SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 13]

hungry-lion-500x375

“ROHO YA UJASIRI”

Mithali 28:1
“Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni WAJASIRI kama simba”

“Basi msiutupe UJASIRI WENU kwa maana una thawabu kuu”
(Waebrania 10:35).

” …na UJASIRI mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu”
(1Timotheo 3:13).

“Wapenzi mioyo yetu isipotuhukumu, TUNA UJASIRI kwa Mungu”
(1Yohana 3:21).

Ujasiri ni roho njema toka kwa Mungu.
Ni kinyume na hofu, woga na mashaka.
Biblia inasema “waovu” hawana ujasiri na hukimbia hata bila kufuatiwa na mtu/ bila kukimbizwa na mtu.

Kila aliyeokoka ni mwenye haki wa Mungu na amefanyika haki ya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu (2Wakorintho 5:21, Warumi 8:33-34).
Kujua kuwa umesamehewa dhambi zako (Wakolosai 1:13-14), Yesu amezichukua kama zake msalabani ili uwe mfu kwa mambo ya dhambi (1Petro 2:24), na umefanyika mtu wa nyumbani kwa Mungu (Waefeso 2:19), itakupa ujasiri wa kuyakabili maisha bila hofu wala mashaka yoyote.
Na itakupa ujasiri wa kumsogelea Mungu kama Baba yako mpenzi (Waebrania 10:19).
Ujasiri huzaa miujiza mingine.
Mwanamke aliyetokwa na damu alichukua hatua ya ujasiri na kuvunja sheria kuuendea muujiza wake na alipokea, kama angeliogopa angekufa na tatizo lake (Marko 5:28-34).
Bila ujasiri Daudi asingelimshinda Goliati na kupata fursa alizokusudiwa na Mungu (1Samweli 17).
Joshua na Kalebu wangepoteza ujasiri wao, wangekufa pamoja na wapelelezi wengine 10 pamoja na wote walioingiwa na woga kwa sababu ya majitu. Ujasiri wao uliwapa kuingia na kumilki nchi ya maziwa na asali (Hesabu 13, Hesabu 14).

KWANINI UJASIRI?

1. Ujaasiri unakutengenezea mazingira mazuri ya kuwasiliana na kushirikiana na Mungu.
(Waebrania 10:19, 1Yohana 5:14, 1Yohana 3:21).

2. Ujasiri unarahisisha kazi ya kuhubiri injili na kuwafikia wengine kwa habari njema za Yesu.
(Waefeso 6:19-20, Matendo 18:26, Matendo 28:31, Matendo 4:29,31).

3. Ujasiri unatufanya tutiishe na kuweka chini yetu kila nguvu za Ibilisi.
Ukiwa na hofu, woga au mashaka huwezi kushinda dhidi ya nguvu za giza.
Yesu alizishinda enzi na mamlaka “kwa ujasiri” nasi tunalinda ushindi huo kwa ujasiri.
(Wakolosai 2:15).

4. Huwezi kumilki bila ujasiri.
Joshua aliambiwa hilo na Mungu.
(Yoshua 1:6-7).

NAMNA YA KUPATA UJASIRI;

1. Utakatifu
“Mioyo yetu isipotuhukumu tunao ujasiri mbele za Mungu”
(1Yohana 3:21, Mithali 28:1).

2. Kuamini katika nguvu ya damu ya Yesu kututakasa na kutukamilisha na kutupa kusimama mbele za BWANA bila hatia wala mawaa (Waebrania 10:19).
Biblia inasema kwa “toleo moja tu” la damu yake (Yesu), ametukamilisha (Waebrania 10:12,14).
Iamini sadaka ya damu ya Yesu!

3. Kuwa mtu wa Neno na amini kile limesema peke yake.
Imani hukimbiza mashaka, hufukuza kutokuamini.
Mashaka na kutoamini ni vyanzo vya hofu bali IMANI KATIKA NENO LA MUNGU huinua kiwango cha Ujasiri wa aaminiye (Warumi 10:17, Wakolosai 3:16, Mathayo 22:29, Yohana 8:32).

4. Pangua kila wazo na fikira inayokuondolea ujasiri (2Wakorintho 10:3-4, Wafilipi 4:8), na tenga muda mwingi kujikumbusha wewe ni nani ndani ya Kristo (1Petro 2:9, Waefeso 2:19, 1Yohana 3:1-3).

Mungu anatarajia uwe jasiri kama simba (Mithali 28:1), kwa sababu Yesu Kristo aliyeko ndani yako ni SIMBA WA KABILA LA YUDA (Ufunuo 5:5)!
Ukija kwa Yesu uwe kondoo wake (Yohana 10, Zaburi 23:1-3), LAKINI unapo-deal na Ibilisi au majaribu na hila za Shetani usikae kikondoo kondoo kaa kwenye nafasi yako kama simba aliyetokana na SIMBA WA YUDA, YESU KRISTO!
Abudu mbele za BWANA kama kondoo ila pambana na adui kama simba.
Vaa ujasiri wako na kuhakikisha Ibilisi anakaa chini ya miguu yako (Warumi 16:20).
Usimpe Ibilisi nafasi (Waefeso 4:27), Bali kwa MPINGE HUYO UKIWA THABITI KATIKA IMANI (UJASIRI)…1Petro 5:8-9.
Umebarikiwa,
WEWE NI SHUJAA, NI MTU MKUU NA MTU WA MIUJIZA.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: