CHAKULA CHA WASHINDI no2

“UPAKO WA KUFANYA ZAIDI YA WENGINE”

Na Mwl Dickson Cornel Kabigumila.

https://i2.wp.com/www.spirituality.org/i/HandsBible.jpg“Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kwelikweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba” (1Nyakati 4:9-10).

Mambo ya kujifunza:

1. Usiruhusu kiwango cha mafanikio ulichopo kikukwamishe kufika kule ambako umeumbwa na Mungu ufike.
Siku zote; Unapoona umefikia hatua fulani au umepata mafanikio fulani, ni ushahidi kwamba kuna kitu au vitu vingine vikubwa viko mbele yako unaweza kuvifanya au kuvipata.
Kupata mafanikio ni dalili tu kuwa kuna uwezekano wa kwenda mbali zaidi kama utaamua na kutobweteka na ulichokwisha kukipata!
Yabesi “ALIKUWA MWENYE HESHIMA KULIKO NDUGUZE” (Mstari wa 10).
Alikuwa ni “family champion”
Alikuwa ni “mtu wa mfano kwa nduguze wote”
Alikuwa “kioo cha wengine katika familia yake”
Wanafamilia wote “walitamani kuwa katika kiwango na ubora wa kimaisha aliokuwa nao Yabesi”
Mbali ya mafanikio haya… Yabesi hakuwa na jina zaidi ya “kiwango cha familia yake”… Kulikuwa na nafasi na uwezekano wa kuwa “mtu wa heshima katika taifa na si familia tu”… Kulikuwa na uwezekano wa kuwa “mtu wa heshima katika kizazi chake chote”… Kulikuwa na uwezekano wa kuwa mtu wa “kiwango cha dunia”… Yabesi hakukubali kupofushwa na kiwango hiki cha mafanikio ya kuwa “family champion”… Akaamua kutafuta “kiwango kipya”
Haijalishi una mafanikio makubwa kiasi gani sasa, Haijalishi wewe ndiwe mtu wa mfano kwenye mtaa wenu au familia yenu, kuna kiwango kipya cha mafanikio kinakusubiria kama uko hai leo.
Yabesi alijipambanua, Hakukubali kulewa sifa, Hakujilinganisha na nduguze na kuvimba kichwa… Alikiendea kiwango kingine cha mafanikio.
Go for higher level of success today in Jesus name.
Don’t settle for less… There is a higher place for you… Keep pressing foward.

2. Usikubali historia yako izuie kesho yako.

Historia ya Yabesi haivutii… Mama yake alimzaa kwa huzuni na uchungu… Na kama haitoshi akampa jina linalobeba ujumbe huo… Lakini hiyo haikumzuia Yabesi (mtu anayejitambua) kufika mbali.
Bila kujali jina na historia yake, aliweza kufanikiwa na “kuwa na heshima kuliko ndugu zake wote” hata wale wenye majina mazuri na historia za kuvutia.
Bila kujali historia yake imekaaje, Alijipambanua na kuweza kuwa mtu kati ya watu.
Aliwapiku ndugu zake wote. Na hakutosheka na hilo akaamua kwenda viwango vingine vikubwa.
Haijalishi una historia gani, haijalishi una jina gani, kama utajipambanua na kumwamini Mungu na kufanya sehemu yako, bado kuna Upako wa kuwa zaidi ya historia yako.
Your history is your past… Your present is your life… Your future is nothing but what you have inside you..!
Historia zote zinatengenezeka… Historia ya Rahabu ilitengenezeka… Historia ya Ruthu ilitengenezeka… Historia ya Sauli wa Tarso ilitengenezeka… Na historia yako inatengenezeka kama utaamua kujipambanua kama Yabesi.
Nakuambukiza upako huo kwa jina kuu la Yesu.

3. Hauwezi kupata kitu kwa Mungu mpaka uwe kwenye kiwango sawa na chake.
“Huyo Yabesi AKAMLINGANA MUNGU…”
Yabesi alihakikisha “anakuwa sawa na Mungu”… Alihakikisha “anamlingana Mungu”… Hapa simaanishi alikuwa Mungu naye, la hasha!
Namaanisha “alifuata vigezo na masharti” ya Mungu na akapata kile ambacho Mungu anacho na anatoa!
Pale utakapojifunza kumsogelea Mungu na kujua namna ya kuingia na kutoka mbele zake, Miujiza mikubwa itatokea maishani mwako na utaishangaza dunia yako!
Utakapojua kulitumia Neno la Mungu mdomoni mwako kwa nguvu na mamlaka, utaanza kupata kiwango cha matokeo anayopata Mungu.
Utaanza kudhihirisha utukufu, nguvu na Ufalme wake.
Haitoshi kumwomba Mungu, Jifunze “kumlingana” kama unataka kufanya anayofanya!
God can do nothing on earth but only through ordinary people with extraordinary level of understanding about Him and His Word.
Mwaka huu ukiamua kuhama kwenye ubinadamu, kuanzia kwenye lugha yako, mfumo wako wa kufikiri ukawa sawa na Neno, nakuhakikishia, utakuwa “umemlingana” Mungu na kilichotokea kwa Yabesi kitatokea kwako!
Lisome Neno la Mungu, litafakari kwa maombi kupata ufunuo, useme huo ufunuo kwa kinywa chako (ukiri), utumie kwenye maombi na tarajia maajabu na miujiza mikubwa!

4. Baraka zipo ila ni kwa wale waliojitenga na uovu.
Yabesi alijua siri hii. Hakumwomba Mungu baraka tu. Alihakikisha anamuua kwanza “mdudu” anayezuia baraka, aitwaye “uovu” ambao kwa lugha nyepesi ni dhambi.
“Lau (Mungu) ungenibariki kwelikweli (ungebadili kiwango changu na utukufu wangu kwa viwango vya juu), na kunizidishia hozi yangu (na kupanua mahali pa milki na mipaka yangu), na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu usiwe kwa huzuni yangu…”
Alijua wazi kwamba, hata kama ukipata kila kitu unachokitaka, kama kuna mianya ya dhambi/ uovu, hautaifaidi hiyo mali/ baraka… Adui atatumia huo mwanya kukushambulia, na badala ya kufurahia mali na baraka zako, zitaishia kukupa kilio na huzuni kama tunavyowaona matajiri wa dunia hii!
Sin will stop you from eating the goods of the land… Sin is the only key to devil’s killing, stealing and destroying demons… A man who is far from sin, is joyful, full of peace and candidate of both God’s blessings on earth and eternal life!

5. Maombi ya imani yana nguvu ya kufanya chochote.
Yabesi alikuwa mwanadamu kama sisi, mwenye tabia kama zetu, mwenye historia ngumu na mbaya kama wengi wetu… Lakini alipochukua hatua ya imani ya “kumlingana Mungu” kila kitu kiligeuka.
Mungu aliye hai “akamjalia yote aliyoyaomba” (mstari wa 10)!
Mdomo unaoomba, uko karibu sana na muujiza wake, bali ulionyamaza umetangaza mwisho wake!
A praying person is a carrier of miracles… He may be this way or that way now, but surely, There is a day when PRAYER ANSWERING GOD will visit him like Jabez.
Ningekuwa wewe ningejisemea, “Niko tayari kukosa muda wa kula lakini si muda wa kuomba”
Umebarikiwa,
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: