SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (MFUNGO WA SIKU 30). [Day 5]

https://i2.wp.com/gabrielsreport.com/wp-content/uploads/2014/09/royalty-free-stock-pictures-happy-african-american-business-man-laughing-while-showing-a-success-sign-36287029.jpg

Day 5, 09/01/2016.

ASUBUHI

“HEKIMA ISIYOWEZA KUSHINDWA NA WATESI NA WAOVU WA DUNIA HII”

“Kwa sababu mimi (Yesu) NITAWAPA KINYWA NA HEKIMA ambayo WATESI WENU WOTE hawataweza kushindana nayo wala kuishinda/ kuipinga”
(Luka 21:15).
Mmmmh! Hii ni kubwa kuliko. Hii ni ya ajabu sana.
Kumbe Yesu ana KINYWA NA HEKIMA ambayo akimpa mtu hakuna chochote kinachotesa wanadamu kitaweza kushindana naye wala kumpinga na kumshinda.

Namuona Yesu akikupa KINYWA ambacho kitazungumza kinyume na kila Shtaka la kuzimu juu yako na ukoo wako.
Namuona Mungu akikupa KINYWA NA HEKIMA YA KUHUKUMU kila mateso ya adui maishani mwako.
Ninakuona ukihukumu umasikini. Nakuona ukiyahukumu magonjwa. Nakuona kwa KINYWA NA HEKIMA hii ya ajabu ukishinda kila kesi ya Ibilisi juu ya ndoa yako.
Mungu anakupa HEKIMA ILIYOBEBA USHINDI, HEKIMA ISIYOSHINDWA NA CHOCHOTE… Lakini… Hekima hii haitapita kwenye kinywa kilichozoea kujilaani, kujikatia tamaa, kujidharau na kujiona si kitu. Hakupi tu hekima bali anakupa na KINYWA KIPYA kitakachosimama kinyume na kila namna ya uharibifu na silaha za kuzimu.
Ebu Mng’ang’anie Yesu akupe KINYWA NA HEKIMA ambayo Watesi wako waliokutesa kwa miaka mingi hawataweza kamwe kushindana nawe wala kukupinga.
Leo ni siku yako ya kupokea KINYWA NA HEKIMA HII YA AJABU ambayo WATESI WAKO HAWAWEZI KUSHINDANA NAYO WALA KUKUPINGA.
Ninaona upanga ukitoka kinywani mwako ukiwa na moto wa Hekima ya Mungu kukatilia mbali kila mtesi kwenye maisha yako.
Ninaona KINYWA CHAKO kikiachilia HEKIMA YA MBINGUNI inayotiisha na kuzima kila kazi ya adui maishani mwako na maisha ya wengine.
Pokea kinywa na hekima hii isiyoshindwa toka kwa Bwana Yesu!!

Stefano alitembea katika Hekima hii, wakashindwa kupambana naye kwa namna ya Rohoni ikabidi wamtengenezee zengwe na kumpiga kwa mawe.
“Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia, na Asia, wakaondoka na KUJADILIANA na Stefano (na kufanya vita na Stefano); LAKINI HAWAKUWEZA KUSHINDANA NA HIYO HEKIMA NA HUYO ROHO ALIYESEMA NAYE.”
(Matendo 6:9-10).

Haya yalikuwa masinagogi ya waabudu Shetani (watu walio kinyume na Yesu na kazi ya msalaba), walijikusanya toka sehemu mbalimbali kwa kusudi la kupambana na Stefano; LAKINI HAWAKUWEZA KUSHINDANA NA HEKIMA NA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKE.
Walipoona VITA YA ROHONI IMEWASHINDA wakaamua kurudi mwilini na kuwaambia watu maneno ya kuwatia hasira ili wamdhuru Stafano (Matendo 6:11-15).
Ninawaona waganga, wachawi, wasoma nyota na watoto wa Ibilisi watakaojaribu kupambana na wewe wakishindwa kuhimili HEKIMA NA ROHO ULIYENAYE ANAYEOMBA NA KUTAMKA VITU KINYUME CHAO.
Nawaona wakiambiana “tumuache huyu mtu ni mtu hatari kwetu”
Nawaona wakiachana na huduma yako, nawaona wakiachana na ndoa yako, nawaona wakikimbia na kuachia elimu yako, nawaona wakiachia destiny yako katika jina kuu la Yesu.
Upokee HEKIMA HII YA AJABU na NGUVU ZA ROHO WA MUNGU za kuwakimbiza adui zako katika jina la Yesu.

Hekima hii ilikuwa juu ya Danieli pia; wakakosa pa kumpata mpaka wakaamua kujaribu kukorofisha maisha yake ya Ibada ili apungue nguvu za rohoni wampate, lakini akakaza na mwisho wa siku wakaishia kuwa chakula cha simba.
(Danieli 6:4-24).
Ukitembea na HEKIMA HII ISIYOSHINDWA NA WABAYA utawazika waliotaka kukuzika.
Mipango yao na hila zao kinyume chako zitawarudia.
Nakuombea UPOKEE KINYWA NA HEKIMA HII YA AJABU.

Andiko la ziada:
“Mimi niliye mdogo kuliko aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; Na kuwaagiza watu wote WAJUE HABARI ZA MADARAKA (MAMLAKA YA SIRI), ambayo tangu zamani ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vyote; ILI SASA, KWA NJIA YA KANISA (MIMI NA WEWE TULIOOKOKA), HEKIMA YA MUNGU ILIYO YA NAMNA NYINGI IJULIKANE NA FALME NA MAMLAKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO;…”
(Waefeso 3:8-10).
Kupitia Wewe na Mimi (Kanisa), Mungu anataka aanza kupractice siri hii ya ajabu iliyokuwa imefichwa, ili kila FALME NA MAMLAKA YA ADUI itii chini yetu kwa kutumia HEKIMA YA MUNGU ILIYO YA NAMNA NYINGI.
Nakuona ukitembea katika hekima hii ya ajabu katika jina kuu la Yesu!

TUKUTANE BAADAE SHUJAA WANGU.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (MFUNGO WA SIKU 30). [Day 5]
  1. Kilonzo Daudi says:

    Amen!

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: