MAOMBI YA SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU [Day 2]

https://i0.wp.com/www.i-ccc.org/wp-content/uploads/2013/03/prayer.jpg

Day 2, 06/01/2016.
MCHANA

NEEMA YA KUFANYA NA KUWA ZAIDI YA WENGINE.

“Nami kwa NEEMA YA MUNGU nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, BALI NALIZIDI SANA KUFANYA KAZI KUPITA WAO WOTE; Wala si mimi, bali ni NEEMA YA MUNGU pamoja nami”
(1Kor 15:10).
Paulo hakupata nafasi ya kukaa na Yesu hata wiki moja. Alikuwa muuaji. Mtaabishaji wa kanisa.
Mtu ambaye Yesu hakumtaja kwenye orodha ya mitume wake kumi na mbili.
Lakini alipokutana na Yesu akielekea Dameski na kubadilishwa na kuwa mhubiri wa Injili, ALIFANYA MAMBO MAKUBWA MNO KULIKO MITUME WENGINE KUMI NA MBILI ambao walikaa na Yesu karibu miaka 4, wakila na kunywa naye, na kulala na kushinda naye.
Paulo huyu alifungua makanisa mabara mbalimbali hata Uarabuni.
Huyu Paulo ameandika karibu nusu ya vitabu vya Agano jipya.
Huyu Paulo amefanya miujiza ya kupita kawaida ambayo mitume wengine hawakuifanya (Matendo 19:11-12).
Mtu huyu anadhaniwa kuwa mtume aliyeleta watu wengi mno kwa Yesu kuliko wale mitume wengine kumi na mbili.
Hakuitwa kwenye orodha ya kumi na mbili wapendwao na Yesu, lakini NEEMA YA MUNGU ILIMFANYA KUWAPIKU WALIOITWA NA KUAMINIWA NA YESU.

Ndugu yangu, kuna neema ya kukufanya kuwa bora kuliko hata wale ambao Mungu mwenyewe kawaita.
Kuna neema ya kuwa bora kuliko hata wale ambao wana vigezo, elimu, watu wenye nafasi na kila sifa ya kufanikiwa.
Mchana wa leo, iitie neema hii ya ajabu.
Tangu nilipojua kuna neema hii ya pekee, maisha yangu hayajabaki yalivyokuwa.
Walionifahamu wakati naanza anza watakueleza.
Kila siku nakuwa mtu mpya na bora sana; Iko neema ya kukufanya kuwa na kufanya kuliko wengine.
Nakuombea mchana wa leo ukutane nayo unapoomba katika jina la Yesu.

Ukiolewa/ ukioa ndoa yako iwe bora mno na iwe ya mfano kwa sababu ya neema ya kipekee iliyoko juu yako kukutofautisha.

Kwenye huduma yako, biashara, kazini kwako, na kila eneo la maisha yako, iko NEEMA YA KUKUTOFAUTISHA NA KUKUFANYA UWE ZAIDI YA WENGINE WOTE.

Neema hii ilikuwa juu ya Yusufu… Akiwa mtoto wa kumi na moja, alikuwa kipenzi cha baba yake.
Alipokwenda utumwani Misri nyumbani kwa Potifa akawa mkuu na kukabidhiwa kuwa mkuu katika ile nyumba.
Alipokwenda gerezani akapewa kuwa mkuu wa wafungwa wote.
Alipoletwa mbele ya Farao akapewa kuwa mkuu juu ya watu wote wa Misri. Baadae akawa mkuu juu ya watu wote wa dunia yake miaka 7 ya njaa ilipokuja.
Hii ni NEEMA YA KUWA ZAIDI YA WENGINE NA KUFANYA ZAIDI YA WENGINE.
Utaiona kuanzia Mwanzo 37 hadi 50.

Mtu mwingine ambaye alikuwa na Neema hii ya ajabu ni DANIEL.
Akiwa kijana mtumwa aliyeletwa utumwani Babeli; Alionekana kuwa na akili MARA KUMI ZAIDI YA VIJANA WOTE WA BABELI.
Alitumika chini ya Wafalme wakuu watatu wa Babeli; Chini ya Nebukadreza, Beltshaza na Dario.
Alikuwa RELEVANT NA IMPORTANT kwenye zama zote hizo kwa sababu ya NEEMA YA AJABU YA KUWA ZAIDI YA WENGINE iliyokuwa juu yake.
Utayaona hayo kwenye Danieli 1 hadi 6.

Nakuombea Mungu akupe neema hii ili Mungu aonekane kupitia maisha yako.
Wale waliokujua kabla watakuja kuwa mashahidi kuwa HAKIKA SI NGUVU WALA HEKIMA YA DUNIA HII ILIYOKUFANYA HIVYO ULIVYO.
Tukutane jioni mashujaa wangu,
Siku hizi 30 za kufunga za miujiza na maajabu; Hautabaki ulipokuwa.
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: