NAMNA YA KUITOA DHAMBI NDANI YAKO (ADDICTION)!

 

https://i2.wp.com/www.rippdemup.com/wp-content/uploads/2012/12/yolanda-spivey_black-woman-pretends-to-be-white-to-get-job1.jpg“Shetani hana nguvu akiwa NJE YA MTU mpaka anapopewa nafasi na mtu ya KUINGIA NDANI YAKE. Mungu alimwambia Kaini; ANGALIA DHAMBI IKO MLANGONI INAKUOTEA (Mwanzo 4:7). Mtu aliyeokoka yuko salama dhambi ikiwa nje, hata kama iko mlangoni, LAKINI akifanya kosa la KUIFUNGULIA MLANGO IKAINGIA NDANI YAKE ni mechi ngumu mno KUITOA TENA NJE YAKE. Wengi wameshindwa namna ya kuitoa na wamebaki na KUANGUKA NA KUTUBU. Anaanguka leo anatubu kesho, anaanguka kesho kutwa anatubu mtondo, halafu anaanguka mtondogoo. YAANI ROHO YA MTU INAJUA DHAMBI NI MBAYA NA HAUIPENDI (analia hata machozi, na hata kujitesa), lakini DHAMBI ILIYO NDANI YA MWILI WAKE INASUMBUA (Hapa nakumbuka alivyoielezea Paulo: Warumi 7:15-20). Dawa ya kesi ya aina hii ni KUPAMBANA NA HIYO DHAMBI IKIBIDI KIASI CHA KUMWAGA DAMU (Waebrania 12:4). Hii itakubidi UUTESE MWILI WAKO NA KUUTUMIKISHA (1Kor 9:27). Hapa PIGA MIFUNGO (Hata kama hujawahi kufunga masaa 24 FUNGA HUTAKUFA… Huwezi kufa kwa kufunga siku moja, mbili au tatu), UTASHANGAA HICHO KIDHAMBI KIMECHOMOKA… Hata ukijisikia kama ufungue, harufu ya chakula inakutamanisha WEWE KAZA TU… NJAA ITAUMA ILA HUTAKUFA… Mwisho wa siku HIYO DHAMBI ITAKOSA CHAKULA NA ITAKUFA…. Kipindi hicho cha mifungo epuka TV, redio na vitu ambavyo VINAPENDWA NA MACHO NA MASIKIO YAKO… Sikiliza MAFINDISHO, MAHUBIRI, NYIMBO ZA KUSIFU NA KUABUDU, SOMA VITABU VYA WATUMISHI WA MUNGU NA BIBLIA YAKO… HIYO DHAMBI ITAKUACHA TU… Lakini hata hiyo dhambi ikikuachia; Jizoeze kuendelea na mfumo wa KUFUNGA NA KUOMBA WALAU MARA MOJA, MBILI AU TATU KILA WIKI… Hata kama ni masaa 12 (asubuhi mpaka jioni), na JIZUIE KUANGALIA NA KUSIKILIZA VITU VINAVYOPENDWA NA MACHO NA MASIKIO… WEKEZA KWENYE VITU VYA ROHONI ZAIDI”
Muhimu: Jitahidi kuyasoma maandiko ndani ya masomo haya

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: