JE! UMEJIANDAA KWENDA MBINGUNI.

https://i0.wp.com/cdn3.whatchristianswanttoknow.com/wp-content/uploads/2013/11/Do-Christians-Go-Immediately-To-Heaven-When-They-Die.jpg

Baada ya mimi na wewe kufa, ndugu zetu watatangaza kuwa tumekufa kwenye magazeti au radio.
Ukweli ni kwamba, tumeenda kuanza maisha mengine. Yawezekana ni MBINGUNI au JEHANAM.

Ukitaka kwenda MBINGUNI ni LAZIMA ujiandae. Ila kwenda Jehanamu haina haja ya maandalizi.

Kwanini unapaswa kujiandaa?
1. Njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingia kwa njia hiyo. Mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni WACHACHE.

2. Mbinguni hakitaingia kinyonge, afanyaye machukizo, na uongo, bali walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana-kondoo (Ufunuo 21:27).

3. Viwango (standards) za kuingia mbinguni ni za Mungu na zimewekwa na Mungu na sio makanisa, hazijawekwa na wachungaji wala mitume. Usijifariji kwa maneno ya watu na kuangalia zaidi watu. HAPANA kama unachofanya ni kinyume na Biblia, Mbinguni hutaingia.

4. Lazima jina lako liwe limeandikwa kwenye kitabu cha uzima. Sio kuandikwa kwenye kitabu cha kanisa; hapana, kitabu cha uzima (Ufunuo 20:15).

JIANDAE KWA MAISHA YA BAADAE

Babu yako aliyekufa aliishi unapoishi, ila leo kafa. Nawe utakufa kama yeye alivyokufa. Jiandae kuhusu kifo kabla hujafa.

Hekima ya kifo: usikubali kufa kama baba yako kama hujui ni njia gani wamepitia. Tafuta njia sahihi wala sio kuiga njia ya wazazi wako.

MSISITIZO

Kila anayemwamini YESU anao uzima wa milele (1Yohana 5:13).

Dhambi hudanganya (Mithali 14:12).

Mshahara wa dhambi ni MAUTI (JEHANAMU) kutengwa mbali na Mungu (Warumi 6:23).

Wokovu unapatikana kwa kumwamini Yesu (Yohana 3:16).
Hakuna mtume, au kiongozi yeyote wa kidini awezaye kuokoa maisha yako. Ni YESU pekee awezaye (Ufunuo 5:4-5, 9-10).

TUBU DHAMBI ZAKO, MWALIKE YESU MOYONI MWAKO.

Barikiwa sana.
Mch. Nimrod Swai
TAG City Light Temple-Matosa.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “JE! UMEJIANDAA KWENDA MBINGUNI.
  1. Barikiwa Mtumishi, Kweli Kufa Kimwili Si Mwisho Wa Maisha Kiroho Japo Waliokufa Hawatuhusu Kitu.. Maana Biblia Inasema Usitafute Habari Kwa Wafu Wala Wapiga Bao Wala Wapiga Kite Kwa Maana Ni Chukizo Mbele Za Bwana.
    MAUTINI TU HAKUNA MAISHA YOYOTE, MPAKA YESU ATAKAPOTHIBITISHA MAISHA AKIRUDI, Wala Wafu Hawajui Lolote Huko Kuzimu.
    Bwana Yesu Asifiwe!

  2. gerson devisy says:

    T

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: