KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA

https://i0.wp.com/www.homegrowntips.com/wp-content/uploads/2013/05/sprout.jpg

1. Haihitaji uwe umeokoka ili ifanye kazi kwako; Mungu huwapa mvua na jua wema na wabaya.
Na mvua na jua vikiwepo mavuno ni lazima.

2. Hata kama una picha kubwa sana na matarajio makubwa sana ya mavuno, itabaki kuwa picha mpaka utakapoanza wewe kupanda mbegu kwanza; Na si mbegu tu bali zinazoendana na unachotarajia kuvuna.

3. Uzuri wa kanuni ya kupanda na kuvuna; Unachopanda ni kidogo kutegemea na utakachovuna.
Mavuno ni mengi mno kulinganisha na mbegu unayopanda.

4. Huwezi kupata kiasi cha mavuno zaidi ya uwiano wa kiasi cha mbegu; Huwezi kupanda debe moja ukavuna magunia mia.
Ili kupata kiasi kikubwa cha mavuno inahitaji kiasi kikubwa cha mbegu.

5. Si kila mbegu iliyoingia ardhini itatoa mavuno; Inategemea na uhai na ubora wa mbegu husika.

6. Si kila mbegu inakubali kwenye kila udongo; Mbegu zina tabia ya kuchagua mazingira na aina fulani za udongo.
Usikurupuke kwenda kupanda mbegu mahali kwa vile kuna udongo, chunguza aina hiyo ya udongo inafaa au la.

7. Ubora wa utakachovuna unategemea ubora wa ulichopanda.
Unataka kilicho bora, panda kilicho bora.

8. Kuwa na mbegu bora na udongo bora na mazingira bora si uhakika wa kuvuna, Unahitaji MKONO WA MUNGU. Panda, sawa! Mwagilia, sawa! Lakini usisahau wala kupuuza nafasi ya Mungu akuzaye.

9. Hili uweze kufurahia kanuni ya kupanda na kuvuna lazima uwe mtu wa SUBIRA NA KUVUMILIA.
Ukiwa mtu wa pupa, utakata tamaa kabla ya mavuno.
Kuna muda kati ya kupanda na kuvuna.

10. Kanuni ya kupanda na kuvuna ni maalum kwa watu WALIOJIKINAI, watu ambao hawataki kuona kila kitu ili waamini kwamba watapata.
Watu wanaojua kwenye ardhi kuna wadudu, lakini bado wanaizika mbegu yao ardhini wakiamini itatoka salama.
Chembe ya ngano isipoanguka chini na kufa hukaa hali hiyohiyo, bali ikianguka n kufa huleta mavuno makubwa.

11. Kanuni ya kupanda na kuvuna inawahusu zaidi watu wanaoangalia KESHO kuliko leo.
Watu wenye mtazamo wa KIWEKEZAJI.
Watu ambao akili yao inaona LEO TU, hawawezi kupanda mbegu.

12. Kila siku, kila tukio unalofanya, kila jambo unalotenda ni mbegu.
Haijalishi ni jema au baya, uko tayari kuvuna uliyopanda au la, haizuii ukweli kwamba utavuna.
Ukipanda vitu vyema kuna mavuno mema, na kinyume chake ni sahihi.

Unapanda nini leo?
Unawapa nini watu utakaokutana nao leo na wiki hii?
Uko tayari kuvuna kila mbegu uliyopanda?
“Maisha yako ya leo ni mavuno kutokana na mbegu ulizopanda jana”
Maandiko:
Mwanzo 8:22, Isaya 55:10-11, Mhubiri 11:6, 1Wakorintho 3:6-7, Wagalatia 6:9, Ayubu 4:8, Zaburi 126:5-6.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “KANUNI YA KUPANDA NA KUVUNA
  1. tulia says:

    that is the reality for sure nobody can denied on this.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: