SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 11]

15/01/2016.https://i1.wp.com/36.media.tumblr.com/5f93035034da332d066429a9d14d3b38/tumblr_nubz3i8fzt1tx2zquo1_500.jpg

“AKILI YA KIUNGU (DIVINE MENTAL ABILITIES)”

2Timotheo 2:7
“Yafahamuni sana haya nikuambiayo, kwa maana MUNGU ATAKUPA AKILI KATIKA MAMBO YOTE”

Hii si akili ya kurithi kwa mama na baba.
Hii si akili ya kutokana na mazingira uliyolelewa au kukulia.
Hii si akili ya kusomea darasani.
Hii si akili ya certificate, diploma, degree, masters au Phd.
Hii ni akili bora kutoka mbinguni.
Hii ni akili ambayo Maprofesa hawana, wasomi na wataalam wa dunia hii hawana.
Hii ni akili ya Mungu mwenyewe.
Unaipata toka kwa Mungu (“KWA MAANA BWANA ATAKUPA AKILI…”).
Ni akili inayokufanya uwe kinara katika mambo yote.
Ni akili inayokufanya uwe kinara rohoni.
Uwe kinara kwenye uchumi na fedha.
Uwe baba/ mama na mme/ mke wa aina yake.
Hii ni akili ya Kiungu kutoka kwa Mungu aliye hai.

Ayubu 32:8
“Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, NA PUMZI ZA MWENYEZI HUWAPA AKILI”

Hii si akili ya kawaida.
Hii ni akili inayokuja ndani ya mtu kutoka kwa ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye PUMZI YA MUNGU.
Roho mtakatifu ni maarufu katika suala zima la kuwapa watu akili zisizokuwa za kawaida.
Iko mifano kadhaa kwenye Biblia;

Suleimani:
“MUNGU AKAMPA SULEIMANI hekima, NA AKILI NYINGI SANA, na moyo mkuu, kama ulioko pwani”
(1Wafalme 4:29).
Ukilisoma hili andiko, utagundua haya yafuatayo;
i) Alipewa hekima kama mchanga ulioko pwani
ii) Alipewa akili nyingi sana, kama mchanga ulioko pwani
iii)Alipewa moyo mkuu (moyo wa kukabili kila habari mbaya, changamoto na mapito bila kuathirika wala kutetereka; Zaburi 112:6-8).
Hivi vyote vipo hata leo, kama umenielewa na umedaka hii siri unaweza kuviomba na ukavipokea bila shaka kabisa!

Danieli, Shedraka, Meshaki na Abednego:

“Basi kwa habari ya hao vijana wanne, MUNGU ALIWAPA MAARIFA NA UJUZI KATIKA ELIMU NA HEKIMA; Danieli naye alikuwa na UFAHAMU KATIKA MAONO YOTE NA NDOTO”
Sijui ukisoma andiko kama hilo unajisikiaje?
Mimi najisikia moto unawaka ndani yangu.
Kumbe Mungu ANA MGAO HADI KWENYE MAMBO HAYA??
Kwanini Waliookoka hatuambiwi haya?
Kwanini Wachungaji na walimu wetu hawasisitizi katika maeneo haya?
Hivi tukijua kwamba kumbe Mungu anaweza kutupa MAARIFA NA UJUZI KATIKA ELIMU NA HEKIMA tutakuwa watu wa namna gani? Dunia itatutafuta kama ilivyomtafuta Suleimani na Danieli hakika!
Mungu akitupa UFAHAMU KATIKA MAONO YOTE NA NDOTO hivi tutapata na kujua siri ngapi ambazo zinatupita kwa sababu tu hatuelewi ndoto tunazoota??
Je, ni wangapi tutawasaidia na kuwavusha kwa kutafsiri ndoto zao kama alivyofanya Yusufu au Danieli?
Nataka ukasirike, usiridhike, iamshe hasira ndani yako ya kumtafuta Mungu kama kichaa, mpaka utakapoona hivi vitu vinatenda kazi ndani yako kwa viwango vya ajabu sana!

Bezaleli mwana wa Huri:
“Bwana akanena na Musa na kumwambia, Angalia nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; NAMI (MIMI MUNGU) NIMEMJAZA ROHO YA MUNGU, KATIKA HEKIMA, NA MAARIFA, NA UJUZI, NA MAMBO YA KAZI YA KILA AINA, ILI ABUNI, KUWA FUNDI WA DHAHABU, NA WA FEDHA, NA WA SHABA, NA KUKATA VITO KWA KUTIWA MAHALI, NA KUCHORA MITI, NA KUFANYA KAZI YA USTADI IWAYO YOTE”
(Kutoka 31:1-5).
Hii AKILI YA MBINGUNI ni kiboko aiseee!!
Imagine huyu ndugu hakwenda chuo chochote lakini ghafla UPAKO WA ROHO WA MUNGU ukamfanya awe na akili za ajabu za kufanya mambo yafuatayo;
1. Kufanya kazi ya kila namna
2. Kubuni kazi za ustadi (designing)!
3. Kuwa fundi wa dhahabu, fedha na shaba (sonara)!
4. Kukata vito (smith).
5. Kuchora miti (pictograms and drawings)!
6. Kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.
Huyu jamaa alikuwa hatari sana.
Hii akili naitaka sana, unajua kila kitu.
Unaweza kufanya chochote.
Hii akili ya Kiungu si ya kawaida.
Huwezi kuwa na AKILI HII ukawa masikini.
Huwezi kuwa na AKILI HII halafu dunia isijue kwamba upo.
Mbona dunia nzima itakutafuta?
Mbona kazi zako zitazungumza kwa niaba yako?
Haaa!
Nakuona ukiishangaza dunia yako kwa sababu ya AKILI YA KIUNGU utakayoipokea sawa na Neno la Mungu lilivyotufunulia.
Utakuwa na akili ya ajabu sana.
“…BWANA ATAKUPA AKILI KATIKA MAMBO YOTE”

WEWE NI SHUJAA, WEWE NI MTU BORA, WEWE NI MKUU!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: