SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO) [day7]

Day 7, 11/01/2016.

ASUBUHI NA MCHANA

“UPAKO WA KUONA FURSA MAHALI AMBAKO WENGINE HAWAONI”https://i0.wp.com/www.sunuker.com/wp-content/uploads/2014/04/Africa-population.jpg

Luka 4:18-19
“… Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana AMENITIA MAFUTA (amenipa upako maalum)…NA VIPOFU WAPATE KUONA TENA…”

Kila nilipokuwa nalisoma andiko hili maalum linaloeleza baadhi ya kazi za Yesu alizokuja kufanya duniani, kila nilipokuwa nasoma kipengele hicho cha “NA VIPOFU KUPATA KUONA TENA” akili yangu ilikuwa inawaza na kuona upande mmoja wa “vipofu wa macho (optical blindness)” na sikuwa naona kuhusu “Upofu wa kutoona fursa” zilizomzunguka mtu.
Niliposoma na kuelewa kuwa hapo juu kabla ya sentensi hiyo alianza na “KUWAHUBIRIA MASIKINI HABARI NJEMA” na nilipojua alifanya hivyo kwa “YEYE KUFANYIKA MASIKINI ILI SISI TUWE MATAJIRI KWA UMASIKINI WAKE” (2Wakorintho 8:9), ndipo nilipojua huo upako wa Yesu hauishii kwa vipofu wa macho ya kawaida tu.
Nilijua YESU KATUTOA KWENYE UMASIKINI ni kweli kama yasemavyo maandiko. Na kwa hilo sina shaka kabisa… Najua na sihitaji mtu aniambie vinginevyo!
Lakini nikajua pia kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya UTAJIRI NA FURSA!
Neno la kumtoa masikini toka kwenye umasikini tayari lipo, lakini huyu masikini ASIPOONA FURSA ZILIZOMZUNGUKA AU ANAZOTENGENEZEWA NA MUNGU atabaki na umasikini wake japo tayari Yesu ameshatoa tangazo la HABARI NJEMA KWA MASIKINI.
Kupata habari njema kwenye Neno kuhusu Utajiri (Kumbukumbu 8:18, Mithali 8:17-21, Rumi 10:11-12, Ufunuo 5:12-13), Mafanikio (Zaburi 1:1-3, 3Yohana 1:2, Ayubu 36:11), LAKINI… Usipokuwa na UPAKO NA NEEMA YA KUONA FURSA zilizokuzunguka na zinazokujia kila siku, UTABAKI MASIKINI mwenye maandiko mengi mazuri na matumaini yasiyotimia!

Yeremia 17:5-6
“BWANA asema hivi, amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemuacha BWANA.
Maana atakuwa kama fukara nyikani, HATAONA MEMA YATAKAPOTOKEA (HATAONA FURSA ZINAPOKUJA); Bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi, isiyokaliwa na watu”

Athari mojawapo ya laana ni kukuzima macho ya moyo wako na nafsi yako ili usiweze kuona mema yanapotokea!
LAANA ikiwa kwenye maisha yako, inapunguza “sharpness” ya moyo na akili yako kudaka “mtandao wa fursa za mema”
Laana inakufanya uishi maisha yaliyo chini ya kiwango chako halisi, na inafanikisha hilo kwa kukuharibia au kukuziba MACHO YA KUONA MEMA YANAPOKUJA (MACHO YA KUONA FURSA)!
Jambo jingine linaloharibu macho ya fursa ni KUTEGEMEA WANADAMU WAKUTOE KIMAISHA kiasi kwamba uko tayari kupindisha hata cha Mungu ili kuwafurahisha ili tu wakupe kitu au jambo fulani.
Mtu wa namna hii ambaye ANAWATAZAMA WANADAMU WAYAFANYE MAISHA YAKE YAENDE anajikuta automatic laana imemkalia na hachomoki kwenye maisha, anabaki kuwa OMBAOMBA NA TEGEMEZI.
Kataa kuweka moyo na tumaini lako kwa wanadamu.
Kuwategemea wanadamu huleta mtego.
Mwamini Mungu aliyeruhusu uzaliwe kwamba ana mahitaji yako yote “KWA KADRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA KRISTO YESU” (Wafilipi 4:19).

Mithali 3:5-7 inatuambia;
“Mtumaini Bwana kwa MOYO WAKO WOTE wala USIZITEGEMEE AKILI ZAKO MWENYEWE, Katika njia zako zote (mambo yako yote) MKIRI YEYE NAYE ATAYANYOSHA MAPITO YAKO”

“Jizoeze KUMTUMAINI MUNGU ATUPAYE VITU VYOTE ILI TUVITUMIE KWA FURAHA…”
(1Timotheo 6:17-18).

Kuna wakati nilikuwa na kiu kubwa ya mafanikio na utajiri.
Nilinunua vitabu vingi kuhusu PROSPERITY na kusoma.
Nikajua ni mapenzi ya Mungu niwe tajiri na nifanikiwe sana kwenye kila eneo la maisha yangu.
Lakini sikujua nini cha kufanya ili vitokee.
Siku moja nikiwa nimelala, Mungu alinisemesha kwa ndoto (maono ya usiku) na kunipatia mambo matano ambayo ni FURSA ZA KUBADILI MAISHA YANGU JUMLA.
Mambo hayo ni;

1. ZAWADI YA UHAI
(The gift of life).
Mhubiri 9:4.
“Kwakuwa liko tumaini kwa yeye aendaye na wote walio hai; Maana ni afadhali MBWA ALIYE HAI kuliko SIMBA ALIYEKUFA”
-Uhai ni fursa ya ajabu;
i)Miujiza huwatokea walio hai
ii) Mungu ni Mungu wa walio hai na si Mungu wa waliokufa… Mungu yuko busy na walio hai, ukishakuwa hai kuna mkono wa Mungu kwa ajili yako.
iii) Hakuna aliyeweka rekodi au historia akiwa kaburini. Uhai ni mtaji wa lazima ili kuweka rekodi au historia njema au mbaya.
Chakula si bora kuliko uhai, mavazi si bora kuliko mwili (Mathayo 6:25-26).

2. MUDA
Hapa utakuta vitu kama Majira (vifurushi vya muda vinavyokuja na kupita, Mwanzo 8:22), Nyakati (vipindi vya muda vinavyobeba matukio mbalimbali ya mtu, mema kwa mabaya… Mhubiri 3:1-11)!
Tajiri na masikini wote wana “FURSA” hii iitwayo muda.
Masikini wa Dar es salaam na masikini wa Dar wote wana masaa 24; Jua lao linachomoza na kuzama sawasawa!
Masikini ana masaa 24, tajiri naye masaa 24 hayohayo.
Mungu yuko very fair.
Wote wana fursa hii kwa kiwango sawa.
Mmoja anaitumia kuzalisha fursa nyingine (tajiri), mwenzie anaiua au kuipoteza (masikini) na hajali!
Watu TUTAKAOTISHA KATIKA KILA ENEO ni watu wa kuheshimu na kutumia muda kwa hekima (Waefeso 5:15-17).
MUDA NI FURSA.

3. WATU
“…NITATOA WATU KWA AJILI YAKO, NA KABILA ZA WATU KWA AJILI YA MAISHA YAKO”
(Isaya 43:4).
Mungu akitaka kukufanikisha ANATOA WATU KWA AJILI YAKO.
Mungu akitaka kuyafanikisha maisha yako ANATOA KABILA ZA WATU KWA AJILI YAKO.
Mafanikio yako yamefungwa kwa watu.
Utajiri wako uko kwa watu;…”Na malango yako yatakuwa wazi mchana na usiku, hayatafungwa daima, ILI WATU WAKULETEE UTAJIRI…” (Isaya 60:11).
WATU MAISHANI MWAKO NI FURSA.
Masikini ana watu. Tajiri ana watu. Kila mtu ana watu. Wengine tunawaona kama FURSA wengine wanawaona tu kama watu tu basi!!!
Kabla WATU HAWAJAWA FURSA KWAKO lazima nawe UGUSE NA KUBARIKI MAISHA YAO.
Yaguse maisha yao kwanza. Huwezi kuvuna usipopanda.
“Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa…”
(Luka 6:38).
Wape watu utu wako, wape heshima acha dharau, wathamini, wabariki, wakubali, wape kidogo ulichonacho… Wape tabasamu lako, watie moyo, wafundishe, waombee, waelekeze wanapoweza kupata msaada… Ni mbegu za namna hii zitakazokufanya UPEWE KIPIMO CHA KUJAA, KUSHINDILIWA NA KUSUKWASUKWA… NDIVYO WATU WATAKAVYOKUPIMIA KIFUANI KWAKO!
Biblia inasema:
” UTUKUFU WA MFALME NI WINGI WA WATU WAKE; BALI UCHACHE WA WATU NI UHARIBIFU WA MKUU WAO” (Mithali 14:28).

4. UHURU WA KUAMUA NA KUCHAGUA BILA KUINGILIWA NA MUNGU AU WATU

Hakuna ambaye haamui au kuchagua.
Wewe kuamua kufunga siku hizi 30 za miujiza na maajabu ni UCHAGUZI NA UAMUZI. Nina marafiki zaidi ya 5000 facebook, group zaidi ya 15 whatsapp, website yangu ya www.yesunibwana.org ina wastani wa watu 2000 kila wiki wanaosoma mafundisho. Lakini ni watu kama 100 tu mmekubali kushiriki kuomba siku hizi 30. Uchaguzi na uamuzi ulikuwa upande wenu.
Lakini mmeamua kufunga na kuomba, na matokeo yatakuwa wazi kati yenu na ambao hawajafunga; Mtawapita mbaaali!
Ila uamuzi na uchaguzi ulikuwa wako kama wao pia walivyokuwa na uhuru kuchagua na kuamua.

Mungu ameupenda ulimwengu wote, kamtoa Yesu, lakini HAINGILII UAMUZI NA UCHAGUZI wa mtu kumpokea au kumkataa, kumwamini au kutomwamini.
Uhuru wa kuamua na kuchagua ni FURSA. Ukiitumia vema utapata baraka na mafanikio na ukiitumia vibaya huwezi kukwepa matokeo yake!
(Kumbukumbu 30:19, Yoshua 24:15).

5. FURSA YA KUMJUA MUNGU KIBINAFSI

Danieli 11:32b
“Bali WATU WAMJUAO MUNGU WAO watakuwa hodari na kutenda mambo makuu”

Ayubu 22:21
“MJUE SANA MUNGU ili uwe na amani, ndivyo mema yatakavyokujia”

Maandiko haya mawili yanaonesha vitu vya pekee kuhusu KUMJUA MUNGU na watu waliolipa gharama kuwa deep katika Mungu na siri zake.
Ni watu wa miujiza.
Ni watu ambao wanayamilki na kuyatawala maisha.
Ni watu wa aina yake kwenye dunia yao.
Nakuombea nawe UWE DEEP PANDE HIZI.
Usisahau hii;
“Mungu anataka na anakutafuta uwe rafiki yake binafsi”
(Ufunuo 3:20).
Halafu…. Hayuko mbali, yuko karibu (Yeremia 23:23), na ukimtafuta utampata (Mithali 8:17, Isaya 55:6-7, Yeremia 29:12-13).
CHUKUA HII FURSA, TWENDE ZETU.

Nikutakie siku njema shujaa wangu; Hautabaki ulipo wala hutabaki ulivyo!

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: