SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (MFUNGO WA SIKU 30). [Day 03]

https://i1.wp.com/www.onechallenge.org/wp-content/uploads/2012/12/prayer300px.jpg

Day 3, 07/01/2016.

MCHANA

“NEEMA YA KUPATA UTAJIRI”

2Wakorintho 8:9
“Maana MMEIJUA NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO, jinsi alivyokuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ILI KWAMBA NINYI MPATE KUWA MATAJIRI KWA UMASIKINI WAKE”

Wapenzi, kuna aina mbalimbali za neema kwa mujibu wa Neno la Mungu (1Petro 4:10).
Baadhi ya hizo neema ni;
i) Neema ya wokovu
(Waefeso 2:6-8, Tito 2:11-13).
ii) Neema ya kuepushwa na mabaya yanayowapata wengine (Mwanzo 6:8, Mwanzo 19:15-22, Zaburi 91:7-10).
iii) Neema ya kukusaidia wakati wa mahitaji (Waebrania 4:16, Mathayo 14:15-21, Yohana 2:1-11).
iv) Neema ya kuwa na kufanya zaidi ya wengine.
(1Wakorintho 15:10, Zaburi 45:7-8).

Na ya tano nitakayoiongelea hapa ni hiyo toka 2Wakorintho 8:9: NEEMA YA UTAJIRI.

Ukilisoma andiko hilo, linaanza na sentensi hii; “MAANA MMEIJUA NEEMA YA BWANA WETU YESU KRISTO…”
Kisha ndipo anaendelea na kusema, “…ALIFANYIKA MASIKINI INGAWA ALIKUWA TAJIRI, ILI SISI TUWE MATAJIRI KWA UMASIKINI WAKE”

Nimekuwa nikiwasikia Wana wa Mungu wengi wakilitaja andiko hili, hasa kipengele cha mwisho. Ni mara nyingi kuwasikia wakisema; “YESU ALIFANYIKA MASIKINI ILI SISI TUWE MATAJIRI”
Bila kujua hilo tu halitoshi kufanya hiyo kitu ianze kutokea kwao.
Ni muhimu ujue huo utajiri ambao Yesu ametutengenezea umeunganishwa na NEEMA MAALUM; NEEMA YA UTAJIRI.
Na ili kuupata na kuanza kuufurahia lazima kwanza;
“UIJUE NEEMA HII YA MAALUM YA UTAJIRI”
Kama unavyozijua neema 4 nilizotaja hapo juu; Neema ya wokovu, Neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji, neema ya kutuepusha na mabaya yanayowatokea wengine na neema ya kuwa na kufanya zaidi ya wengine, LAZIMA UJUE NA KUTAMBUA UWEPO WA NEEMA HII YA UTAJIRI.
Usipoijua hii neema haiwezi kukupa matokeo.
Kweli unayoifahamu ndiyo inayokuweka huru (Yohana 8:32).
Hauwezi kuwa huru zaidi ya kiwango cha kweli ulizonazo.
UKIISHAIJUA NEEMA HII MAALUM YA UTAJIRI ni rahisi kufanya yafuatayo;

1. Utajua ni haki yako ya msalaba kutokuwa masikini tena

2. Utajua kuna utajiri wako umeachiliwa tayari na Yesu

3. Utajua kama ni neema maalum, basi niifuate na kuiomba kwenye KITI CHA NEEMA (Waebrania 4:16).
4. Hautakubali kuishi chini ya viwango hivyo maana ukijua wewe ni nani hautakubali na hautayumbishwa na wasemayo wengine au Ibilisi.

Nakuombea katika Jina la Yesu; Ukutane na NEEMA HII YA AJABU… Umasikini ukukimbie katika jina kuu la Yesu!

Maandiko ya ziada;
Warumi 10:12
“BWANA YESU ana utajiri kwa wote wamwitao”
“Yesu alichinjwa ili kupokea utajiri (kati ya vitu 7 alivyopokea), na hakuvipokea kwa ajili yake bali kwa ajili yetu sisi Kanisa (mwili wake)”
(Ufunuo 5:9-12).

Tukutane jioni kumshangilia na kumfurahia Mungu wetu kwa kumaliza siku ya tatu tukiwa na NEEMA MBALIMBALI alizonazo bila kuacha hata moja.
Mwl D.C.K
www.yesunibwana.org

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: