SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU (MFUNGO WA SIKU 30). [Day 03]

https://i2.wp.com/orlandograce.org/wp-content/uploads/2013/03/fasting-and-prayer.jpg

Day 3, 07/01/2016.

ASUBUHI

“NEEMA YA KUKUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI (MAGUMU/ SHIDA/ CHANGAMOTO/ MATATIZO)”

Waebrania 4:16
“Basi na tukikaribie KITI CHA NEEMA kwa ujasiri, ili tupewe REHEMA, NA KUPATA NEEMA YA KUTUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI”

Ni habari njema mno kujua kuwa mbinguni hakuna kiti cha hukumu tu.
Hakuna kiti cha enzi tu.
Pia kuna kiti cha neema. Kiti maalum ambacho kinaachilia neema kwa walio ndani ya Yesu.
Ukimwendea Yesu kama Mungu wa neema zote, huwa anaketi kwenye kiti hiki na kuachilia neema kwa anayeihitaji.
Ni habari njema iliyoje kujua kuwa Mungu anapenda UPOKEE NEEMA na ndiyo maana ana kiti maalum kwa ajili ya hilo; KITI CHA NEEMA.
Kama ambavyo benki kuna madirisha mbalimbali, yote yako benki lakini yana kazi tofauti au kama vile hospitali kulivyo na madirisha mengi na yana kazi tofauti, Vivyo hivyo Mungu anacho kiti maalum kwa ajili ya NEEMA.
Hii itakuonesha ni kwa kiasi gani neema ni muhimu mno ili mtu afanikiwe na afike kule Mungu amemuitia.
Angalia, hatusomi kokote kuwa mbinguni kuna KITI CHA MIUJIZA AU KITI CHA UPONYAJI AMA KITI CHA IMANI, lakini kutokana na umuhimu wa neema, Mungu ana KITI CHA NEEMA.
Na aina mojawapo ya neema anazotoa ni NEEMA YA KUTUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI.
Neema maalum ambayo tunaipokea kabla mahitaji hayajaja, na yakija yanatukuta tuko WELL EQUIPED AND EMPOWERED ili kuhakikisha kuwa TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA KATIKA MAMBO YOTE (Warumi 8:34-38).

Ni maombi yangu kwako, ifikie mahali ambako haijalishi ni hali gani inakujia au unapitia, ila kutokana na wingi wa NEEMA YA KUKUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI usiweze kusikia joto na maumivu ya hilo jambo.
Lolote litakalotokea maishani mwako, likukute tayari una NEEEMA YA KUKUSAIDIA DHIDI YA HILO HITAJI.

Kabla hitaji la divai kuisha kule Kana, tayari Yesu alishakuwa na NEEMA YA KUMSAIDIA kutatua hilo tatizo.
Walipouliza cha kufanya hakujiuliza, neema ilikuwepo tayari kukomesha hilo hitaji.
(Yohana 2:1-11).

Wakati alipohitajika kulisha wanaume elfu tano na wanawake na watoto, bila kujali hali ya kidogo kilichokuwepo, kwa sababu NEEMA YA KUMSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI ILIKUWEPO, alichukua wale samaki wawili na mikate mitano na kutoa suluhu.
(Mathayo 14:15-21).

Nakuona ukitembea katika neema hii ya ajabu.
NEEMA YA KUKUSAIDIA WAKATI WA MAHITAJI.

Tukutane mchana ukiwa umehama viwango.
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: