HII NI TAMU SANA

Hii ni Tamu

Hii ni Tamu

Kuna wakati ULIKUWA KWENYE KIFUNGO CHA DHAMBI, Ukiwa kwenye MINYORORO YA UTUMWA WA SHETANI Kwa sababu ya ASILI NA MWILI WA DHAMBI… SHETANI Alikuwa AKICHEKELEA NA KUSHANGILIA Akisema, “MUNGU AMEPOTEZA MAANA KILA MTU NILIYEMUUMBA NIMEMCHUKUA NAKWENDA NAYE JEHANAMU MILELE”
Ulikuwa UMENYWEA NA HUNA RAHA, HUNA TUMAINI, HUNA FURAHA, Hofu YA MAUTI, Hofu YA KUTENGWA NA MUNGU MILELE Ilitawala Na Kutanda MOYONI, NAFSINI NA MWILINI MWAKO… ULIKUWA UMEPOTEA MILELE!!!
LAKINI GHAFLA
Wakati Shetani Anashangilia Na Kufurahi Kwa Jeuri Na Kejeli… ILISIKIKA SAUTI TOKA MBALI… SAUTI YA MWOKOZI… SAUTI YA MWANAPEKEE WA MUNGU AICHUKUAYE DHAMBI YA ULIMWENGU… SAUTI YA YESU KRISTO….
Nayo Ilisema, “IBILISI MWACHIE HUYO DICKSON… MWACHIE HUYO (TAJA JINA LAKO HAPO)… MAANA NIMEKWISHA LIPIA GHARAMA YA MAUTI NA KIFO CHAKE KWA DAMU YANGU MWENYEWE… NIMEMNUNUA TAYARI KWA GHARAMA KUBWA YA DAMU YANGU… NILIKUFA NA KUFUFUKA KWA AJILI YAKE… MWACHIE HARAKA… MARA KAMBA ZA MAUTI ZIKAKATIKA NA KUKWACHIA… MARA MINYORORO YA DHAMBI IKAVUNJIKA NA KUYEYUKA… UKAWA HURU… FURAHA NA AMANI VIKAJA… IMANI NA TUMAINI VIKAMWAGWA NDANI YAKO… KAMA MTOTO MCHANGA UMEZALIWA UPYA, UMEZALIWA NA ASILI YA MUNGU… U KIUMBE KIPYA, NA YA KALE YAMEPITA… HAKUNA WA KUKUHUKUMU WALA KUKUSHTAKI.. YESU AMEZIFUTA HATI ZA MASHTAKA NA KUZIGONGOMELEA MSALABANI… UKO HURU TENA HURU KWELIKWELI… HALELUYAAH!!!
Usifiwe Msalaba,
Lisifiwe Kaburi,
Linalozidi Yote ASIFIWE MWOKOZI.
Naamini UFUNUO HUU Umeinua Moyo Wako UPYA.
Wewe Ni MTU WA AJABU NDANI YA KRISTO YESU, FURAHI, CHANGAMKA.
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo, sala
6 comments on “HII NI TAMU SANA
  1. Noah says:

    Meumishi wa Mungu, umenibariki sana kwa somo hili. Ubarikiwe na Mungu Mwenyezi Akuzidishie

  2. John Matiku says:

    UBARIKIWE MWAL. DICK KWA MASOMO MAZURI

  3. mtumishi wa mungu umeendelea kufungua maisha ya wana DAR ES SALAAM tulio wengi nikiwemo na mimi maana nilimkuwa sijui kuwa nimekalia kiti cha ENZI.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: