2016 MWAKA WA KUJIONESHA

(THE YEAR TO SHOW OFF).

https://i0.wp.com/3219a2.medialib.glogster.com/media/52/5249a9dd449769352435805a88a5883e3cbc3b2a5e83530b8e2ac420dcc749c3/amigos1sdfdfase.jpg1.Utajionyesha kwa wote WALIOKUKATIA TAMAA kuwa uko hai na umebarikiwa katika kila eneo la maisha yako.
Yusufu alishakatiwa tamaa na baba yake, ya kuwa amekufa, lakini kuna siku alijionesha kwake akiwa hai na akiwa amebarikiwa.
Itakuwa kwako mwaka huu 2016; Wote waliodhani umekufa au mambo yako yamekufa, UTAJIONESHA KWAO ukiwa hai na ukiwa umebarikiwa sana.
“…AKAJIONYESHA KWAKE…”
(Mwanzo 46:29).

2. Kuna watu wamekuwa na mashaka na wokovu wako, wamekuwa na maswali kuhusu imani yako kwa Yesu; 2016 kwa neema ya Mungu, na kwa nguvu za Roho wake mtakatifu, UTAJIONYESHA KWAO KUWA MTAKATIFU kama Baba yako wa mbinguni alivyojionyesha kuwa mtakatifu kwa Israeli huko Meriba.
(1Petro 1:15-16, Zaburi 16:3, Hesabu 20:13).

3. Mungu, Baba yako wa mbinguni ATAJIONYESHA KWAKO 2016;
a) Atajionyesha kuwa mkamilifu kwako (atajifunua kwa urefu, kimo, kina na kina chake endapo na wewe utaenenda kwa ukamilifu mwaka huu).
b) Atajionesha kwako kuwa mwenye fadhili iwapo wewe nawe utawafadhili wengine.
c) Mwenye nguvu iwapo utausafisha moyo wako na kuondoa kila kikwazo na uchafu.
(1Nyakati 16:9, 2Samweli 22:26,27).
d) Atajionyesha kwako kuwa wa ajabu; Atajifunua kwako KWA MAAJABU endapo utajishusha na kujinyenyekeza kwake.
(Ayubu 10:16).

4. 2016 UTAJIONESHA KUWA MWENYE HAKI kwa;
-Kuyakataa mambo ya aibu yaliyositirika
-Kutoenenda kwa hila
-Kutolichanganya NENO LA MUNGU na uongo
-Dhamiri za watu (mashahidi) waliokuzunguka wakikushuhudia mbele za Mungu.
(2Korintho 4:2).

5. 2016 UTAJIONESHA KUWA UMEKUBALIWA NA MUNGU, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari endapo UTALITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI.
Maana yake;
-Ukilitumia Neno la Mungu si kujitetea katika dhambi bali kuliruhusu likuguse na kukurekebisha kurudi kwenye mstari.
Usipolitumia Neno kama kichaka cha kujifichia; 2016 UTAJIONESHA KUWA UMEKUBALIWA NA MUNGU.
(2Timotheo 2:15).

6. 2016 UTAJIONYESHA KUWA KIELELEZO kwa;
-Matendo mema
-Usahihi na Ustahivu katika Mafundisho yako.
(Tito 2:7).

7. 2016 UTAJIONYESHA KWA WAKUCHUKIAO na uwepo wako kati yako utaleta majibu ya kile kilichowafanya wakakuchukia.
(1Wafalme 18:1-2).

8. 2016 UTATOKA KWENYE KILA KIFUNGO NA GIZA na UTAJIONYESHA WAZIWAZI YA KUWA UKO HURU na UTAPATA MIUJIZA/ UTAJILISHA MAHALI PASIPOWEZA KUWA NA CHAKULA.
Utastawi hata mahali ambako kibinadamu na kimazingira hapana ustawi.
(Isaya 49:9).

9. 2016 kama WAKOMA walivyokwenda KUJIONESHA kwa kuhani kuwa WAMEPONYWA; Wewe nawe UTAJIONESHA KWA WALIOKUITA TASA KWAMBA UMEZAA, WALIOKUITA MASIKINI KUWA UMETAJIRIKA, WALIOKUITA ULIYESHINDWA KUWA UMESHINDA.
Utarudi kwao KUJIONESHA KUWA JINA LAKO LIMEBADILIKA.
Utarudi kwao UKIWA NA MATOKEO ambayo hawawezi kuyapinga au kuyabishia maana YAKO KINYUME na walivyokuwa wakikuita kabla.
(Mathayo 8:4).
Kadri utakavyokuwa UNAKWENDA KATIKA SAFARI YA 2016, utagundua hilo jina walilokupa limefutika, utagundua ukoma waliokuwa wakikutenga nao umekuachia, utagundua umetakasika.
2016 haitaisha, UTAJIONESHA KWAO TENA ukiwa na matokeo tofauti.
(Luka 17:14).

“Huu ni mwaka wako, kama utatendea kazi maelekezo ya NENO LA MUNGU katika vipengele hivyo hapo juu, mwaka huu ni mwaka wako wa kujionesha”
Usisubirie nafasi ya kuonekana ijilete, 2016 toka KAJIONESHE.
Huu ni mwaka wa KUJIONESHA.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: