FAHAMU THAMANI NA NGUVU YA DAMU YA YESU

1. Ni uhai wa Mungu uliotutoa mautini kutuingiza uzimani (1Petro 1:18-19, Yoh 5:24).

2. Damu ya Yesu ni tiketi na ufunguo pekee uliotuingiza kwenye familia ya Mungu (Ufunuo 5:8-10)

3. Ni silaha ya vita inayompa ushindi mtu aliye katika familia ya Mungu (Ufunuo 12:10-12)

4. Damu ya Yesu ilishalipia msamaha, ondoleo la kila dhambi yangu na yako… Dhambi zote ulizotenda, utakazotenda leo au kesho “zililipiwa miaka zaidi ya 2000 iliyopita”… Ila hiyo si tiketi ya kukufanya utende dhambi makusudi… (Waebrania 10:12,14, Ufunuo 1:4-5, 1Yoh 1:6-7)

5. Damu ya Yesu imeshikilia uhakika wa umilele wetu… Ni damu ya agano la milele… Imetuingiza kwenye familia ya Mungu na hakuna kitu cha kututoa kwenye uhakika wa uzima tulionao… (Waebrania 13:20-21)

6. Damu ya Yesu inatupa uhakika wa kufutwa kwa hati za mashtaka zilizokuwa zikitutenga na Mungu kabla hatujampokea Yesu… Lakini inaweza kufuta kila shtaka lolote (na hukumu mtu anayoisikia ndani yake kwa sababu ya dhambi au kosa alilofanya baada ya kuokoka)… (Waefeso 2:10-15, Wakolosai 2:10-16)

7. Damu hii ya thamani inaweza kutumika kwa imani kuleta upatanisho kati ya watu au makundi yasiyopatana (maadui)… Kama ilitupatanisha na Mungu ni rahisi zaidi ikitumika “kwa imani” kuwapatanisha maadui (Waefeso 2:10-15, Waebrania 12:14).

8. Damu hii ya Yesu ndiyo inayotupa ujasiri wa kusogea mbele za Mungu mkamilifu na mtakatifu pasipo hofu kwenye maombi na ibada zetu… Kile alichokifanya Yesu kwa ajili yetu, kukubali kuwa mbadala wetu, na kubeba hukumu yetu msalabani na kumwaga damu yake… Imetupa haki kisheria kuwa haki ya Mungu (2Kor 5:21), na kutupa ujasiri kumsogelea Baba yetu wa mbinguni, Abba kwa ujasiri (Waebrania 10:19).

9. Damu hii ya thamani inaweza kutumika kama “karata ya mwisho” katika kumtoa mtu kutoka kwenye utumwa (kifungo) ambacho kinamtesa, ingawa anaona miujiza au matendo ya Mungu maishani mwake lakini bado amefungwa…. Ilikuwa hivi pia kwa waisraeli kule Misri… Walikuwa watu wa Mungu… Waliona miujiza na matendo makuu ya Mungu (miujiza 9 mikubwa) lakini haikuwasaidia kutoka kwenye kifungo/ utumwa wao!
Kuna watu ambao wameokoka lakini kuna tabia, dhambi na vifungo fulani vinawatesa japo mioyoni mwao wameokoka na wanampenda Yesu kwelikweli… Suluhu ya hili ni kuitumia Damu ya Yesu kwa imani dhidi ya hicho kitu, tabia au dhambi!
Waisraeli walipoitumia “damu ya kondoo” kwa imani, iliwatoa utumwani… Nasi kwetu wa Agano jipya, Kristo Yesu ni pasaka wetu… Ni mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu… Aliyechinjwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa… (ufunuo 5:5-6, 9, Yoh 1:29, 35-36)!
Ukiitumia “kwa imani” damu ya Yesu itakufungua na kukukomboa…. Kwa damu yake tunao ukombozi wetu (Waefeso 1:7).
Iamini na itumie Damu ya Yesu ikusaidie,
Mwl D.C.K
Email: http://www.kabigumilacornel.dick@gmail.com
Web: www.yesunibwana.org
0655 466 675/ 0753 466 675 (WhatsApp, kupiga na meseji)

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: