ATHARI YA AGANO LA KUPOTEZA USICHANA/ UVULANA WAKO KABLA YA NDOA

(MAAGANO YA KIPEPO DHIDI YAKO UNAPOFANYA UASHERATI NA KUPOTEZA UBIKRA WAKO)!

Kuna MSEMO WA WAPUMBAVU, MAJUHA NA MATAAHIRA Ambao Nimewahi Kuusoma Mahali Usemao, “VIRGINITY IS NOT DIGNITY BUT LACK OF OPPORTUNITY” Yaani Kwa Kiswahili Inasema Hivi, “UBIKIRA SI KIPIMO CHA UTU NA KUJITUNZA BALI NI KUKOSA FURSA YA MTU WA KUUONDOA”
Haya MANENO YA KIPUUZI Nimekuwa Nikiyaona Kwenye WALL NYINGI ZA AKINA DADA, Wasio Na Yesu Ndani Yao Wala Wasio Na Hofu Ya Mungu Ambao TAYARI WAO WAMEPOTEZA ‘HESHIMA’ YA UBIKRA NA WANAJARIBU KUWASHAWISHI WALIOJITUNZA KUFANYA ILI WAWE KAMA WAO… Hakika Hiyo Ni KAULI YA KIPEPO, Ambayo IMELENGA KUWASUKUMA AKINA DADA [HASA] NA AKINA KAKA PIA KUFANYA TENDO LA NDOA NJE YA NDOA, Lakini Shetani Akiwa Anakusudia KUWAINGIZA KWENYE UTEKA NA UTUMWA Kupitia LILE TENDO LA UASHERATI [MWENYE MASIKIO NA ASIKIE]!

AGANO LINAKUJAJE MTU ANAPOZINI NA KUPOTEZA UBIKRA WAKE NA NINI ATHARI ZAKE?

Biblia Inasema, “PASIPO DAMU HAKUNA AGANO”
Na Kama Ujuavyo, Kwa MTOTO WA KIKE ANAPOFANYA TENDO LA NDOA KWA MARA YA KWANZA, LAZIMA DAMU IMWAGIKE, Na Hiyo DAMU INAFUNGA AGANO ZITO SANA LINAYOANZA KUYAGHARIMU MAISHA YAKO KUANZIA MUDA ULE ULIPOMWAGA DAMU YAKO!

KWA WATOTO WA KIUME ANAPOFANYA TENDO LA NDOA YEYE SI RAHISI DAMU KUTOKA, LAKINI MBEGU ZA KIUME HUTOKA NDANI YAKE KUINGIA KWA YULE ANAYEFANYA NAYE HICHO KITENDO!
Mtoto Wa Kiume Anapofanya Tendo La Ndoa Kwa Mara Ya Kwanza Zile MBEGU ATOAZO Kibiblia ZINAITWA ‘NGUVU ZAKE NA MALIMBUKO YA UWEZO WAKE” (Mwanzo 49:3).
Hili Tunaliona Kwa Mzee Yakobo, Mwanaeo Wa Kwanza Anaitwa REUBENI, Ambaye Alimpata ALIPOFANYA TENDO LA NDOA NA MWANAMKE WAKE WA KWANZA AITWAYE LEA… Na Mzee Yakobo Anamwita Reubeni Kuwa “MALIMBUKO YA UWEZO [NGUVU] WAKE”
Hii Ni Siri Kutuonesha Kuwa Ndani Ya Mwanaume KUNA MBEGU ZA KWANZA KWA MWANAMKE WA KWANZA Ambazo Zinaitwa “MALIMBUKO YA UWEZO WAKE” Ambazo Zinasimama Kuwakilisha UWEZO WA KUZAA NA KUONGEZEKA (KUPITISHA UZAO WA WATOTO) LAKINI PIA UWEZO WA KUZAA NA KUONGEZEKA KWENYE KILA JAMBO MAISHANI MWAKE!
Mtoto Wa KIUME ANAPOFANYA UASHERATI, ANAUZA NGUVU ZAKE ZA ‘KITANDANI’ Lakini Pia Anauza, “NGUVU ZAKE ZA MASWALA YA UZAAJI NA KUENDELEZA KIZAZI” LAKINI PIA ANAUZA NA MBARAKA WAKE WA KUZAA NA KUONGEZEKA KATIKA AYAFANYAYO HAPA DUNIANI!
Na Uwezo Huo Na Nguvu Hiyo ANAIUZA NA KUIWEKA RASMI MIKONONI KWA IBILISI KISHERIA KUPITIA UASHERATI AMBAYO NI DHAMBI ILIYOFUNGUA HUO MLANGO!

KWA WOTE MABINTI NA WAVULANA
Unapopoteza UBIKIRA Wako Mambo Yafuatayo Yanatokea Maishani Mwako;

1.NAFSI YAKO INAUNGANISHWA NA HUYO ULIYEFANYA NAYE UASHERATI KISHERIA (MNAINGIA AGANO)
Ndiyo Maana Unaweza Kukuta MAMA KAOLEWA Lakini ANAMLINGANISHA MMEWE NA NA YULE MWANAUME ALIYEMBIKIRI…Au Anaweza Hata KUFIKIA HATUA YA KUZINI NJE YA NDOA NA YULE MWANAUME IKITOKEA WAKAKUTANA TENA, MAANA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO KUNA ‘KANDOA RASMI’ KANAFUNGWA PALE MTU ANAPOUPOTEZA UBIKRA WAKE!
Wako Wengi WANATOKA NJE YA NDOA Kuwarudia WALE WALIOWATOA BIKIRA Wakisema “WANAKUMBUSHIA ENZI”
Wanajua Ni DHAMBI, WANAJUA WANASALITI NDOA ZAO HALALI, LAKINI NAFSI ZAO ZILIPELEKWA HALALI KWA WALE WALIOWAONDOLEA UBIKIRA WAO, WANAKUWA WATUMWA WAO!
Kwa Wasomaji Wa BIBLIA Wanajua HABARI YA DADA KATIKA FAMILIA YA YAKOBO AITWAYE DINNA AMBAYE ALIONDOLEWA UBIKIRA NA KIJANA WA KIGENI, HALAFU GHAFLA YULE KAKA AKAJIKUTA NAFSI YAKE IMETEKWA NA DINNA KIASI CHA KUFIKIA HATUA YA KUANGAMIA YEYE NA TAIFA LAKE LAKINI SABABU IKIWA NI “NAFSI YAKE KUTEKWA” Kupitia “PENZI LA KWANZA”

2.UNAPOFANYA UASHERATI NA KUPOTEZA UBIKIRA WAKO
UNAWEZA KUJENGA UADUI NA MKAKA/MDADA ALIYEKUONDOLEA HAKO KA HAZINA KAKO;

Wasomaji Wa Biblia Watakuwa Wanazijua Habari Za AMNONI NA TAMARI…Baada Ya AMNONI Kufanya UASHERATI Na TAMARI, Ghafla ILIKUJA CHUKI YA AJABU NA ILIYOPITILIZA MOYONI MWAKE DHIDI YA TAMARI, ILHALI HAPO MWANZO ALIKUWA AKIMPENDA MNO KIASI CHA KUUGUA NA KUKATAA KULA!
Pia Nimeziona Kesi Nyingi Za Wavulana Na Wasichana Waliokuwa MAADUI KAMA PAKA NA CHUI MaraTu Baada YA kUMALIZA KUPOTEZEANA UBIKIRA!

3.MIKATABA YA KIPEPO
Unapofanya TENDO LA NDOA Kwa Mara Ya Kwanza, KWA MSICHANA DAMU INATOKA NA KWA MVULANA MBEGU ZA KIUME ZINATOKA… Hizi Ni Milango MIKUBWA SANA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO Ambayo Kile ALICHOBEBA MDADA KINARUKIA KWA MKAKA NA CHA MKAKA KINAKWENDA KWA MDADA, KUNAKUWA NA MABADILISHANO YA “MIUNGU/ ROHO” ZILIZO PANDE ZENU!
Msichana Unapokea MIUNGU INAYOLETA MATATIZO KULE KWAO NA MVULANA NAYE ANAPOKEA MIUNGU INAYOLETA MATATIZO KWENU Kupitia MLANGO HUU WA DAMU YA UBIKIRA NA MBEGU ZAKO ZA KIUME KWA MWANAMKE WAKO WA KWANZA!
Hapa Ndipo Mashambulizi Ya Kipepo Na Uharibifu Wao HUMWINGIA MTU Na Kuanza Kuharibu NURU NJEMA YA MAFANIKIO Ambayo ILIKUWEPO MAISHANI MWAKE…YAANI GIZA LINAPATA MLANGO WA KUINGIA NA KUIZUIA NURU YAKO NA KISHA UBAYA WA SHETANI NA KAZI ZAKE HUANZA KUONEKANA NDANI YA MTU…Mfano Dada Alikuwa Ametulia Au Kaka Alikuwa Ametulia, LAKINI AKIMALIZA TU KUFANYA UASHERATI NA KUPOTEZA UBIKIRA WAKE, Anaanza KURUKARUKA NA KAKA/DADA MMOJA BAADA YA MWINGINE MPAKA MNAJIULIZA NINI KIMETOKEA, LAKINI SHIDA INAKUWA NI ULE MLANGO AMBAO MAPEPO YAMEPATA KUPITIA LILE TENDO LA KUPOTEZA DAMU YA UBIKIRA AU MBEGU ZAKO ZA KWANZA KWA MWANAMKE… Kumbuka Kila UNAPOZINI NA KUTENDA TENDO LA NDOA NJE YA NDOA UNAFUNGULIA MLANGO WA KUINGIWA NA KILA NAMNA YA ROHO CHAFU…HAYA NI MAMBO YA ROHONI, MUNGU AMEKUPA NEEMA UYAJUE NA USAIDIKE!

MWISHO;
Kwa Wale Ambao Bado HAMJAPOTEZA UBIKIRA WENU, TAFADHALI MWOGOPENI MUNGU NA KUJITUNZA, MWOMBENI SANA MUNGU AWAFIKISHE SALAMA KWENYE NDOA MKAWE ZAWADI KWA WAUME NA WAKE ZENU!

KWA WALE MLIOKOSEA NA KUPOTEZA UBIKIRA WENU, KUNA SHIDA IMEINGIA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO, KUNA MATATIZO YANATOKEA KWAKO SASA AU YATAJITOKEZA MAISHANI MWAKO KUPITIA HIYO MBEGU ULIYOPANDA YA UHARIBIFU…LAZIMA UGEUZE MAMBO, LAZIMA UGEUZE SHERIA NA MAAGANO YALIYOKO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO… NENDA MBELE ZA MUNGU KWA TOBA YA MOYONI, TOBA YA KWELI, NA KISHA TUMIA MAMLAKA NA KUJITENGA NA NGUVU ZA KIPEPO ZILIZO NYUMA YA HILO TUKIO, JITOE [DISCONNECT YOURSELF] TOKA KWENYE MADHABAHU ZA KIPEPO NA KISHA TUMIA DAMU YA YESU KUHARIBU MATUMIZI YOTE YA NGUVU ZA GIZA KWENYE DAMU AU MBEGU ZAKO ‘ULIZOPOTEZA’

Kwa Ushauri Zaidi, Au Maombi Ya Ukombozi Na Kufunguliwa, Tuwasiliane Kwa Anwani Zifuatazo;
dicoka@rocketmail.com
0655 466 675 au 0753 466 675

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
2 comments on “ATHARI YA AGANO LA KUPOTEZA USICHANA/ UVULANA WAKO KABLA YA NDOA
  1. Catherine Dawson says:

    Asante kwa somo zuri

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: