MFUNGO WA SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU

Kusudi la Mfungo:

https://pastorjesusfigueroa.files.wordpress.com/2014/05/fasting-with-the-word-of-god.jpg?w=874&h=635
Kutafuta uso wa Mungu kwa ajili ya 2016 MWAKA WA KUJIONESHA.

Ni mfungo wa masaa 12; Ifikapo saa 12:00 jioni ruksa kufungulia.

Tunaomba muda gani;
Asubuhi muda wa chai,
Mchana muda wa lunch,
Jioni kabla ya kufungulia.

Tumeanza leo 05/01/2016 tunamaliza 04/02/2016.

Maombi ya asubuhi hii;
Utakaso wa mioyo yetu.
Zaburi 66:18-20.
“Kama NINGALIWAZA MAOVU MOYONI MWANGU…BWANA ASINGELINISIKIA…”
Moyo ambao una mambo mengi yasiyo na utukufu kama vile; kuumizwa, visasi, kutosamehe, uchungu, maumivu, majeraha, kudhalilishwa, kutelekezwa, kudhulumiwa… Unakuwa kizuizi cha kujibiwa na Mungu.
Mungu hujibu maombi kwa kuangalia hali ya moyo wa mwombaji kwanza.
Hatutajitesa bure kufunga na tusipate matokeo kisa mioyo yetu ina mambo yasiyofaa mbele za Bwana Yesu.
Tutaanza kwa kujitakasa mioyo yetu.

Angalizo;

Usifanye yale matoba ya jumla jumla, matoba ya juu kwa juu, ya kukurupuka… Hapana!

Kaa chini, tafakari maisha yako… Tangu umejielewa hadi hapo ulipo… Angalia waliokuumiza, waliokujeruhi, waliokudhalilisha, waliokudhulumu, waliokujeruhi… Halafu tengeneza… Achilia hayo… Achilia hao watu… Achilia hayo matukio!

Yeremia 17:9-10
“Moyo uwa mdanganyifu una ugonjwa wa kufisha… Ni nani awezaye kuujua? Mimi Bwana nauchunguza moyo na kuvijaribu viuno”

Mungu ana tabia ya kuangalia moyo wa muombaji kuliko maneno mazuri anayotamka, maandiko anayosema au ukiri wake.
Moyo ni kituo kikuu cha mahusiano na mawasiliano kati ya mtu na Mungu.

Mathayo 15:8
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila MIOYO YAO iko mbali na mimi”
Unapokuja mbele za Mungu, anachokiangalia cha kwanza ni moyo na si mdomo.
Kila mmoja anaweza kuongea ila si kila mtu anaweza “kuwa sawa na asemayo mdomoni” … Mungu yuko serious mno na hali ya moyo wa mtu kuliko maneno ya mdomo wa mtu.

Zaburi 73:1
“Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli (watu wake), Kwao hao WALIO SAFI MIOYO YAO”
Wema wa Mungu kwa mtu unategemea hali ya moyo wa mtu.

Zaburi 10:17
“Bwana, umeisikia tamaa ya wanyonge, UTAITENGENEZA MIOYI YAO, utalitega sikio lako”
Kabla Mungu hajakutegea sikio lake, mpe nafasi akutengeneze moyo wako kwanza!

Anza na moyo wako… Tengeneza moyo wako kwanza.

Tukutane mchana ukiwa na moyo mwingine.
Moyo uliopondeka.
(Isaya 66:1-2).
Moyo wa nyama na si wa jiwe.
(Ezekieli 11:19, Ezekieli 36:26).
Kwa kuamua kufunga tu… Maaajabu na miujiza imeanza kwako!
Mwl D.C.K
www.yesunibwana.org
NB: Muda wa lunch (saa 6:30-7:30 mchana), nitaleta maombi ya mchana.

NB: nina nafasi kadhaa za wale ambao “mlikuwa bado mnajishauri moyoni” kujiunga na mfungo huu wa siku 30, kabla ya saa 6:30 mchana ukiona uko tayari, niambie nitakuunganisha kwenye group tukimbize maelfu pamoja.
Group maalum ya whatsapp ya maombi haya; 0655 466 67

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “MFUNGO WA SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU
  1. gracembwambo says:

    Mungu akubariki kwa huduma hii nimetiwa moyo sana na mafundisho haya ya mfungo name nitayafuatilia kwa karibu japo siku nanyi tangu mwanzo.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: