CHAKULA CHA WASHINDI No10

“UPAKO WA KUFANYA ZAIDI YA WENGINE”

“Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa kwamba yumo nyumbani. Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao Neno lake. Wakaja watu wakimleta mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu umesamehewa dhambi zako…Nakuambia, ondoka, jitwike godoro lako uende nyumbani kwako. Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe” (Marko 2:1-12).

Mambo ya kujifunza:

1. “Si kila aliyesimama kwenye foleni ya kuelekea kule kwenye hatma unayoiendea anakiona kile unachokiona”

Biblia inasema hawa ndugu walipofika, walikosa mahali pa kupita, njia yao kuelekea hatma yao ilijaa watu.
Ilikuwa imesongamana kiasi kwamba hapakuwa na nafasi ya kuweza kukifikia kile kilichowafanya wafunge safari kuja kukipokea.
Wote walionekana wamekuja kwa Yesu lakini si wote walitaka muujiza wa mtu aliyepooza.
Hii ni kanuni iliyo kwenye maisha; Si kila anayeonekana mshindani wako ana maono, ndoto na picha uliyonayo wewe, Wengine wamejaza tu njia kutukatisha tamaa na sisi tusichukue hatua kuelekea kwenye kile tunachokitaka.
Wengi wanaonekana kama wanaelekea tunakoelekea, tena wako hatua nyingi mbele zetu, lakini usiwaogope, waliokuwa wameziba nafasi hawakuwa wameona kile ambacho hawa ndugu walikiona tangu wakiwa nyumbani.
Usiwaogope unaosoma nao darasani au wanaotoka vyuo na degree kama yako, hawaelekei njia unayoiendea, hawana picha uliyonayo!
Usiwaogope wafanyakazi wenzako au wafanyabiashara wanaouza bidhaa kama zako, hawana picha ya ndani kama yako iliyokupelekea kufanya hicho; Wengi wanaoonekana wanaelekea tunakoelekea, wanafuata tu mkumbo, hawana picha/ maono, Wasikutishe wala kukukatisha tamaa!

2. “Kama kweli una imani, hiyo imani haitaishia kukupa tumaini, bali itakupa maelekezo moyoni ya nini cha kufanya utakapokutana na upinzani”

Imani si matumaini japo imani huzaa matumaini. Imani huleta picha moyoni mwa mtu ya namna ya kupata kile anachokitarajia. Imani haiwezi kuzuiwa na vizuizi vilivyoko kati yako na muujiza wako.
Hawa ndugu walikuwa na imani, walipokutana na vizuizi imani iliwapa cha kufanya… Iliwaambia wapande na kupasua dari na kutokea pale muujiza ulipo.
Imani hulenga pale muujiza ulipo. Imani haichoki wala kukatishwa tamaa na vizuizi.
Imani huushinda ulimwengu na upinzani wake wote.
Na huku ndiko kushindako kuushindako ulimwengu yaani hiyo imani yetu.
Mwenye imani ya kweli atakuwa na maelekezo ya namna ya kuvuka viunzi kuelekea muujiza wake.
Mwenye matumaini huishia kwenye kizuizi na kubakiza lugha tamu za “najua siku moja Mungu atatenda” na hii si imani… Imani hutenda sasa!

3. “Chanzo kikuu cha magonjwa ya wanadamu ni dhambi”

Magonjwa na mateso mengi waliyonayo wanadamu ni matokeo ya dhambi zao binafsi na wengine kutokana na madhara waliyopatilizwa ya dhambi za waliotangulia (hii tunaita laana) yaani kubeba matokeo ya dhambi ya wengine!
Hili kuponya jumla tatizo lolote la kiafya, lazima kwanza iponywe dhambi iliyopelekea ugonjwa ukapata nafasi ndani yake!
Yesu alielewa hili… Mbali ya imani ya waliomleta mgonjwa, bado aliishughulikia dhambi ya mgonjwa… Dhambi yako imesamehewa!
Sehemu nyingi Biblia inatuambia chanzo kikubwa cha magonjwa ni dhambi.
Dhambi imeleta uharibifu maishani mwa mwanadamu.

Unamkumbuka yule aliyekuwa amepooza kwa miaka 38 pale kwenye birika la Bertzatha? Yesu alipomaliza kumponya alimwambia, “Angalia umekuwa mzima, usitende dhambi tena likaja kukupata jambo lililo baya zaidi” (Yohana 5:14).
Zaburi 103:3 inakazia siri hii: “Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote”
Unapotenda dhambi unaharibu afya yako na kumpa Ibilisi ruhusa kukupatia mshahara wa magonjwa kabla ya mafao ya dhambi yaitwayo mauti!
Tauni haitaikaribia hema ya mwenye haki, wala uele uharibuo adhuhuri… Mwenye haki/ mtakatifu yuko mbali naagonjwa… Ukiishinda dhambi… Magonjwa yanakukimbia!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
One comment on “CHAKULA CHA WASHINDI No10
  1. JOHN MATIKU says:

    Mungu wa Mbinguni akubariki Mtumishi kwa Mafundisho mazuri. Nice moment!!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: