Siri

https://i0.wp.com/scienceblogs.com/startswithabang/files/2012/04/IR_MilkyWay_WISE_vertical1.jpg“Wahubiri Wengi Waliotingisha Ulimwengu Wa
Injili Marekani Na Ulaya… Waliotumiwa Na
Mungu Kwa Viwango Vya Kutisha Na
Kushangaza… Kwa Ishara, Miujiza Na Matendo
Ya Kushangaza; WENGI WAO [zaidi ya 50%]
WALIMALIZA VIBAYA: Wengi Walikuwa
HOMOSEXUAL [Mashoga Na Walawiti],
ALCOHOLICS [Walevi Wa Kutupwa], SMOKERS
[Wavuta Sigara Na Madawa Wa Kutupwa],
WOMANIZERS [Watu Wa Wanawake Na Uzinzi
na Uasherati], BROKEN FAMILY AND
MARRIAGES [Watoto Na Wake/ Waume Zao
Walishindwa Kuwalea Na kuishi Nao Maisha Ya
Ushindi- Walioa Na Kuacha Mara Kibao Na
Walishindwa Kulea Watoto Wao Katika Njia
Yenye Ushuhuda], LOVERS OF MONEY
[Walitegwa Kwenye Mtego Wa Kupenda Pesa Na
Wakaishia Huko], PRIDE [Kiburi Na Kubeba
Utukufu Wa Mungu Kuliharibu Kila
Walichokuwa Wamefanya Kwa Miaka Mingi]…
Kwa Kifupi WENGI WALIMALIZA VIBAYA….
Sababu Kubwa Ni Hii; UNAPOINGIA KWENYE
KAZI YA INJILI YA NGUVU ZA MUNGU NA
ISHARA NA MAAJABU NA UDHIHIRISHO WA
WAZI WA ROHO MTAKATIFU ‘Inaharibu sana
kazi mipango na shughuli za malango ya
kuzimu’ Ebu Fikiria UNAVUNJA MIKATABA YA
PEPO WALIOKAA KWENYE UKOO KWA MIAKA
MIA KADHAA WAKIHARIBU UKOO FULANI NA
WALE WATU WANARUDI KUMUISHIA NA
KUMTUMIKIA MUNGU WA KWELI NA
KUTUMIKIA KUSUDI LA MUNGU BADALA YA
KILE ALICHOKUWA AMEKUSUDIA ADUI…
Unapindua na kugeuza MAAZIMIO
YALIYODUMU KWA MIONGO NA MAMIA YA
MIAKA… Unageuza na kuondoa MIFUMO YA
KISHETANI ILIYOTAWALA ENEO AU SEHEMU
[Mkoa, Taifa, Bara]… SHETANI NA SERIKALI
YAKE HAWAWEZI KUNYAMAZA TU…
WATAHAKIKISHA WANAPAMBANA; Yamkini
Ikiwezekana WAKUHARIBU NA KUHARIBU
ULICHOBEBA NA UNACHOFANYA KISIENDELEE
KUSUMBUA UFALME WAO NA KULETA SERIKALI
YA MBINGUNI DUNIANI… Watawinda WAPI
ULIKO NA UDHAIFU [kila Udhaifu Ulionao Ni
Mlango Utakaokuangusha USIPOKAZANA
KUUONDOA AU KUU-REPLACE NA NGUVU ZA
MUNGU]… Watawinda HUDUMA YAKO
[Watapitia Kwa Watumishi wa kweli wa Mungu
Ili Uumie Na Kuona Inakuwaje Ushambuliwe
Na Watu Ambao WALIPASWA KUKUTIA MOYO…
Atapitia Kwa Watu Wa Karibu Kwenye TIMU
YAKO YA HUDUMA… Atamtumia Mke/ Mmeo
Nk]… Atawinda NDOA YAKO [Kama Mme/ Mkeo
Si MTU HATARI WA IMANI Hakika Hiyo Ndoa
Ina Asilimia Nyingi KUVUNJIKA Au Kuishia
Kushikwa Na Kipengele CHA KIFO PEKEE
KIWATENGANISHE Ingawa Ndoa Ilishafutika
Mioyoni Mwenu Muda]… Atakuwinda Kupitia
WATOTO WAKO [Haishangazi Kuona Watoto Wa
Watumishi Wa Mungu Ni VIMEO BALAA]… Kila
NAFASI UTAKAYOMPA IBILISI ATAITUMIA
KUKUMALIZA NA KUMALIZA KILA
ULICHOKIFANYA WAKATI UKIWA VIZURI NA
MUNGU… Ni Rahisi KUANZA VIZURI KAZI YA
INJILI Ila Ni NGUMU MNO KUDUMU NA
KUMALIZA SALAMA… Paulo Alisema,
ANAJILINDA NA KUFANYA KILA ANALOWEZA ILI
ASIJEKUISHIA KUWAHUBIRI WENGINE HALAFU
YEYE AKAWA WA KUKATALIWA… HATA DAKIKA
ZA MWISHO ZA KAZI YAKE Alisema, ANAKAZA
MWENDO KUIFIKIA MEDE YA THAWABU;
AKIYASAHAU YALIYOPITA [Akisahau Past
Achievement, Past Glory, As If Anaanza Siku
Hiyo… Maana KURIDHIKA NA MTEMBEO
ULIOPITA WA MUNGU NI MTEGO WA
KUSHINDWA KUMALIZA SALAMA]… Yesu
Aliwahi Kudokeza Hili Pale Aliposema, ‘SIKU ILE
WENGI WATAKUJA WAKISEMA, TULIPONYA,
TULITOA PEPO KWA JINA LAKO, TULIFUFUA
WAFU, TULIFANYA MIUJIZA YA KUSHANGAZA,
TULITABIRI’ Lakini Atawaambia ONDOKENI
KWANGU NINYI SIKUWAJUA… Yesu Alisisitiza
Sana Hili Pale Wanafunzi Waliporudi Na RIPOTI
YA HUDUMA Wakisema, “HATA PEPO WALITUTII
NA MAMBO MENGI MAZURI YAMETOKEA
HUKO”… Yesu Aliwasisitiza Akisema,
“MSIFURAHI KWA KAZI MLIZOTENDA NA
MNAZOTENDA… BALI HAKIKISHENI MAJINA
YENU ‘YANADUMU KUANDIKWA MBINGUNI
[Maana Yanaweza kufutwa Ukiharibu]’ NA HII
NDIYO INAPASWA KUWA FURAHA HALISI
KWENU”… Wahubiri Wenzangu, Vijana Kama
Mimi, Na Nyie Mliotutangulia Kwenye Injili…
TUSIPOKAA KWENYE KWELI YOTE NA ‘KUDUMU
KATIKA KUOMBA… TUKIKESHA KWA SALA ZOTE
NA MAOMBI… TUKITEMBEA KATIKA UPENDO…
KATIKA UNYENYEKEVU WOTE… HEKIMA YOTE…
UTAKATIFU WOTE… Hakika Tutakwama Kama
Wengi Waliotutangulia WALIOACHA HISTORIA
NZURI Lakini MIISHO YAO Ilikuwa MIBAYA
[Wengine Ilijulikana Na Wengine Ilifichwa]…
HATUNA MUDA WA KUCHEZA; ULE MOTO WA
KWANZA Unapaswa KUWA MOTO WA KILA
SIKU… KULE KUFUNGA KWAKO KWA
KWANZA… KUKESHA KWAKO… KUSOMA
KWAKO NENO ISIVYO KAWAIDA… KUJITENGA
NA WATU WANAOKUCHAFUA NA KUKUPOTEZEA
MUDA NA YESU [KUKOMBOA WAKATI]… Bila
Haya Kuwekwa Sawa Na Kuacha UKISASA NA
MAZOEA… Tutaangukia Pua”
HII CHANGAMOTO…
Binafsi nahitaji MNIOMBEE MIMI NILIYE
MDOGO NA MWANENU PIA [KWA BAADHI
YENU]; Sitaki Kuharibu, Sitaki Kupoteza Muda,
Sitaki Kukataliwa Siku Ile!!
Tujikwamue Na Kuwakwamua “WAHUBIRI
VIJANA HASA” Ili Kuufanya Mwili Wa Kristo
Usiendelee Kupata Hasara Hii.
Namnukuu Benny Hinn
“Nilipopata Mtikisiko Wa Ndoa Na Mke Wangu
Suzan, Nilijikuta Kwenye Wakati Mgumu, Kiasi
Kwamba Shetani Aliutumia b HUO Na
Nikaanza Ku-date WANAWAKE, Kama Si MUNGU
KUNIWAHI; Ningeanguka Na Kupoteza KILA
NILICHOKUWA NIMEFANYA KWENYE UFALME
WA MUNGU Na Mbaya Zaidi NINGEANGUKA NA
WATU WENGI WANAONITAZAMA KAMA KIOO
NA MFANO Katika Ufalme Wa Mungu; Naamini
MAOMBI YA WATAKATIFU Walioniombea Kipindi
Kile Ndiyo YALINIOKOA NISIZAME Ila Nilikuwa
Kwenye HATUA ZA MWISHO KUHARIBIKIWA”
Mwisho Kunukuu;

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “Siri
  1. Joshua Sospeter says:

    Bwana AKUTIE NGUVU mtumishi.

  2. Asant says:

    Nabarikiwa kwa masomo mazur mtumishi,MUNGU azidi kukutumia

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: