MAHUSIANO YA KUELEKEA NDOA

https://i1.wp.com/d236bkdxj385sg.cloudfront.net/wp-content/uploads/2012/09/black-woman-with-white-man-pf.jpg

NINI KUSUDI LA MAHUSIANO?

1. Kukutengenezea mazingira ya kujifunza kupitia kwa mtu mwingine.
Hii ina maana kuna vitu huvijui na hutavijua kuhusu wewe, Mungu, imani, mazingira, uchumi nakadhalika ukiwa peke yako, ila AKIONGEZEKA HUYU MTU kwenye maisha yako, UKILICHUKULIA KAMA DARASA UTAPATA MENGI.
Kikubwa usiwe na moyo na akili ya kujifanya UNAJUA KILA KITU.
Mungu anaweza kutumia yeyote kukufundisha.
Huyo dada/ kaka ana mengi ya kukufundisha ukiingia kwenye mahusiano kwa kusudi la KUJIFUNZA KWA MWENZIO.
(Mithali 1:5).

2. Ni nafasi ya KUMJENGA MWENZIO NA KUMUONGEZEA THAMANI.
Unapoingia kwenye mahusiano ukiwa na KUSUDI LA KUMFANYA MWENZIO KUWA BORA KULIKO ULIVYOMKUTA utakuwa umefanikiwa sana.
Hakuna mtu asiyempenda mtu anayemjenga na kumfanya kuwa bora.
Ukiingia kwenye mahusiano na huyo kaka/ dada na kumsaidia kuwa bora, utakuwa umefaulu kutimiza kusudi mojawapo la mahusiano.
(Mithali 27:17).

3. Ni wakati wa kujifunza kujali, na kutunza wengine.
Kuna watu ambao hata kujijali na kujithamini ni kazi, lakini wakiingia kwenye mahusiano wanajifunza. Mazingira yanawalazimisha kuwa watu wa kujali. Huyo mtu mmoja anakuwa darasa lako zuri la kujali na kutunza vitu akupavyo Mungu.
Yeye atunzaye mtini wake atakula matunda yake.
(Mithali 27:18).

4. Ni fursa ya kupima kama huyo mtu uliyenaye ana maono ma kusudi sawa na lako.
Biblia inasema WATU WAWILI HAWAWEZI KWENDA PAMOJA WASIPOPATANA.
Hatusubirii tuolewe au tuoe ili tugundue wake/ waume zetu wamebeba vitu tofauti na sisi.
Kusudi mojawapo kubwa la mahusiano ni hilo.
(Amosi 3:3)

HITIMISHO
“Usipojua kusudi la kitu, kukichezea/ kukitumia vibaya na kukiharibu hakukwepeki”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: