CHAKULA CHA WASHINDI No12

“UPAKO WA KUFANYA ZAIDI YA WENGINE”

“Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng’ombe na kondoo na hema. Na nchi ile haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja. Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu na wale wa Lutu; siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi. Abramu akamwambia Lutu, Basi, uwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wako na wachungaji wangu; maana sisi tu ndugu. Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami nakusihi; Ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume, Ukienda upande wa kuume nitakwenda upande wa kushoto.
Lutu akainua macho yake akaliona bonde lote la Yordani, ya kwamba lote lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri unapokwenda Soari. Basi Lutu akajichagulia bonde lote la Yordani; Lutu akaenda upande wa mashariki, wakatengana wao kwa wao. Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile bonde; Akajongeza hema yake mpaka Sodoma. Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA” (Mwanzo 13:5-13).

Mambo ya kujifunza:

1. “Usijefanya kosa la kuachana na mtu sahihi aliyebeba baraka zako mara tu unapoona umepata kiwango fulani cha mafanikio…”

Lutu alitoka Uru akiwa na Ibrahimu. Alikuja akiwa hana kitu chochote. Alipoanza kubarikiwa na kufanikiwa Ibrahimu kwa mkono wa BWANA ndipo na wale aliokuwa nao walipoanza kufanikiwa. Kufanikiwa kwa Lutu kulitoka katika mbaraka wa Ibrahimu. Nyota ya utukufu ya Ibrahimu ndiyo iliyoyarahisisha maisha ya Lutu. Kama si Ibrahimu, Lutu asingelifika hapo. Mafanikio na kuongezeka kwake kulikuwa kumefungwa kwa Ibrahimu.
Kuna watu ambao tangu wamekuja maishani mwetu wamesababisha maisha yetu yageuke na kupata nuru. Tangu wamekuja maishani mwetu, milango mingi imefunguka. Kana kwamba walikuwa na funguo za milango yetu ya baraka. Hawa ni watu wa muhimu sana, hawa si watu wa kuwaachia waondoke kirahisi maishani mwetu.
Tujifunze kwa Potifa, alipogundua kuwa Uwepo wa Yusufu unamfanikisha na kumtajirisha, hakushindana naye wala kumpiga vita, bali alimkabidhi kila kitu na ndipo alipobarikiwa na kufanikiwa sana sana na mali yake kuongezeka sana!
Farao alipogundua kuwa uwepo wa Yusufu una nguvu ya kumbarikia na kuongeza kiwango chake cha mafanikio, hakutafuta kushindana naye, bali alimpatia cheo kikubwa, na akawa anaingiza faida zaidi.
Kuna wako maishani mwako ambao tangu umekutana nao na kufahamiana nao wamekusaidia kwa namna moja ama nyingine kupiga hatua na kustawi… Usikubali kuwapoteza… Usiseme sasa nina uzoefu wa kutosha naweza kufanya hili jambo peke yangu… Usimpoteze Ibrahimu wako kisa ugomvi wa Wachunga mifugo wenu!

2. “Ukipata nafasi ya kufanya uchaguzi au uamuzi, usidanganyike na hali unayoiona sasa… Vinavyoonekana ni vya muda, visivyoonekana ni vya milele”

Kilichompoza Lutu ni hiki. Aliangalia wingi wa maji… Aliangalia uzuri wa nje… Bila kuangalia vigezo vya kufanya huo uzuri ukae na kuongezeka!
Alikuwa anakwenda kutengana na mtu ambaye anaweza kumsikia Mungu… Mtu aliyekuwa role model wake… Mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa yeye kufikia hapo…. Na hakufanya lolote kuuliza hekima kwa Ibrahimu… Alikurupuka na kuchangamkia fursa ya kuchagua “akiwa wa kwanza” bila kutafuta shauri la Mungu au kupata hekima toka kwa mtu wa Mungu Ibrahimu.
Lutu aliyaamini macho yake kuliko ufahamu wa Kimungu ndani ya Ibrahimu.
Lutu aliamini mwonekano mzuri wa bonde la Yordani kuliko Neno la Mungu linalosema Wasio haki hawatafanikiwa na akaenda kujiunga nao katika miji ile ya Sodoma na Gomora.
Kwa Wasomaji wa Biblia mnajua kwamba mwisho wa siku alipoteza mali zake zote, akampoteza mkewe, akaponea chupuchupu, akawa frustrated na kuishia kuzaa na mabinti zake!
Biblia inasema, “Tusiyatazame yanayoonekana, bali yasiyoonekana, kwa maana yanayoonekana ni ya muda tu, bali yasiyoonekana ni ya milele”
Pia Biblia inatupa hekima kuhusu machaguo, inatuhasa; “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu lakini mwisho wake ni mauti”
Unapopata fursa ya kufanya maamuzi au machaguo… Ni mchezo wa hatari… Haijalishi kwa nje inaonekana ni njema kiasi gani… Unahitaji neema ya Mungu na hekima itokayo juu kufanya maamuzi sahihi!
Usipotezwe na kipande cha nyama unachokiona, ukanaswa na kitanzi usichokiona!

3. “Haijalishi umepata fursa gani nzuri sana; Kama kuna dhambi katika mazingira yako ya kazi, mwisho wako ni mbaya”

Hiki ndicho kilichomkuta Lutu. Hakuwa mwenye dhambi. Alikuwa na hofu ya Mungu aliyoipata wakati akiwa na Ibrahimu. Lakini alipojichanganya na wafanyabiashara wa Sodoma na Gomora, kila kitu kilipotea mwishowe.
Alianza kama mtu anayefanikiwa au kupata faida. Biblia inasema aliongezeka, akatanua hema yake hadi Sodoma. Alivutiwa na mapato ya udhalimu. Mwisho wake haukuwa mwema.
Haijalishi unafanya deal gani, unavuna mapesa, kama unafanya kitu ambacho kinawahusisha watu wasiomcha Mungu, na kina mazingira ya dhambi, hautakuwa na mwisho mzuri… Macho yako yatafunikwa na hiyo faida ya muda mfupi, ukija kushtuka utajikuta uko mahali pabaya… Utapoteza ushuhuda na hata hicho kilichokuwa kinakutia jeuri.
Ikipimbie dhambi…. Hata kama unavuna kwa kiasi gani… Mwisho wake ni mbaya!
Usikubali kuchanganya mambo yako na dhambi… Utapoteza!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “CHAKULA CHA WASHINDI No12
  1. Elisha says:

    Mungu akubariki mtumish kwa ujumbe mzur, Mungu nisaidie

  2. gano mwaibale says:

    Nikweli kabisa ktk maamuzi ni vizuri kutanguliza hekima ya mungu

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: