CHAKULA CHA WASHINDI No09

“UPAKO WA KUFANYA ZAIDI YA WENGINE”

Anania, pamoja na Safira mkewe

“Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja, akaliweka miguuni pa mitume. Petro akasema, Anania, kwanini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwishauzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia hayo akaanguka akafa. Hofu nyingi ikawashika watu wote walioyasikia haya. Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje wakamzika.
Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho mtakatifu? Angalia miguu ya waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua wewe nawe. Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika na mumewe. Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya” (Mdo 5;1-11).

Mambo ya kujifunza:

1. “Shetani atakuletea mawazo na sauti yake ya uangamivu; Simama imara uipinge na kuizuia isigeuke matendo yako na hatimaye dhambi”

Tunaona hapa kuwa ni Shetani aliyemdanganya Anania na mkewe Safira na kuwajaza mioyo yao kumwambia uongo Roho wa Mungu… Anania na Safira walikuwa na maamuzi yao kukubali au kukataa ushawishi wa Shetani. Lakini wao walichagua kutii sauti ya adui na kuuingiza uongo wake mioyoni mwao.
Shika hii: Shetani kukuletea mawazo mabaya na ya dhambi si kosa lako, ila kukubali na kupokea hayo mawazo na kuyatendea kazi, ndicho kitakachokuponza kama akina Anania.
Kila muda Ibilisi akikujia na mawazo yake mabaya;Mpinge ukiwa thabiti katika imani, kwa kuliangalia Neno la Mungu tu, naye atakukimbia!
Usimpe Ibilisi nafasi kama Anania na mkewe… Mpinge naye atakukimbia (1Petro 5:8, Yakobo 4:7, Waefeso 4:26, 2Kor 10:3-5).

2. “Si kila anayetoa sadaka anapata baraka na faida; Wengi wameharibikiwa baada ya kutoa sadaka”

Unamkumbuka Kaini? Unakumbuka kuwa matatizo yake yalianza baada tu ya kutoa sadaka vibaya? Huyu ndugu alipoteza future yake na ya wanawe kupitia sadaka (Mwanzo 4).

Unamkumbuka Mfalme Sauli mwana wa Kishi?
Huyu alipoteza Ufalme wake, future yake na ya wanae kupitia sadaka… Alipokosea, akapoteza kila kitu (1Samweli 15).

Na Anania na mkewe nao walipoteza maisha, future na kila kusudi jema la Mungu kupitia sadaka.
Wako wengi wameharibikiwa maisha yao mara tu baada ya kuleta sadaka zao mbele za Mungu!
Ni muhimu kujipanga vizuri na kumsikiliza Roho wa Mungu kabla ya kutoa sadaka yako… Maana si wote wanabarikiwa kupitia sadaka, wengine wanaharibikiwa!

3. “Mnapokubalina huko kanisani kwenu kuhusu utoaji au jambo lolote; Ujue Roho wa Mungu atakufuata kuona unatekelezaje mlichokubaliana”

Anania na wenzake wa kanisa la Mitume walikubaliana kwamba wote wenye viwanja, mashamba, wauze na kuleta chote walichouza chini ya mitume ili kitumike kuhudumia watakatifu wote, walionacho na wasio nacho (Mdo 4:34-36).
Kilichompoza Anania na mkewe ni kufanya nje ya makubaliano nyuma ya sadaka hii.
Walipunguza badala ya kuleta kila walichokipata kwenye mauzo.
Yaheshimu makubaliano ya watakatifu wawili au watatu ama kanisa, maana Mungu anakuwa nyuma kuyafuatilia.
Ukikubali na kutii unakula mema ya nchi.
Bali ukikataa na kuasi (kwenda kinyume) unaangamizwa kwa makali ya upanga (Isaya 1:19-20).

4. “Unaposikia sadaka, usiweke akili yako kwenye sadaka bali kwa Mungu atakayekuja kupokea sadaka yako; Hii itakusaidia yasikukute ya akina Anania”

Watu wengi wakisikia kuhusu sadaka wanawaza tu aina, kiasi na madhabahu ya kuipeleka hiyo sadaka lakini hawamuwazii kabisa Mungu atakayekuja kupokea sadaka yao kwa mikono ya mtumishi wa Mungu wa madhabahu husika.
Ni muhimu ujue… Sadaka ni ibada kamili katika Ufalme wa Mungu… Na sadaka yako inakubaliwa au kukataliwa na Mungu hata kabla haijafika madhabahuni.
Ikikubaliwa baraka ya Mungu inakujia.
Ikikataliwa mauti, uharibifu au laana vinakupata.
Unapokwenda kutoa sadaka ni muhimu umsikilize Mungu, usogee mbele zake kwa toba… Ili kuepusha yaliyomkuta Anania na Safira mkewe… Hata siku moja usijaribu kumzoelea Mungu..!

5. “Mahali pasipokuwa na nguvu za Mungu zinazodhihirika waziwazi, Watu hawawezi kuwa na hofu ya Mungu na utakatifu”

Mungu asiyeonekana na kujifunua katikati ya watu, huyo Mungu hawezi kuwa na nafasi mioyoni mwa watu.
Watu hawawezi kumheshimu na kumcha kwa dhati, kutakuwa na mazoea… Litakuwa kusanyiko la kidini lisilo na nguvu ya kigeuza mioyo na maisha ya watu!
Biblia inasema, Baada ya watu kuona namna Mungu alivyowashughulikia “waongo” Anania na Safira, Hofu nyingi ililishika kanisa na watu wote waliosikia habari hii.
Uwepo wa Mungu uliowazi katika utendaji ndio unaojenga uchaji wa kweli wa Mungu.
Watu wakiishia tu kumsikia Mungu bila kumuona… Hawawezi kumcha!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: