MATENDO MEMA ALIYOYASEMA YESU NI YAPI?

https://www.lds.org/bc/content/bible-videos/videos/the-savior-suffers-in-gethsemane/jesus-christ-is-arrested.jpg

Kwenye kitabu cha Mathayo 5:16, Bwana Yesu anasema;

” Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze
mbele ya watu, wapate kuyaona
matendo yenu mema, wamtukuze Baba
yenu aliye mbinguni.”

Nilikuwa nikijiuliza, matendo mema ambayo Yesu anatazamia sisi tuyatende, yaonwe na watu wote na kwa kuyaona wamtukuze Mungu tumwabuduye, ni yapi?

Bila shaka, ni yale yanayoitambulisha dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu yaani:
– Kwenda kuwatazama Yatima na wajane katika dhiki yao.
– Kujilinda na dunia pasipo mawaa. (Yak 1:26-27)

Ni matendo mema ambayo yakitendwa, Bwana Yesu anahesabu katendewa Yeye, na kutokuyatenda ni kutokumtendea Yeye! (Mt 25:35-46)
– Kuwapa chakula wenye njaa.
– Kuwanywesha wenye kiu.
– Kuwahifadhi wageni.
– Kuwavika wasio na nguo.
– Kutembelea wagonjwa na wafungwa.

* Hayo ndiyo baadhi ya matendo mema ambayo Mungu anatarajia kutoka kwetu.
* Ni hayo ambayo Neno la Mungu linasema ajuaye kuwa ni mapenzi ya Mungu asiyatende, kwake huyo ni dhambi (Yak 4:17).

Hivi unadhani unatakiwa uwe na uwezo kiasi gani, ili ufanye hayo matendo mema ambayo kwa hayo Mungu atatukuzwa? Angalia hapa: (2Kor 8:12)

” Maana, kama nia ipo, hukubaliwa
kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si
kwa kadiri ya asivyo navyo.”

TATHMINI

Hivi kama ukichunguza, hivi unadhani Katika kufanya Mema yaliyoorodheshwa hapo juu, sisi kama Kanisa tunatumika katika viwango vya kuridhisha?

Hapo katika eneo lako, hesabu vituo vya kulelea Yatima unavyovijua, ni vingapi vinamilikiwa na Kanisa?

Fuatilia watu au vikundi vya watu wanaojitolea kutembelea Mahospitalini na Magerezani, nani wengi kati ya Wana wa Mungu na hao wengine?

Wakifanya hao wengine, ni mungu yupi anatukuzwa!?

DOKEZO:

Katikati ya mwezi Septemba, wale wote wenye utayari katika wilaya ya Temeke tutatangaziana sehemu ya kukutana ili kuangalia jinsi ya kupata kibali cha kudumu cha kutembelea Hospitalini, Magerezani, Vutuo vya waathirika wa dawa za kulevya, Yatima na wengineo, walau Mara moja kwa kila mwezi, ili kuhubiri Injili kwa Neno na tendo. Pamoja na kuudhihirishia ulimwengu ya kuwa YESU YU HAI.

Baada ya kukutana watu wa Temeke, tutajulishana tufanyeje kwa walio mbali wanaohitaji kushiriki. Lakini ni vyema hapo ulipo Uzinduke iwapo ulijisahau, pima Ukristo wako!

Kama umeona ni jambo jema na ungependa kushiriki kwenye jambo hilo tunalokusudia kulianza mwezi Ujao, tafadhali weka namba yako ili nikuunganishe kwenye Group letu la WhatsApp liitwalo “WANA WA NURU”

Ubarikiwe.
By Alex E. Alex Emmanuel Bubelwa

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
3 comments on “MATENDO MEMA ALIYOYASEMA YESU NI YAPI?
  1. John Matiku says:

    Ubarikiwe kwa mafundisho mazuri!

  2. kipomajr says:

    Habari, niunge kwenye group 0764524329

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: