SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 12]

https://www.mercyships.org/wp-content/uploads/2014/08/oral-health-care-smiles.jpg

Day 12, 16/01/2016.

“UPAKO MAALUMU WA KUTUNZA MWILI WAKO (ANOINTING TO KEEP AND REPAIR YOUR PHYSICAL BODY)”

Warumi 8:11
“Lakini, ikiwa ROHO YAKE yeye aliyemfufua Yesu katika wafu ANAKAA NDANI YENU, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ATAIHUISHA NA MIILI YENU ILIYO KATIKA HALI YA KUFA, kwa ROHO WAKE aliye ndani yenu”

Wakati nimeokoka sikuwa najua Mungu anajali wala kuthamini MWILI WA MTU ALIYEOKOKA. Kanisani kwangu tulisisitizwa Mungu anaangalia roho na si mwili kwa sababu mwili (damu na nyama) hautaurithi uzima wa milele.
Nakubali kabisa kuwa mwili hautaurithi uzima wa milele, walikuwa sahihi kabisa.
Lakini usahihi huo haukujitosheleza kwa marefu na mapana yake.
Niliposoma andiko hili la Warumi 8:11 nililiangalia mara mbili tatu.
Kwanza nilidhani nimesoma vibaya.
Nilidhani inasema ROHO WAKE ALIYEMO NDANI YETU ATAHUISHA ROHO ZETU.
Nikarudia kusoma na kusoma na kusoma nikaona mwishowe ROHO MTAKATIFU ALIYEMO NDANI YETU ANAWAJIBIKA KUHUISHA (KUIPA UZIMA) MIILI YA WOTE WALIOMWAMINI YESU KRISTO.

Nilipokuwa nikiendelea kusoma niligundua kuwa ALIYEUFUFUA NA KUUPA UHAI MWILI WA YESU NI ROHO MTAKATIFU.
Niliwaza na kutafakari kuhusu KUSULUBISHWA kwa Yesu, alivyoteswa na kuharibiwa sana mwili wake, ikiwemo kupigwa kwa mijeledi, kuchomwa mkuki, kubeba msalaba, kuburuzwa na mateso mengine makali.
Lakini siku ya tatu alipofufuliwa na ROHO MTAKATIFU kila kitu kwenye mwili wake kilirudi kana kwamba hakuwahi kuteswa au kusulubiwa.
Mungu alibakiza alama za misumari na mkuki kwa ajili ya ushuhuda.
Lakini huyu Yesu alikuwa ameponywa kila eneo na ROHO MTAKATIFU ndani ya sekunde chache za kufufuka.
Alipotoka nje (Yesu), hata akina Mariamu walishindwa kumtambua wakadhani ni Mlinzi wa kaburi, wakamsihi awaonyeshe alipomuweka Yesu wasijue ni Yesu mwenyewe.
Alikuwa FIT SANA kiasi kwamba hawa akina mama wasingeamini kwamba ule mwili uliosulubishwa uko mbele yao ukiwa mzima kabisa bila kasoro; HIKI NDICHO ANACHOWEZA KUFANYA ROHO MTAKATIFU!!!

Baadae niliendelea kuitafakari Yohana 11, Habari za Lazaro wa Bethania.
Huyu ndugu alikufa na alikuwa kaburini kwa siku nne.
Ndugu zake walisema ananuka sasa (maana yake ameoza).
Lakini kwa kauli moja ya Yesu, ROHO MTAKATIFU ALIMFUFUA NA KUUPONYA MWILI WOTE KAMA NDOTO VILE.
Viungo vilivyokuwa vimeoza vilipata uhai ndani ya sekunde tu baada ya Neno “Lazaro njoo” kutamkwa!!
HII NDIYO KAZI YA ROHO MTAKATIFU LINAPOKUJA SUALA LA KUPONYA MIILI YA WATAKATIFU.

Kinachotuponza kama watu waliookoka na Miili yetu kuendelea kuteswa na magonjwa ni kwa sababu ya KUTOJUA KWELI KAMA HIZI.
Lakini kwa waliojua wengi wamekuwa hawaamini kuwa Neno la Mungu ni kweli na lilichosema kuhusu Roho mtakatifu na miili yao ni sahihi!!
Ni wakati wa kuamka na kuacha mapokeo ya wanadamu na kuling’ang’ania Neno la Mungu.

Binafsi nina miaka 6 sasa nimeacha kuugua na kuwa rafiki wa magonjwa tangu nilipojua siri hii.
Kumbe Roho mtakatifu aliyemo ndani yangu ana kazi ya KUHUISHA MWILI WANGU (KUUPA UHAI), na si roho yangu na nafsi yangu tu.
Nimeondoa mipaka juu ya nguvu na utendaji wa Roho mtakatifu na nimemruhusu awe “Bwana aniponyaye” (Kutoka 15:26).
Sisubirii niugue ili niombe uponyaji.
Huwa namuambia nirekebishe na kuhuisha kila eneo langu lenye kasoro.
Na nimekuwa nikiishi kwenye AFYA YA KIUNGU (DIVINE HEALTH) kwa miaka zaidi ya sita sasa na sina mpango wa kuumwa wala kuugua.
Nimepata tiba ya kudumu ya afya yangu.

3Yohana 1:2
“Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote NA KUWA NA AFYA YAKO kama roho yako ifanikiwavyo”
Mapenzi ya Mungu ya kwanza si kutuponya!
Mapenzi ya kwanza ya Mungu ni TUWE NA AFYA ZETU.
YAANI TUKAE BILA MAGONJWA kwa kadri tunavyoendelea kuwa deep katika Neno lake na ushirika naye!
Ndugu yangu kuna NGUVU YA KIUNGU MAALUM KABISA KWA AJILI YA KUTUNZA, KUPONYA NA KUREKEBISHA KASORO YOYOTE KWENYE MWILI WAKO.

Ayubu 33:4
“ROHO YA MUNGU IMENIUMBA, na pumzi za mwenyezi hunipa uhai”
Siku nilipoliona andiko hili nililia kwa uchungu!
Niliumia kwanini sikuliona au sikuwa naliona mapema?
Kwanini sikuona ufunuo unaohusu hali ya mwili wangu kwenye hilo andiko tangu mapema?
Nakumbuka wakati huo nilikuwa naugua malaria hata mara tatu kila mwezi… Nilipoliona na Mungu akanifunua macho lilinitoa sehemu na kukata jumla uonevu wa kuzimu kupitia magonjwa!

Niligundua kwa mujibu wa Ayubu 33:4, kumbe ROHO MTAKATIFU NDIYE ALIYENIUMBA.
Kama ni muumbaji na ANAKAA NDANI YANGU SASA baada ya kuokoka, basi anaweza kurekebisha, kukarabati na hata kuumba chochote kwenye mwili wangu.
Tangu wakati huo nimekuwa nikimuamini Roho wa Mungu kufanya SUPERNATURAL OBSERVATION AND PRESERVATION kwenye mwili wangu na hakika nimehama jumla kwenye orodha ya wanaofahamiana na bwana magonjwa!

Hakika ukiifahamu kweli hiyo kweli inakuweka huru kwenye hilo eneo ulilopata nuru.
(Yohana 8:32).

Ninakuombea uudake ufunuo huu na kuufanyia kazi.

Imagine mtu kama Musa, Ibilisi aligombea hadi mwili wake alipokufa (Yuda 1:9).

Elisha alipokufa, alikuwa na nguvu hii nyingi mno hadi kwenye mifupa yake.
Kiasi kwamba maiti ilipotupwa kwenye kaburi lenye mifupa iliyooza ya Elisha ilifufuka.
( 2Wafalme 13:21).
Natamani kila aliyeokoka ajae upako huu maalum mifupani mwake: MAGONJWA YATAOMBA POO!

Yesu alitembea kwenye upako huu.
Hakuna sehemu yenye rekodi au ushahidi kwamba Yesu aliugua au alilazwa au alikuwa hoi kwa ugonjwa.
Alitembea na haya mafuta maalumu ya kutunza na kuhuisha mwili wake.

Nakuombea hii nguvu ikuguse na kugeuza hali ya mwili wako.
Roho mtakatifu aamke ndani yako na kuanza kuhukumu kila chenye kuhatarisha hekalu la Mungu.
Umebarikiwa.
WEWE NI MTU MKUU, WEWE NI SHUJAA.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: