SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day 9]

https://i2.wp.com/www.follio.me/uploads/1449490918holyspirit.jpg

Day 9, 13/01/2016.

“USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU”

2Wakorintho 13:14
“Neema ya Bwana Yesu Kristo, na Pendo la Mungu, na USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE”

Kuna mambo makubwa matatu katika sentensi hii;
i)Neema ya Bwana Yesu Kristo
ii)Pendo la Mungu
iii) Ushirika wa Roho Mtakatifu

Asilimia kubwa tunajua na tumesikia kuhusu NEEMA na pia tumesikia mara nyingi kuhusu UPENDO WA MUNGU lakini kanisa halijafundishwa kuhusu USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU KUKAA NASI.

Neema ya Bwana Yesu imetuokoa, hiyo tunaijua.
Upendo wa Mungu Baba tunaufahamu maana ndio uliomsukuma kumtoa mwanae kwa ajili yetu.
Lakini hatujapata maarifa na elimu ya kutosha kuhusu USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU KUKAA NASI.

Yesu amefanya sehemu yake na amepaa juu ameketi juu sana mkono wa kuume wa Baba, na atarudi kutuchukua siku moja.
Upendo wa Mungu tunaujua na tumeuona kupitia kazi ya msalaba.

Aliye hapa duniani pamoja nasi muda huu ni Mungu-Roho mtakatifu.
Huyu yuko duniani “full” tangu siku ya Pentekoste (Matendo 2).
Na amekuja kukaa NDANI yetu (Yohana 14:17).
Anakaa NASI HATA MILELE (Yohana 14:16).
Anakaa JUU ya waliopewa kazi za Ufalme wa Mungu ili kuwapa nguvu zote za kukamilisha walichoitiwa (Luka 4:18).
Anakaa KATIKATI YETU kila tunapokusanyika ili kudhihirisha Uwepo wa Bwana Yesu asiyeonekana (Mathayo 18:18-20, Mathayo 28:20).

Wakristo wengi hawajawa na ushirika na huyu ROHO MTAKATIFU. Wengi wanauhisi uwepo wake wakienda kwenye ibada zenye nguvu ya Mungu (kwenye makusanyiko)!
Baada ya hapo wanarudi kuwa wanadamu kama wanadamu wengine bila badiliko na miujiza na maajabu yanayothibitisha kwamba wana Roho wa Mungu mtenda maajabu pamoja nao.

Wengine wamejitahidi, wanajua wanaye ndani yao, lakini hawana ushirika naye.
Wana Roho mtakatifu lakini mambo hayaendi.
Ni sawa na kuwa na Yesu kwenye mashua halafu unazama na Yesu kalala.
Ndivyo ilivyo kwa Waliookoka wengi, wamebaki kunena kwa lugha lakini wanazama.
Wamebeba ndani ya Roho wa miujiza na maajabu lakini ndoa haziendi, biashara hazisogei, pesa hazipatikani, wakifanya vitu vinakufa kama watu wengine!
Hii ni kwa sababu hawajaanza kumtumia huyu Roho Mtakatifu waliye naye ndani yao kwa kiwango kinachotakiwa.

Namna ya kumpa uhai/ kumuamsha Roho mtakatifu aliyelala ndani yako;

1. Amua kuishi maisha matakatifu.
Roho wa Mungu ni mtakatifu na hakai pachafu.
(Mathayo 5:8, Waebrania 12:14, 1Petro 1:15-16).

2. Kuwa Mtu wa Neno.
Neno la Mungu ndo kitendea kazi/ silaha ya Roho mtakatifu.
Neno la Mungu ndilo upanga anaotumia Roho mtakatifu kushinda vita zote za Mkristo.
(Waefeso 6:17).
Kazi ya Roho mtakatifu ni kuchambua Neno sahihi ulilojaza ndani yako la kupambana na kushinda kila vita uliyonayo.
Ndio maana yatupasa Neno la Kristo likae ndani yetu kwa wingi (Wakolosai 3:16).
Roho mtakatifu hufanya kazi ya kuthibitisha Neno la mtumishi wake (Isaya 44:26), kadri unavyofurika kwa Neno jema la Mungu utaanza kuflow mno kwenye nguvu za Mungu.

3. Kufunga na kuomba.
(Mathayo 17:19-21, Isaya 58:6-12).
Watu wote waliotembea kwenye Ushirika na Roho wa Mungu walikuwa watu wa KUFUNGA NA KUOMBA.
Muangalie Musa, Muangalie Eliya, Muangalie Danieli, Muangalie Paulo, Muangalie Esta na Modekai.
Zaidi ya wote muangalie Bwana Yesu.
WATU WA ROHONI ni watu wa kufunga na kuomba ili kumtengenezea Roho wa Mungu mazingira ya kuwatumia na kuachilia nguvu yake iliyoko ndani yao.
Kufunga huondoa ukuta wa mwili (the wall of flesh) unaozuia Roho mtakatifu asiflow kwa urahisi na kufanya vitu nje kwenye mazingira yetu.
Kadri unavyokuwa mtu wa kula kula tuuu, kula kula tuu, unamziba Roho wa Mungu asipenye toka ndani kuja kufanya miujiza nje kwenye maisha yako.

iv) Kudumu katika kuomba na kuombea watumishi wa Mungu.
(Waefeso 6:18-20, Luka 18:1, Wakolosai 4:2-3).
Kadri unavyowaombea watumishi wenye neema ya Mungu, unajikuta neema iliyoko juu yako inaanza kufanya kazi juu yako.
“Hakuna anayeutunza mzabibu na asile matunda yake”

Neno ushirika kwa kiingereza limetafsiriwa fellowship (fellow-ship)… A fellow relation.
Yaani Mungu anakuwa jamaa yako/ mtenda kazi pamoja na wewe.
Ndiyo maana anakupa haki ya kuweka mikono yako juu ya wagonjwa kwa “jina lake” halafu matokeo yawe sawa na yeye kama angekuwepo live!
Ndio maana unaweza kumuamuru pepo atoke kwa jina la Yesu na akatoka kwa sababu kuna “ujamaa” kati yako na Yeye!
Natamani uongezeke na kuzidi.
Ifikie hatua ujae Mungu Roho Mtakatifu na kufanya kila anachoweza kufanya huyu Roho wa Mungu aliyeko ndani yako.
Kivuli chako kiponye wagonjwa, utakavyovigusa vibebe nguvu ya Roho wa Mungu.
Tamani kukua katika USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU.

NB: Roho mtakatifu yupo, yuko hai kama mimi na wewe japo haonekani kwa macho ya kibinadamu.
Anaongea (Matendo 13:2).
Anahuzunishwa (1Wathesalonike 5:19, Isaya 63:10).
Anafundisha na kukumbusha(Yohana 14:26).
Anaongoza (Warumi 8:14).
Anachukua taarifa kutoka kwa Bwana Yesu na kwa Mungu Baba na kutuambia nini Mungu anawaza na kutaka juu yetu na maisha yetu (Yohana 16:13-15).
Anafunua hata siri za moyo wa Mungu (1Wakorintho 2:10-12).

Una mengi utapata ukianza kumuomba Roho mtakatifu ajifunue kwako na awe na Ushirika na wewe.
Muite Roho mtakatifu.
Mwambie unatambua uwepo wake.
Mwambie unampenda kuliko uhai wako.
Mwambie unazipenda karama na vipawa vyake.
Jizoeze kuongea naye kwa upendo na ukimya.
Tenga muda wa ukimya, msifie, muabudu, mtukuze, mpe nafasi aseme na wewe.
Ushirika na Urafiki hujengwa.
Fanya sehemu yako na hakika Roho wa Mungu atajifunua kwako kwa viwango vya juu.

Usisahau hii; Roho Mtakatifu ni haki yako kabisaaaa wala si ombi.
Roho mtakatifu ni zawadi yako toka kwa Mungu.
(Luka 11:9-13, Matendo 2:38-39).

Nakuona ukitembea katika viwango vya juu vya ushirika na Roho wa Mungu.

WEWE NI MTU MKUU SANA, NI SHUJAA WA MUNGU.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: