SALAMU KUTOKA KUZIMU

 (Luka 16:19-31).
“Wanaokufa duniani, hawasahau wala kupoteza kumbukumbu… Ukiwa mbinguni au kuzimu utakuwa na akili na uelewa wako wote… Utateseka kuzimu kama tajiri au kufurahia kama Lazaro mbinguni… Uamuzi ni wako”


“Kuzimu hakuna maji ya kunywa… Japo walioko wana kiu tena kali kuliko hata sisi tulioko duniani… Kiu inaweza kuua mtu lakini cha ajabu hawafi… Ungependa kwenda huko? Ukimwamini Yesu utapakwepa huko, utakwenda alikokwenda Lazaro… Uamuzi ni wako”

 

“Walioko kuzimu wanajua tayari wamepotea… Wanajua hawawezi kupata nafasi ya kuokoka… Wanaelewa kuwa wokovu ni kwa sisi tulioko duniani tu… Wanajua tusipoikubali kazi ya msalaba na kumpokea Yesu na kuishi maisha matakatifu tutakwenda huko pia… Tajiri anasema tusiende huko… Na ndugu zako waliofia dhambini wanamsihi Mungu ukubali injili usiende waliko… Utampokea Yesu lini? Ukifa dhambini, hata kama unasali kanisa linaloitwa la kiroho au la waliookoka unaishia kuzimu milele… Walioko kuzimu hawataki twende huko… Kwanini usiokoke leo rafiki? Ukifa dhambini kufumba na kufumbua utakuwa kuzimu na tajiri”

 

“Walioko kuzimu wanajua kuwa walikuwa na nafasi ya kutubu na kumwamini Yesu na kuingia mbinguni lakini waliipoteza… Wanaumia na kusikitika… Wanakumbuka kuhusu mahubiri yote waliyosikia… Wanakumbuka kila onyo walilopewa na Roho mtakatifu… Je, ungependa ujikute katika hali kama hii ambayo majuto hayawezi kukusaidia? Mpokee Yesu na kuishi maisha matakatifu, usicheze na dhambi ujue tu wapitaji hapa duniani na muda wowote tunaondoka”

Misty Dark Lake Wallpaper

“Ukishaingia kuzimu, tayari umepotea milele, utateseka milele… Hautatoka huko kamwe bali utateseka milele huku ukijuta kwa kupoteza fursa ya kuokoka… Utakumbuka post zangu kuhusu utakatifu, namna ya kuishinda dhambi nakadhalika… Utakumbuka kwenye friendlist yako ulikuwa na rafiki kama mimi ninayeweza kukusaidia kuujua wokovu na kuokoka, kukusaidia kuacha dhambi inayokutesa na ungeweza kuwasiliana nami lakini hukufanya hivyo… Itakuuma, utajilaumu, utasikitika, utajuta lakini hautatoka humo kamwe… Unatumiaje nafasi kama hii ya kuwa rafiki wa mtumishi wa Mungu kutengeneza maisha yako toka dhambini? Unaishia ku like na ku comment, kumbe ni mwathirika wa dhambi, na hautaki kuwa mkweli usaidike… Umeamua kufa na tai ya ulokole na udini shingoni kumbe unajijua moyoni hauna Yesu… Ukienda kuzimu, utanikumbuka… Utainua macho yako na kuniona mbinguni na itakuuma kweli kwa kutotafuta msaada wa kiroho tulipokuwa marafiki facebook”

 

“Walioko kuzimu ni wapweke… Wanatamani wangepata hata mtu wa kuongea naye au kuwatia moyo lakini haiwezekani… Wamejaa wengi kuzimu lakini ukali wa mateso, hali ya kifo iliyotanda huko, harufu mbaya ya miili ya watu inayoungua japo haiteketei, uhaba wa hewa nzuri na kutokuweko kwa furaha na amani kunaondoa kabisa maisha na matumaini… Je, ungependa kuwa huko? Ukienda kuzimu kwa sababu ya hiyo dhambi uliyoamua kuikumbatia, hautamlaumu mtu… Uko hai sasa, kwanini usiamue kuiponya roho yako? Kwanini usinitafute nikusaidie na tumsihi Mungu pamoja utoke kwenye hiyo dhambi? Kwanini uendelee kufanya kitu unachojua kitakupeleka kuzimu dakika yoyote? Yesu anakupenda na hajakukatia tamaa… Ndio maana watu kama mimi wenye msaada tuko kwenye friendlist yako… Unatumiaje fursa ya kuwa rafiki yangu au mtumishi yeyote wa kweli wa Mungu?”

 

“Ndugu zako waliokufa dhambini walioko kuzimu muda huu… Wanamsihi Bwana Yesu, wengine wanasema, Yesu unaonaje ukifufuka katika wafu na kwenda kuwahubiria ndugu zetu, wazazi, marafiki na jamaa zetu walioko dhambini ili wasije mahali hapa pa mateso tulipo, maana wakiona alama za misumari mikononi na miguuni wataamini! Halafu Yesu anawajibu, Kwenye friendlist yao facebook wana akina Mwalimu Dickson Cornel Kabigumilawakiwasikiliza hao na kutafuta msaada kwao kuhusu wokovu, maisha matakatifu watawasaidia, la sivyo hawatanisikiliza mimi hata nikitoka nikaja na alama za misumari na kovu la mkuki ubavuni…. Na wewe ambaye hujaokoka, unataka ufike kuzimu ndipo uanze kujuta? Unataka uendelee na dhambi yako mpaka lini? Yesu hataki upotee… Kwanini usinitafute nikusaidie? Kwanini uende kuzimu unajiona?… Uamuzi wako leo utaamua umilele wako…”

 

“Walioko kuzimu wanajua ya kuwa WENYE TIKETI ZA MBINGUNI si watakatifu waliokufa (akina Lazaro, bikira Mariamu, Paulo, Petro na wengineo), bali ni sisi WATUMISHI WA MUNGU TULIO HAI NA TUNAMHUBIRI YESU DUNIANI… Hakuna aliyekufa anayeweza kuleta wokovu kwa walio hai… Tajiri aliambiwa, HUKO DUNIANI WAKO WATUMISHI WA MUNGU WENGI WA KWELI NA WENGINE WANAO HADI FB NA WHATSAPP WASIPOWASIKILIZA HAO NA KUGEUKA WATAKUJA HUKU KUZIMU… Ni machozi na huzuni ukienda kuzimu ilhali ulikuwa rafiki yangu facebook, WhatsApp na Instagram… Nilikuwa tayari kukusaidia hukutaka… Ungeweza kuwasiliana nami ukapuuza… Itakuuma na kukuliza kama utakwenda kuzimu ilhali nilikuwa rafiki yako… Kwanini hukunitumia nikusaidie uache hiyo dhambi uliyojaribu kuiacha bila mafanikio? Urafiki wa kweli ni kufaana na si kufanana… Unataka msaada nitafute nikusaidie”
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “SALAMU KUTOKA KUZIMU
  1. emmanuel jason says:

    nahitaji kuwasiliana na wewe Mtumishi wa Mungu
    0785056545 namba yangu

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: