CHAKULA CHA WASHINDI no1

https://i1.wp.com/thecatholicspirit.com/wp-content/uploads/2013/07/crucifix_against_sky.jpg “Akasema, mtu mmoja alikuwa na wana wawili; Yule mdogo akamwambia babaye, Baba nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake kwa maisha ya uasherati. Alipokuwa amekwisha kutumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, naye akaanza kuhitaji. Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana aliyempa kitu. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia,  Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwanao tena. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; mleteeni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; kwakuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka: Alikuwa amepotea, naye amepatikana….. Alipokuja mwanae mkubwa na kujua yaliyotokea baada ya kuwauliza watumishi, Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akatoka nje akamsihi. Akamjibu babaye, akasema, Tazama, nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wowote, hujanipa mimi walau mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; Lakini alipokuja huyu mwanao aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote, na vyote nilivyonavyo ni vyako. Tena kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwakuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. ” (Luka 15:11-32).

Mambo ya kujifunza;

1. “Kwenye Ufalme wa Mungu- Baba yetu, hautapata chochote isipokuwa kile unachojua ni haki yako na urithi wako katika Kristo Yesu” Kilichomfanya mwana mpotevu apewe mali ya urithi, bila kujali uwezo wake mdogo wa kutunza na kusimamia pesa/ mali, ni ile tu kujua kuwa ana urithi/ mali ambayo ni haki yake katika mali alizonazo baba yake. Usipojua “yaliyo yako” kwenye mali alizonazo baba yako wa mbinguni, utaishia kuwatazama wenzio “wanatumia (wanabarikiwa, stawi na kuongezeka)” ilhali hali yako iko palepale! Kile usichokijua hautakifaidi. What you don’t know, you won’t expect, and what you don’t expect you won’t experience! Remember, it is your expectation that will bring on your manifestation. The bible puts it clear: “The expectations of the righteous will never be cut off” What do you know in the Kingdom of God? What do you expect? It is up to your understanding knowledge..! 2. “Usithubutu kufanya maamuzi yanayohusu fedha na mali kwa kukurupuka” Huyu mwana mpotevu hakufikiri mara mbili mbili. Alichowaza ni kuchukua urithi wake na kuwa nao mkononi kisha ndipo atajua cha kufanya. Hii si kanuni ya pesa. Kanuni ya pesa inasema, “Ujue cha kuifanyia pesa, na uamue bila kugeuka nyuma kuwa utafanya hicho kabla pesa haijaja” Ukisubiri pesa ije ndipo uipangilie nafasi yako, utaishia kuharibu kila kitu. Kabla hujauza gari lako, kiwanja chako, nyumba, shamba na rasilimali yoyote uliyonayo, Jiulize, Utaifanyia nini hiyo pesa kitakachokupa zaidi ya ulichouza?? Utanunua nini cha thamani na cha maana kuliko ulichopoteza?? Kabla hujachukua mkopo, jiulize, hilo unalotaka kufanya litarudisha hiyo pesa ndani ya muda sahihi? Je, una maarifa ya kutosha na uzoefu kuhusu hicho unachotaka kufanya?? Usichukue mkopo kwa ajili ya harusi, kipaimara, send off, kitchen party au chochote ambacho kinakula na hakizalishi. Kilichompoza mwanampotevu ni kuiweka mali yake kwenye vitu vinavyokula tu bila kuingiza! Maamuzi kuhusu pesa yanahitaji hekima kubwa sana. Kumbuka hii: “Pesa inayopita mikononi mwako inaweza kukufanya uwe tajiri au masikini” (Kauli ya mwl. Mwakasege). 3. “Kila unachokifanya ukiwa nje ya uwepo wa Baba/ Mungu hakiwezi kugeuza maisha yako na kukufanikisha” Hiki ndicho tunachokiona kwa huyu mwana mpotevu. Alipojaribu kuchanganya karata zake akiwa “nchi ya mbali” yaani mbali na uwepo wa Baba, hakufanikiwa! Aliishia kufanya kazi/ shughuli za uzalilishaji… Aliishia kulisha nguruwe na kutamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe… Kila “mwenyeji wa nchi ya mbali (mtu asiyeokoka)” utakayejishikamanisha naye hatakupa kitu cha maana, ataishia kukupeleka kwenye tope za mavi ya nguruwe. Kama umeharibu uhusiano wako na Mungu, na uko nchi ya mbali, nakusihi kwa jina la Yesu, imetosha… Rudi kwa baba yako, acha kupoteza muda kwenye shamba la nguruwe… Waache nguruwe wale maganda yao, nyumbani kwa Baba yako wa mbinguni unasubiriwa kwa hamu kubwa. Kama ulikuwa umerudi nyuma/ dhambini au haujampa Yesu maisha na umelisoma na kulielewa somo hili na ungependa kurudi kwa Baba yako wa mbinguni, rudia sala hii kwa imani: Sema, “Ee Bwana Yesu, ninakuja kwako, mimi ni mwenye dhambi, unitakase na kunisafisha kwa damu yako, nimerudi tena kwa Baba yangu wa mbinguni, nimechoka kukaa katikati ya nguruwe, unipokee na kuniokoa, katika jina la Yesu, amen” Ikiwa umeomba sala hii, tayari uhusiano wako na Mungu umerejea, haijalishi ulikuwa ukifanya nini huko “nchi ya mbali” tayari Yesu amekupokea… Kuanzia leo utaanza kula “ndama walionona” nyumbani mwa baba yako… Maisha yako yamegeuka sasa! Nitafute nikusaidie zaidi kukua kiroho na kuyaona mema ya Mungu kwako. Nipigie: 0655/ 0753- 466 675. 4. “Hakuna kitakachogeuka maishani mwako mpaja ugeuke unavyofikiria na kuyatazama mambo” Huyu mwana mpotevu aliendelea kula kwa tabu na kutamani makombo waliyokula nguruwe mpaka pale “alipozingatia moyoni (Untill he reasoned and give a deep thought)” ! Usipochukua muda kuiangalia kwa jicho la moyoni hiyo hali unayopitia, na kuanza kutafakari na kuumiza kichwa namna gani unatoka hapo, Mungu hatakupa wazo jipya la kugeuza hali yako! Mwanampotevu alipozingatia moyoni tu, na kuamua kubadilisha hali yake, Mungu aliweka upatanisho kati yake na baba yake hata kabla ya kuomba msamaha! Biblia inasema, “Njia za mtu (mipango, mikakati, mawazo na fikira) zikimpendeza Mungu hata maadui zake humpatanisha nao (atahakikisha umasikini, magonjwa, aibu, kilio, huzuni na maadui zako wengine wanatiishwa chini yako pale utakapoanza kufikiri na kupanga sawa na Neno lake lilivyoelekeza)” Usipozingatia moyoni, na kutenga muda kila siku ku-engage kwenye solution thinking, brainstorming, hautahama kwenye shamba la nguruwe! 5. “Kwa waajiriwa; Haijalishi mwenye nguruwe anakupenda kiasi gani, hatakupa nguruwe bali atakupa mshahara kwa kulisha nguruwe” Kabla ya yote ni muhimu ujue naiheshimu ajira yako, lakini pia ujue siheshimu kile unachokipata kwenye hiyo ajira. Unachofanya ni kikubwa kuliko unachopokea. Unachowekeza ni kidogo kuliko unachovuna. Ujuzi, muda, uhai, uaminifu, bidii, weredi, upendo na mengi unayowekeza katika “kulisha nguruwe” yanatosha kabisa kukufanya uwe na nguruwe wako! Hata siku moja, kiwango bora cha maisha hakitapatikana kwa kulisha nguruwe (kuajiriwa) bali kwa kufuga nguruwe (kubuni na kuanzisha shughuli/ kitega uchumi chako)! Mungu amekupa nafasi kwenye shamba la nguruwe upate uzoefu na si kutamani kujishibisha kwa makombo wanayokula. Thamani ya mchunga nguruwe ni kubwa kuliko nguruwe… Thamani ya ajira ni ndogo kuliko mwajiriwa! Wake up my dear friend… You can do a lot if you can only think enough! Na hiki ndicho chakula cha washindi leo, Umebarikiwa, Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
4 comments on “CHAKULA CHA WASHINDI no1
 1. jane says:

  mungu wangu wa mbingu na nchi na azidi kukuinua kwa viwango vikubwa asante sana nimepokea katika jina layesu

 2. Elisha Daudi says:

  Amen hakika hiki ndicho chakula cha washindi kweli,Ubarikiwe mtumishi

 3. gano mwaibale says:

  mimi nimeipenda sana mbarikiwe

 4. Zabron Nashon says:

  Amina na asante kwa darasa bora baba yetu akuzidishie…

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: