NAMNA YA KUWA TAJIRI BAADA YA KUFA

https://d1ai9qtk9p41kl.cloudfront.net/assets/db/14127878871642.jpg“Utajiri unaopatikana duniani unaishia hapahapa duniani. Siku ukifa unaacha ulivyochuma kwa nguvu, akili, muda na maisha yako yote KWENYE MIKONO YA WATU WENGINE WASIOJUA GHARAMA ULIYOLIPA KUVIPATA. Njia rahisi ya kuwa tajiri ambaye MALI YAKE HAIPOTEI AKIFA NI KWA KUWEKEZA MALI YAKO KUGUSA MAISHA YA WENGINE. Biblia inasema yafuatayo; AMSAIDIAYE MASIKINI NA KUMHURUMIA HIMKOPESHA MUNGU (Mithali 19:17). Kila Unapotumia mali yako kuweka kicheko kwenye USO WA MTU MASIKINI NA MHITAJI UNAONGEZA MKOPO KWA MUNGU, NAYE ATAKULIPA KWA TENDO LAKO HILO JEMA. Una uhakika UMEJIWEKEA HAZINA KULE WASIPOHARIBU WEZI, NONDO AU KUTU. Lakini pia Biblia inasema kuhusu KORNELIO; ALIKUWA AKIWAPA WATU SADAKA NA KUOMBA DAIMA (Matendo 10:1-3). Huyu ndugu ALIJIZOEZA KUTOA VITU KWA WATU KWA JICHO LA SADAKA. HATA AKIKUPA MAJI ANAYATOA KWA JICHO LA SADAKA. AKIMSAIDIA JIRANI MWENYE UHITAJI, HATOI MSAADA BALI SADAKA. Jifunze kila unachotoa ukitoe kwa jicho la SADAKA. Itakusaidia USITOE VITU OVYO (VISIVYOKUGUSA), na itakusaidia kuwa na MENTALITY YA KUTUMIA UTOAJI KAMA UWEKEZAJI KWENYE UFALME WA MUNGU. Acha kutoa misaada, ANZA KUTOA SADAKA KWA WATU (Misaada inaishia na asante ya aliyepokea, ila sadaka inakuwa kumbukumbu mbinguni, ungechagua lipi?). Pia Biblia inasema; WALIO MATAJIRI WA ULIMWENGU HUU UWAONYE WASIZITUMAINIE MALI ZAO BALI WAWE MATAJIRI KWA KUTOA MALI ZAO, WASHIRIKIANE NA WENGINE KWA MOYO; HUKU WAKIJIWEKEA AKIBA IWE MSINGI KWA WAKATI UJAO, ILI WAPATE UZIMA ULIO KWELIKWELI (1Timotheo 6:17-19). Jambo jingine ambalo Biblia inatufundisha kuhusu namna ya kuwekeza mali ili zisiishie siku ukifa ni hili; WEKEZA KWENYE INJILI, SAPOTI KAZI ZA MUNGU NA HUDUMA ZINAZOSAMBAZA HABARI NJEMA (Marko 10:29-30). Ukizingatia haya, UTAJIRI WAKO HAUTAISHIA SIKU YAKO YA MAZISHI”
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “NAMNA YA KUWA TAJIRI BAADA YA KUFA
  1. AMBOKILE GWAKISA says:

    NASHUKURU WATUMISHI WA BWANA, MUNGU AWABARIKI KWA MAFUNDISHO YENU KWA KWELI TUNATIWA NGUVU.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: