CHAKULA CHA WASHINDI No.13

“UPAKO WA KUFANYA ZAIDI YA WENGINE”

“BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya nyumba ya Baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; Nami nitawabariki wale wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; Na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Basi Abramu akaenda kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka 75 alipotoka Harani. “ (Mwanzo 12:1-3).

Mambo ya kujifunza:

1. “Umri mkubwa si kigezo cha wewe kutofanikiwa au kutotimiza kusudi kubwa la maisha yako duniani”Biblia inasema Ibrahimu alikuwa na miaka 75 pale Mungu alipomtoa Harani kumpeleka Kanaani.
Kwa umri huu alikuwa mtu mzima sana na hata mkewe Sara alikuwa na miaka 65 (maana walizidiana miaka 10).
Kwa umri kama huo wengi wetu tungekuwa tumekata tamaa na tusingekuwa na wazo la kuhama kutafuta “kiwango kikubwa na bora zaidi” cha maisha!
Wengi katika umri wa miaka 75 tungekuwa tunasema, “tumestaafu” na tunakaa tu nyumbani ili kula “mafao” tuliyochuma kazini pamoja na “marejesho” kidogokidogo kutoka kwa wanetu.
Lakini haikuwa hivyo kwa Abramu.
Alikuwa bado na “picha kubwa ya maisha” ndani yake na alikuwa bado akitafuta “fursa” ya kutimiza kila ndoto aliyonayo.
Nimewahi kumsikia bibi mmoja wa miaka 75 nchini Tanzania aliyemaliza degree yake ya kwanza.
Huyu mama angeweza kuwa na sababu za kukaa tu na kula mafao nyumbani.
Lakini ndani yake kulikuwa bado na “utupu/ nafasi” iliyokuwa inahitaji kujazwa kielimu.
Kulikuwa na ndoto ambayo hakuwa tayari kurudi nayo kaburini.

Rafiki yangu na baba yangu mchungaji, na Luteni mstaafu wa Jeshi Mzee Sosteness Langula alipata degree yake ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana akiwa na zaidi ya miaka 60!
Ndani yake “hakuwa ameridhika” na kiwango cha elimu alichokuwa nacho, na hakukubali kupoteza sehemu ya maisha yake kielimu.
Nakupa changamoto wewe unayedai “umri umekwenda” na umejikatia tamaa kuwa hizo “ndoto” ulizonazo ndani yako haziwezi kutimia… Nakuambia, umri si tatizo la kukuzuia kufikia malengo yako.
Kama Ibrahimu aliweza kuchangamka na kufanyia kazi ndoto zake akiwa na miaka 75 kwanini wewe mwenye miaka 48, 50 na kitu, 60 na kitu usitimize ndoto zako?
Usiwe mbinafsi… Biblia inasema, “Mtu mwema huacha urithi hata kwa wana wa wanawe (wajukuu)”
Ukiamua kutoa sadaka ya muda wako uliobakia kugusa vizazi vijavyo… Hakutakuwa na kitu kinachoitwa “kustaafu” na kukaa tu nyumbani ukila mafao!

Kalebu alikuwa na umri wa miaka 85 alipopambana na Majitu katika nchi ya Kanaani na kuimilki Hebroni (Joshua 14:6-14).

Musa alikuwa na miaka 80 na Haruni alikuwa na miaka 83 pale Bwana alipowatuma waende kuwakomboa Waisraeli utumwani (Kutoka 7:7).

Ukipata muda google kwenye mtandao “people who succeeded at old age” au “People who became great at old age”
Lengo ni kukuonesha kuwa kama Ibrahimu alivyokuwa akiifuata ndoto yake na kusudi la maisha yake akiwa na miaka 75, mzee yeyote mwingine anaweza kufanya makubwa na KWA WENGINE SISI WADOGO walio kwenye miaka 20 na kitu kama mimi, na 30, 40 na 50 tuna deni kubwa la kufanya vitu vikubwa kwa utukufu wa Mungu!

2. “Mungu anapokubariki hataki uwe na vya kukutosha wewe na watoto wako tu… Anataka akubariki mpaka wewe pia uwe baraka kwa wengine”

Mungu alimwambia Ibrahimu, nitakubariki ili uwe baraka (I will bless you to the extent you become a blessing yourself)!
Mungu anapotubariki ni ili “tuyaguse” na “kuyabariki” maisha ya wengine.
Hivi unajua Mimi Mwl D.C.K nimebarikiwa sana na Mungu? Kila siku nayagusa maisha ya maelfu ya watu duniani kote kupitia kile ambacho Mungu amenipa… Na kwangu haitakuwa muujiza baada ya miaka michache kuwa tajiri mkubwa, mmiliki wa vitu vingi vikubwa, taasisi, makampuni nakadhalika… Nimekuwa mwaminifu kutumia baraka aliyonipa Mungu kuleta masuluhisho kwa wengine… Mungu anapotubariki na kutupatia chochote si kwa ajili ya kuosha majina yetu na kuwa mastaa… Bali ni wajibu mkubwa wa kuwa baraka kwa wengine!
Nikienda kitandani, nikiamka, nikitembea, nawaza namna gani nitawafikia mamilioni ya watu kila siku…. Nawaza namna gani nitawaleta watu walau 100 kwa Yesu kila siku… Nawaza namna gani nitafanya kwa Neema na Upako wa Roho mtakatifu watu waponywe… Huduma za wengine zikue… Namna gani nitafanya makanisa yote yawe na moto wa Mungu na utakatifu… Nawaza namna ya kuwa baraka zaidi… Halafu jina langu litakua… Nitaongezeka na kuwa mtu mkuu!
Hii ndiyo kanuni, amua kuwa baraka kwa wengine… Una vitu vya kugusa na kubariki maisha ya wengine… Wewe ni mwana wa Ibrahimu…. Una nguvu na neema ndani yako kuwa baraka kwa wengine!

3. “Umeitwa na Mungu kuwa mtu wa kiwango cha dunia (global personality)… Jiandae na fanya bidii usibweteke njiani”

“…Na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (mstari wa 3).
Mungu ametuita tuwe watu wa kiwango cha dunia. Kila tunachokusudia na kupanga kama wana wa Ibrahimu lazima kiwe cha ngazi ya dunia… Katika sisi jamaa zote za dunia watabarikiwa… Wazo ulilonalo Tanzania linaweza kufanya kazi Kenya pia… Biashara iliyokubali Mbeya inaweza kufanyika Nairobi.
Upako unaoponya Mtanzania unaweza kumponya Mmarekani.
Yesu anatuita SISI TULIOOKOKA kuwa ni CHUMVI NA NURU YA DUNIA (Mathayo 5:13-14).
Hatuiti chumvi ya wilaya au mkoa au taifa bali ya dunia nzima!
Kila mahali utakakokwenda hakuna mahali watakataa UMUHIMU WA CHUMVI…Hakuna watakaokataa na kuipokea NURU… Hizi ni bidhaa za kuhitajika kila mahali duniani!
Yesu anasema SISI TULIOOKOKA AMETUOKOA ILI TUWE GLOBAL PERSONALITIES… WATU WA KIWANGO CHA DUNIA.
Kwangu mimi kuwa Mwalimu wa kiwango cha dunia sio muujiza… Ni kawaida…. Yesu ameniokoa ili niwe global personality… Siwezi kuishia Tanzania… Wako wengi wananisubiri kila kona duniani… Wako wengi wanakusubiri rafiki yangu… Umeokolewa uwe bidhaa ya kiwango cha duniani!
“Kwako jamaa zote za dunia watabarikiwa

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
3 comments on “CHAKULA CHA WASHINDI No.13
  1. JOHN MATIKU says:

    Hakuna kitu kizuri kama kumjua Mungu!!! Asante sana Teacher kwa Mafundisho mazuri. Mungu akuinue tena na tena katika Jina la YESU.!! Mtumishi,tuko Pamoja;

  2. Frederick Laizer says:

    amen

  3. Mwakalengela, L. A says:

    nipo law school of tanzania dsm muda huu, najisomea kwa maandalizi ya mitihani. basi naamua kupitia NENO ili kujaza “mafuta” na google maneno haya ‘toka wewe kwa jamaa zako’ lo! nimemshangaa Mungu! injili hii ambayo nimekutana nayo imeachilia mlipuko wa ajabu moyoni mwangu! UBARIKIWE SANA MTUMISHI. umeumba kitu kipya ndani yangu,,. kweli una wito mkuu.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: