA 12 MFULULIZI [Marko 5:28-34] Anaweza Kugeuza Historia Yako.
Mungu Aliyegeuza Historia Ya Yule KIPOFU ALIYEZALIWA KIPOFU NA KUWA MTU MZIMA KATIKA HALI YA UPOFU [Yohana 9] Anaweza Kugeuza Historia Yako.
Mungu Aliyegeuza Historia Ya Yule ALIYEPOOZA KWA MIAKA 38 [Yohana 5] Anaweza Kugeuza Historia Yako.
“HATA KAMA WATAKUDHARAU WATU WOTE, UWE MTU PEKE UNAYEJIKUBALI NA KUJITAMKIA MEMA NA MAFANIKIO”
Note: Usiandike “Amen” Zinajaza Notifications, Andika Comment Nzima.
HILI NI NENO LA MUNGU KWAKO… USIKUBALI KUJIKATIA TAMAA, MUNGU HAJAKUKATIA TAMAA… USIKUBALI KUJIDHARAU NA KUJISHUSHA MUNGU BADO ANAINUA WATU HATA LEO
!!

Salamu Toka Tabora,
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “USIJIDHARAU NA KUJISHUSHA
  1. ritha says:

    Nashukuru sana mtu wa MUNGU kwa neno hili limenifungua akili..ubarikiwe sana

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: