USHUHUDA WA R.W. SHAMBACH

“USISEME KWA SAUTI- WAKRISTO WENGI HAWAJUI HILI”

Wakati Nikiwa Kijana Mdogo Kiumri, Na Nikiwa Najifunza KAZI YA MUNGU Chini Ya Kaka Na Rafiki Yangu A.A.ALLEN, Siku Moja Wakati Wa Mikutano Ya Uponyaji Na Kufunguliwa Watu, Alitokea Mama Mmoja Aliyekuwa Na Mapepo Masumbufu. Yalipolipuka Na Tukawa Tukiyaamuru Yamtoke, Lakini Ilionekana Kama “MBINGU ZIMENYAMAZA” Ama “TUNATWANGA MAJI KWENYE KINU”
Na Wakati Huo Mtumishi Wa Mungu Kaka ALLEN Alitaka Kuendelea KUHUBIRI NENO LA MUNGU Na Wale Pepo Walikuwa Wakiondoa USIKIVU NA UTULIVU.
Kaka ALLEN Akanigeukia Na Kuniambia, “Kaka Shambach, Mchukue Huyu Mama Huko Nyuma, Mwombee Mpaka Uhakikishe Amefunguliwa”
Nikatii Maelekezo Yake Na Nikawaita VIJANA WENGI WADOGO WA KIPENTEKOSTE Waliopenda Sana Kazi Hizi Za Kutoa Pepo. Tukaenda Nyuma Kabisa Mbali Na Alipokuwa Akifundisha Na Kuhubiri Kaka ALLEN.
Wale Vijana Walikuwa Na SHAUKU NA KIU SANA Ya Kushughulika Na MAPEPO Na WALIANZA KUMSHAMBULIA YULE PEPO HARAKA Kwa Mamlaka Ya JINA Na DAMU YA YESU… Robo, Saa Ikapita, Nusu Saa Ikapita, Saa 1 Likapita Na HAKUKUWA NA MATOKEO; Yule Mama Alikuwa Amefungwa Bado.
Ile Hali Iliniumiza Sana, “KWANINI PEPO WATUSUMBUE?? KWANINI ASIFUNGULIWE?? JE, DAMU NA JINA LA YESU HALINA NGUVU??”
Haya Ni Baadhi Ya Maswali Yaliyopita Kichwani Mwangu Kama Kijana Mdogo Na Mchanga Kwenye KAZI YA MUNGU NA HUDUMA KWA UJUMLA.
Ghafla Nikaikumbuka WAKOLOSAI 2:14-15, “Akiisha Kuifuta Ile Hati Yenye Kutushtaki Kwa Hukumu Zake, Iliyokuwa Na Uadui Kwetu; AKAIONDOA ISIWEPO TENA, AKAIGONGOMEA MSALABANI; Akiisha KUZIVUA ENZI NA MAMLAKA, NA KUZIFANYA KUWA MKOGO KWA UJASIRI, AKIZISHANGILIA KATIKA MSALABA HUO”
Kwa Hasira Ya Roho Mtakatifu Nikasogea Pale Alipokuwa Yule Mama Mwenye Pepo Wale Wasumbufu, Kwa Ujasiri Wote Nikasema, “SHETANI MWACHIE HUYU MAMA HARAKA, YESU ALIKUSHINDA NA KUKUNYANGANYA MAMLAKA NA NGUVU ZOTE MIAKA 2000 ILIYOPITA”
Kitu Cha Ajabu Kilitokea!!!
Yale Mapepo Yalipiga Kelele Yakisema, “USISEME KWA SAUTI…SHIIII… WAKRISTO WENGI HAWAJUI HILI…. TAFADHALI USISEME KWA SAUTI”
Niliposikia Vile, Furaha Iliongezeka, Nuru Ilichanua Moyoni Mwangu…..
Nikamaka, “Umesema Nini Wewe Pepo Mchafu??”
Akajibu, “TAFADHALI USISEME KWA SAUTI KUBWA, WAKRISTO WENGI HAWAJUI, NA HATUTAKI WAJUE, WAKIJUA TUTAKUWA NA WAKATI MGUMU…USISEME KWA SAUTI KUBWA TUTATOKA”
Kwa Ujasiri Wote Na Kwa SAUTI KUBWA SANA Nikasema, “SHETANI, MWACHIE HUYU MAMA HARAKA SANA, YESU ALIKUSHINDA NA KUKUNYANG’ANYA NGUVU ZOTE NA MAMLAKA YOTE MIAKA 2000 ILIYOPITA”
Yale Mapepo Yakamwangusha Chini Na Kumtoka Saa Ileile!!!
HALELUYAAAH… UTUKUFU KWA YESU!!
Usisahau Mapepo Yalichosema, “TAFADHALI USISEME KWA SAUTI KUBWA; WAKRISTO WENGI HAWAJUI; TUNATUMIA UJINGA WAO [KUTOJUA KWAO] KUWATESA NA KUWAHARIBIA MAISHA… WAKISIKIA NA KUSIMAMIA HILO TUTAPOTEZA PAMBANO”
Umejifunza Nini Hapa Mkristo Mwenzangu??
Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: