CHAKULA CHA WASHINDI No11

“UPAKO WA KUFANYA ZAIDI YA WENGINE”

mwanamke mmoja mwenye kutoka damu

“Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharamiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya. Aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake; maana alisema, nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusongasonga nawe wauliza ni nani aliyenigusa? Akatazama kila upande ili amwone aliyetenda neno hilo. Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Akamwambia, Binti, Imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena” (Marko 5:25-34).

Mambo ya kujifunza:

1. “Kila lenye mwanzo lina mwisho endapo hautakata tamaa na kulipa nafasi likumalize”

Kila jambo ambalo linamtokea mtu, liwe baya au zuri linakuwa na kusudi nyuma yake. Na linaruhusiwa kuja kwa mtu huyo na si mtu mwingine kwa sababu ana msuli wa kulibeba na kulishinda. Lakini wako wengi waliokufa kwa magonjwa, habari mbaya au mambo mabaya yaliyotokea maishani mwao. Badala ya kuyakabili kwa Neno la Mungu, wameishia kuangalia ubaya na ugumu na wamezamishwa jumla.
Jambo lolote linalokujia, ni kwa sababu liko ndani ya uwezo wako, na kama utatunza amani na utulivu wa moyo, utapindua meza na kupata ushindi.
Huyu mwanamke alikabiliana na hii kansa kwa muda wa miaka 12 mfululizo, lakini hakukubali hata mara moja kufa na hili tatizo. Alipambana kwa akili, nguvu na ufahamu wake wote, hakukubali kukata tamaa na kuingia kwenye orodha ya watakaokufa.
Kumbuka hili; Uwezo wa uzima au wa mauti uko ndani yako… Kwa ulimi wako unaamua kipi kije kwako… Kwa miaka 12 huyu mama hakuwahi kusema hii damu itaniishia mwilini na nitakufa. Bali alipambana kutafuta suluhu. Aliupigania uhai wake kwa gharama zote. Hakukipa kifo nafasi mpaka muujiza wake ulipotokea!
Unamkumbuka yule ndugu aliyekuwa amepooza kwa miaka 38? Hakukata tamaa na kuondoka birikani… Alikaa kwenye mkondo wa uponyaji na siku moja Mungu katika umbo la Yesu alimtembelea!
Umeshikilia zaidi ya nusu ya muujiza wowote unaotaka… Usipokata tamaa… Usipokubali kuamsha mikono na kuruhusu kushinda, Muujiza utapatikana hata kama ni kwa kuchelewa!
Una nguvu ndani yako ya kuhimili huo upinzani… Una nguvu ndani yako ya kuitawala hiyo hali unayoipitia… Muujiza wako upo… Mungu aliiona shida wakati inaingia…. Anajua ilipokufikisha sasa na anajua namna ya kuikomesha kama utaamua kuvipiga vita vizuri vya imani!
Usikate tamaa… Muujiza wako hauko mbali na wewe.

2. “Si kila aliyeko kwenye foleni ya kuelekea unakokwenda naye anataka kile unachokitaka… Usiogope ushindani”

Walikuweko wengi walioligusa vazi la Yesu siku ile, lakini ni mwanamke huyu aliyeponywa peke yake.
Walikuweko washindani na wapinzani wengi wanaoonekana wanataka kuchukua alichokijia… Lakini hakukatishwa tamaa… Alipambana… Alijipenyeza… Alimpangua mpinzani mmoja baada ya mwingine na kufikia ndoto yake!
Usiwaogope wapinzani… Usiwaogope washindani… Si kila anayefanya unachofanya wewe ana picha kama yako… Wengine wanawaza pesa tu halafu hawajui cha kufanya baada ya kuipata… Wengine wanataka tu umaarufu na wakishaupata wanabweteka na kupotea… Usiwaogope washindani na wapinzani… Ni wengi waliomgusa Yesu lakini ni mmoja anayejielewa aliyepata muujiza!
Kama unajielewa na unajua unachotafuta, usiwaogope wapinzani na washindani walioko kwenye njia yako ya mafanikio… Songa mbele… Penya na uliguse hilo vazi ulilokusudia!

3. “Imani hutoa maelekezo ya namna ya kupata muujiza… Imani hutoa matendo ya kufanya ili kupata unachotaka”

Imani ya kweli, imani ijayo kwa kusikia habari za Yesu (kama ilivyokuwa kwa huyu mama) haikupi tu matumaini moyoni, bali inakupa na njia na mbinu ya kupata kile ulichoamini moyoni!
Imani moyoni mwa mwanamke huyu ilimpa cha kufanya kupata muujiza wake.
Imani mioyoni mwa wale ndugu wanne waliombeba ndugu yao aliyepooza iliwapa cha kufanya kupata muujiza kwa ajili ya ndugu yao.
Imani kwenye moyo wa yule akida aliyekuwa na mtumwa wake mgonjwa ilimpa njia ya kuweza kupokea muujiza wa mtumwa wake bila hata Yesu kumfikia na kumwona!
Imani ya kweli inaambatana/inakupa na matendo fulani ya kufanya “ndani yako” ili kupata matokeo!
Hauwezi kusema unaamini na ilhali umekaa tu… Imani huambatana na matendo kuuelekea muujiza unaouona kwa imani ndani yako!

4. “Si kila anayemsonga Yesu atapata kitu kwake… Yesu hababaiki na miguso ya watu bali imani iliyo ndani ya mguso”

Yesu hakumwambia huyu mama ya kuwa “mguso wake” umemponya, la hasha!
Bali alimwambia, “Binti yangu, enenda kwa amani, IMANI YAKO IMEKUPONYA”
Ni wengi wana bidii “kumsonga Yesu” na wengine “wanamgusa kabisa” lakini kinachomfanya mmoja arudi na ushuhuda na mwingine abaki kuwa mtu wa dini ni IMANI ILIYOCHANGANYIKA NA MGUSO!
Imani ndiyo pesa pekee inayoweza kununua chochote kwenye duka la Ufalme wa Mungu ambalo Yesu ni Shop keeper!
Yesu haangalii kelele za “Muuzaji nipe hiki au kile” anaangalia “pesa iliyoko mkononi” iitwayo Imani inayonunua bidhaa unayotaka!
Mguso wako usipochanganyika na Imani, utaishia kuwaona wenzako wanakuja na kukuta halafu wanapokea miujiza yao na wewe unabaki palepale… Kumgusa Yesu hakutoshi… Changanya na imani kwenye mguso!

5. “Yesu anapokutendea muujiza, Usiingie mitini… Njoo utoe ushuhuda na kuna kitu kikubwa zaidi utapokea”

Unawakumbuka wale wakoma 10 walioponywa na Yesu? Ni mmoja tu alirudi kushukuru na Hali hii ilimshangaza hata Yesu, akasema, “Je hawakuponywa wote 10? Je wale kenda wako wapi?” Na hakuishia hapo bali alimpa kitu kikubwa na cha ziada yule mmoja aliyerudi kushukuru… He made him whole… He did not just heal the leprosy but he made him whole!

Na ndicho kilichotokea pia kwa mwanamke huyu aliyetokwa na damu. Kwa kugusa pindo la Yesu “msiba wake ulikauka” lakini bado Yesu alimuulizia aje, maana alikuwa na kitu kingine kikubwa cha kumpa zaidi ya uponyaji!
Alipojitokeza na kurudi kwa Yesu… Yesu alitoa tamko (declaration) ya kukomesha jumla ule msiba… Alisema, “Enenda kwa amani, Usiweko tena msiba huu kwako”… Mimi ninaamini kama angeondoka bila kupata hili tamko, kuna wakati msiba huu ungemrudia!

Angalizo: Kila Mungu akikutendea muujiza kwenye madhabahu fulani au kupitia kwa mtumishi fulani, usiingie mitini jumla kama wale wakoma tisa… Rudi na shukurani… Njoo ushuhudie kile ulichotendewa na Bwana… Halafu mtumishi wa Mungu atatamka Neno au kukuombea na kuthibitisha muujiza wako usipeperuke!
Kutorudi kumshukuru Mungu ni sababu mojawapo inayofanya miujiza inapeperuka.
Mwenye masikio na asikie… Huwezi kuwa na ujanja kuliko Yesu… Lazima tutende kwa ukamilifu kama tunataka matokeo kamili!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
3 comments on “CHAKULA CHA WASHINDI No11
  1. JOHN MATIKU says:

    Thank you! God bless you my teacher for your good Lesson!!

  2. gano mwaibale says:

    mafundisho nimazuri sana nimeyafurahia

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: