SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA. (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day 10]

resurrected-christ-with-people-1103021-print

Day 10, 14/01/2016.

“UPAKO WA KUKUTANGAZA/ WA KUKUFANYA UJULIKANE

Luka 4:14
“Yesu akarudi KWA NGUVU ZA ROHO, akaenda Galilaya; HABARI ZAKE ZIKAENEA KATIKA NCHI ZOTE ZA KANDOKANDO”

Sikuwa ninajua hapo kabla kwamba UPAKO kazi yake moja ni KUENEZA HABARI ZA ALIYENAO/ KUMTANGAZA.
Wakati huo kama kijana mdogo aliyeanza kazi ya Ualimu wa Neno la Mungu nilikuwa na shauku ya KUJULIKANA na pia KAZI YANGU KUTAMBULIKA.
Nilitamani watu wajue kuwa nipo, na wajue kuwa na kitu/ vitu vya tofauti linapokuja suala la Ufundishaji wa Neno la Mungu na Utendaji wa karama za Roho mtakatifu.
Wakati naendelea kusoma na kupitia Biblia yangu niligindua NJIA RAHISI YA KUJULIKANA/ KUTAMBULIKA na ITAKAYONITANGAZA NA KAZI HII YA MUNGU NINAYOIFANYA ni kuwa na Upako maalum ambao UNAENEZA HABARI ZANGU hata mimi nisipopajua na ambapo sijawahi kufika.
Kabla ya Yesu KURUDI KATIKA NGUVU ZA ROHO (UPAKO MAALUM), kila mtu alimchukulia “poa” kama wasemavyo watoto wa mjini!
Lakini alipokutana na upako huu maalum, HAKUHITAJI MATANGAZO KUJITANGAZA, HAKUITA WATU WAJE ALIKO.
“Habari zake (huduma, maisha yake binafsi na kila alichoganya) zilienea kila kona ya nchi zilizokuwa karibu na Israeli”
Kuna Upako maalum ndugu yangu unaoweza kuitangaza huduma yako.
Kuna upako maalum ndugu yangu unaoweza kuitangaza biashara yako.
Kuna upako maalum rafiki ambao unaweza kutangaza kazi yako kwenye ofisi na kampuni uliyoajiriwa.

Huu upako ulikuwa juu ya Yusufu mwana wa Yakobo.
Akiwa kijana mpya na mwajiriwa mpya (mtumwa) kwenye nyumba ya Potifa, UPAKO MAALUM ulimfanya kutambulika na kupanda chati harakaharaka.
Mwisho wa siku Boss alipogundua kuwa mambo yake yanakwenda kwa sababu ya Yusufu, alimpa kuwa mkuu wa kila kitu nyumbani kwake.
Upako ULIMFANYIA PROMO.
(Mwanzo 39:1-6).
Hata akiwa gerezani Upako huu maalum ulimpigia debe akawa kiongozi wa Wafungwa wengine wote.
Kama haitoshi, UPAKO ULIMFANYIA PROMO MBELE YA FARAO akawa Waziri mkuu Misri na baadaye njaa ilipokuja AKATAWALA DUNIA YOTE kwa sababu aliukamata uchumi wote wa dunia kipindi hicho!
Huu ndio Upako wa kukutangaza, kukutambulisha na kukufanya ujulikane!

Nakumbuka hata Daudi alikuwa na UPAKO HUU MAALUM; Alipopakwa mafuta na Samweli, ROHO YA BWANA ILIKUJA JUU YAKE KWA NGUVU TANGU SIKU HIYO (1Samweli 16:13).
Nguvu hii ya Mungu iliyokuja juu ya Daudi ilianza KUMTANGAZA NA KUMTAFUTIA SOKO.
Alikuwa mpiga kinanda mzuri lakini hakuonekana wala “kipawa chake hakikumleta mbele ya wakuu” mpaka pale ALIPOTIWA MAFUTA NA NGUVU ZA MUNGU KUJA JUU YAKE ndipo alipoanza kuuzika.
Habari zake hazikuishia kule machungani, wala nyumbani kwa Yese; Upako huu maalum ULIMPROMOTE mbele ya Mfalme Sauli bila yeye kujua wala kuwepo.
Kwa mara ya kwanza akaitwa Ikulu kuja KUTUMBUIZA.
Kumbe unaweza kuwa na karama, vipawa na huduma kubwa sana, lakini kama HAUTAKUWA NA UPAKO MAALUMU WA KUKUTANGAZA HAUTAFIKA KOKOTE.
Utaishia hapo mtaani kwenu!
“Ndipo akajibu mmoja wa watumishi wa Mfalme, akasema, Tazama, NIMEMWONA MWANA MMOJA WA YESE, Mbethlehemi, ALIYE STADI WA KUPIGA KINUBI, TENA NI MTU SHUJAA, HODARI WA VITA, ANENAYE KWA BUSARA, MTU MZURI, AMBAYE BWANA YU PAMOJA NAYE. Basi Sauli akampelekea Yese wajumbe kusema, Nipelekee Daudi mwanao aliye pamoja na kondoo….”
(1Samweli 16:18-23).
Maisha ya Daudi yaligeuka kama ndoto.
Ni asubuhi ametoka nyumbani kuelekea machungani kulisha kondoo wachache wa baba yake, halafu mchana ANAHITAJIKA IKULU kwa Sauli.
Upako maalum wa kumtangaza ULIPELEKA CV YAKE HALISI ambayo hakuna aliyekuwa akiijua.
Ilisema Daudi ni mtu hodari wa vita japo hakuwahi kuua hata askari mmoja vitani.
Ilisema Daudi ni stadi wa kupiga kinubi ingawa familia yake na jamii yake haikuwahi kuwaza kuwa hicho kipawa kitamketisha na wakuu.
Hawakuwahi kumuona lakini bado walisema ananena kwa busara!
Upako huu wa ajabu unaeleza sifa zako hata zile ambazo hazijaanza kuonekana, na kuwafanya wanaosikia washindwe kukunyima nafasi au upendeleo!

Sio hili tu, alipompiga na kumuua Goliati peke yake (mtu mmoja), Upako huu maalum wa kutangaza na kumtambulisha mtu ulimfanya asifiwe kila kona na kila mtu kwamba “kaua makumi elfu” na Mfalme Sauli kaua “Elfu” (1Samweli 18:6-8).
Muda mchache uliopita gumzo la Israeli lilikuwa ni Mfalme Sauli lakini ndani ya muda usiofika siku moja, tayari Upako wa kutambulisha na kutangaza ulishamfanya Daudi kuwa TALK OF THE NATION!

Nakuona Ukipokea upako huu wa ajabu.
Hautahitaji kujieleza sana ili ukubalike.
Hautahitaji matangazo wala msaada wa mtu kupata cheo au nafasi; Upako huu maalumu ukiupata utakutambulisha!

Danieli alipoupata upako huu, hakuhitaji matangazo ili kutambulika kule Babeli; Alikuwa Waziri mkuu wa serikali zote tatu za Babeli katika kipindi chake cha maisha.
Kila mtu alisema “Roho bora ya Miungu watakatifu iko ndani yake”
Hakuhitaji kupiga kampeni.
Hakuhitaji flyers, tayari upako ulikuwa umeshamfanya a fly high!
Hakuhitaji posters, upako ulishampa post!

Nakuona ukielekea kwenye viwango hivyo.
Dunia italazimika kukujua.
Wanaokupenda na wasiokupenda watalazimika kukutazama na kukushangilia.
Nauona upako huu wa ajabu ukikufanyia kazi.
Mungu akupake mafuta mabichi ya ajabu yatakayokufanya UJULIKANE NA KUTAMBULIKA.

“Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwahiyo wanawali hukupenda”
(Wimbo Ulio Bora 1:3).
Ukiupata upako huu (manukato ya Roho mtakatifu) yatanukia na kuvutia watu kwa niaba yako.
Upako una harufu i see, na hiyo harufu haikwepeki, inavuta watu (wanawali)!
Upako unafanya JINA LAKO liwe kama MARHAMU (PAFYUMU) ILIYOFUNGULIWA.
Imagine Jina lako linukie namna hiyo.
Huu ndio upako maalum unaotangaza na kutambulisha mtu.
Nakuombea Mungu akujibu na upako huu uanze kukufanyia kazi katika jina la Yesu Kristo!

WEWE NI MKUU, WEWE NI SHUJAA NA MBARIKIWA!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: