BONGO MOVIE & BONGO FLEVA STARS

Kufa kila mmoja atakufa ni sawa, Ila ukiwa “msanii” na kuishi “kisanii” pia unakufa kisanii… Vijana wanaondoka wabichii… Anayefikisha miaka 40 au 50 ni kama amefikisha 100 hivi!
Viburi, kutoheshimu wazazi, kukosa maono, ulevi, uzinzi, kupenda utajiri wa haraka na usio na malengo zaidi ya kutaka watu waone tu kuwa wana pesa nakadhalika vinawaondoa mapema!

Hakuna mtu anayezalisha “wazo la kwake” hapa duniani… Ni aidha unalipata kwa Mungu au Shetani!
Hawa “wasanii” wana mawazo mengi ambayo yanajionesha waziwazi yametoka wapi… Na gharama ya wazo toka kwa Shetani siku zote ni vifo vya mapema.

Kama unamfahamu “msanii” anayeishi “kisanii” na akaishi maisha marefu ya baraka na ustawi nipeleke unioneshe!
Shetani hajawahi kulipa mshahara mzuri.

Nimewaza vijana kama akina Langa, Mangwair, Mez B, Steven Kanumba, Adam Kuambiana, Shalo Milionea, na wengine wengi walioondoka wabichii… Wameishi kisanii na wamekufa kisanii.

Yeyote unayemuona sasa katika hiyo miziki, filamu za Kibongo, au presenter wa radio au TV na anaishi maisha machafu “mtafute miaka 10 tu” ijayo na hautamuona!
Biblia inasema, “Usifurahie kufanikiwa kwa mtu muovu maana ni kwa kitambo tu. Utamtafuta wala hautamuona… Kufanikiwa kwa mpumbavu kutamuangamiza”

“Hauwezi kula ujana na ukatarajia utafikia uzee mwema.”
Biblia inasema muda wa kujitunza na kutembea na Mungu ni ujana… Ukikosea hapo tu, umekwenda na maji!

“Ni vema mwanadamu aichukue nira wakati wa ujana wake” (Maombolezo 3:27).

“Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha ya maisha” (Mhubiri 12:1).

“Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa (siku zangu za ujana), Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu” (Ayubu 29:4).

Sijui wako wapi akina Dudubaya, Mr Nice, Q-Chief, Daz Baba, Matonya, Z-Anto, Pingu na Deso, Zay bee, H-baba, na wengine waliovuma miaka 10 iliyopita?

Ujana bila Yesu hakika ni maji ya moto hakika yatakubabua kama sio kukuua kabisa!

Salamu kwa kila kijana,
Tengeneza maisha yako,

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “BONGO MOVIE & BONGO FLEVA STARS
  1. NESTORY AMOS says:

    amina mtumishi nimekupata sana

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: