SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA. (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 14 ]

https://i1.wp.com/www.virgin.com/sites/default/files/Articles/Entrepreneur%20Getty/leader.jpg

18/01/2016.

“UPAKO WA UONGOZI (LEADERSHIP ANOINTING)”

Uongozi kwa mtu aliyeokoka HAUKWEPEKI.
Dunia tunayoishi ina uhaba wa watu sahihi.
Watu wacha Mungu, wa kweli, wanaopenda na kusimamia haki, waadilifu na wanaosimama upande wa haki.
Watu pekee ambao wanaweza kuisaidia hii dunia kuendelea kuwa mahali salama pa kuishi ni WENYE HAKI.
Na wenye haki ni wale walionunuliwa kwa damu ya Yesu.
Biblia inatuambia;
“Wenye haki wakiwa na amri (wakikamata nafasi za uongozi na mamlaka), watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua”
(Mithali 29:2).
Tunapozungumzia uongozi tunaongelea hali za watu na hatma ya ndoto zao.
Biblia inasema mwenye haki akipata nafasi ya kuongoza anapitisha vitu ambavyo vinapelekea watu kufurahi.
Ila waovu wakitawala huleta hali mbaya na ngumu kwa watu walio chini yao.
Ukiona hali ya watu katika eneo ni mbaya, vitu haviendi, malalamiko, kero haziishi, vilio, maandamano hayakomi unajua moja kwa moja utawala uliopo ni wa watu wasio haki.
Uongozi ni kwa ajili ya walioko chini yako si kwa ajili yako wewe kiongozi.

Suleimani kiongozi mahiri aliyekaa kwenye kiti cha uongozi bila kupigana vita hadi moja hadi anamaliza uongozi wake, alijua siri hii ya kuwa uongozi si kwa ajili ya kiongozi bali ni kwa ajili ya watu walioko chini yake.

Alipopewa jukumu la kumrithi baba yake Daudi haya yalikuwa maombi yake kwa Mungu;

“Na sasa, Ee Bwana, Mungu wangu, umenitawaza niwe Mfalme badala ya baba yangu Daudi (UMENIPA NAFASI YA UONGOZI KITAIFA); Nami ni mtoto mdogo tu; SIJUI INIPASAVYO KUINGIA NA KUTOKA. Na mtumwa wako yu katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao kwa kuwa ni wengi.
Kwahiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?
NENO HILI LIKAWA JEMA MACHONI PA BWANA, YA KUWA SULEMANI AMEOMBA NENO HILI”
(1Wafalme 3:7-10).

Mambo ya kiuongozi ambayo tunaweza kujifunza kwa kiongozi aliyefanikiwa Sulemani;

1. Alijua mbali ya kuwa yeye kapewa nafasi ya uongozi wa kitaifa, lakini yeye pia ni MTUMWA KWA MUNGU (NI MTUMISHI WA MUNGU)!
Maana yake yeye anatumika katika ile nafasi kwa niaba ya “BOSS” wake Mungu.
“Umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako” (mstari wa 7).
Usipojua kuwa nafasi ya uongozi uliyonayo kwenye familia (kama mama, baba, kijana mkubwa wa familia), ofisi, idara, taasisi, kampuni au hata serikalini ama kanisani UMEIKALIA KWA NIABA YA BOSS WAKO ANAYEKUANGALIA KILA SAA TOKA MBINGUNI, utakosa nidhamu na utafanya bora liende.
Lakini ukijua UTATOA HESABU SIKU MOJA KWAKE; itakufanya uwe serious kutumika na si kutumikiwa!

2. Alijua hao watu ANAOWAONGOZA si wake ni wa Mungu.
“…nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu WATU WAKO…” (Mstari wa 9).
Ukitambua kuwa watu unaowaongoza ni wa Mungu na si wako, itakufanya UWAFIKIRIE WAO KWANZA.
Biblia inasema, “Huwezi kumpenda Mungu unayemuona ilhali unamchukia jirani yako unayemuona”
Huo ni unafiki!
Ukishajua nafasi yako ya uongozi inakufanya ukutane na watu wa Mungu, utawahudumia na kugusa mahitaji yao kwa uaminifu ukijua “unapomtendea mmojawapo wa wadogo hao umemtendea yeye”
Itakufanya uwe na mentality ya kutumika kuliko kutumikiwa.
Watu wengi wanapopata nafasi za uongozi wanawa-abuse walioko chini yao kwa sababu hawajui kwamba hawa ni watu wa Mungu hata kama Mungu kawaweka chini yao!
Ukielewa hili uongozi hautakusumbua, utajua unafanya kwa ajili ya Mungu na hakika utapokea baraka za uongozi.

3. Alijua kuongoza mwanadamu mwenzako ni kazi kubwa sana ambayo inahitaji NGUVU YA MUNGU na si hekima ya kawaida ya kibinadamu na akatafuta msaada kwa Mungu.
i) Aliomba na kumueleza Mungu mashaka yake na hofu zake.
(Wafilipi 4:6-7).

ii) Aliomba MOYO WA ADILI (UADILIFU);
Uadilifu si kitu ambacho mtu anazaliwa nacho au kukiokota.
Ni kitu kinachojengwa na Mungu ndani ya mtu ambaye ana HOFU YA MUNGU na aliyekiomba kwa BWANA.
Suleimani aliomba “moyo wa uadilifu” (mstari wa 9).
Bila uadilifu hauwezi kuwa kiongozi bora kwenye eneo Mungu alilokuitia.

iii) Aliomba karama ya kupambanua mema na mabaya.
“…na kupambanua mema na mabaya”
Biblia inasema;
“Moyo wa mtu ni mdanganyifu na una ugonjwa wa kufisha, nani awezaye kuujua?”
(Yeremia 17:10).
Pia inasema; “Mna hila nyingi moyoni mwa mtu…” (Mithali 19:21).
Hii ndiyo hali halisi ya mioyo ya wanadamu.
Mioyo yao haiko salama, kama huna uwezo wa kupambanua mema na mabaya, utafanya makosa mengi ya kimaamuzi unaposhughulika na kesi za watu.
Wanaweza kukuingiza matatani na kuharibu kabisa sifa zako na uongozi wako.
Unahitaji kuwa na uwezo wa kupambanua mema na mabaya ili uweze kutofautisha kati ya mbivu na mbichi na mchele na chuya!

4. Suleimani aliomba msaada wa Mungu kwenye uongozi aliopewa na Mungu na alipewa;
-hekima
-akili nyingi sana
-moyo mkuu kama mchanga wa bahari (uongozi unahitaji uwe na moyo wa kipekee, maana utakosolewa, utatukanwa, utabebeshwa mizigo isiyo yako, utasingiziwa na mengine mengi ya kuumiza)!
(1Wafalme 4:29).

KWANINI KILA MTU ALIYEOKOKA ANAPASWA KUKAA TAYARI KWA AJILI YA UONGOZI?

1. Kila mtu ni kiongozi.
Usipokuwa mama utakuwa baba, kaka au dada wa wengine, na wote watatarajia kitu kipya cha kujifunza na kusogezwa toka kwako!

2. Nafasi alizotupa Yesu kama wanafunzi wake zinamlazimisha Mkristo kuwa kiongozi automatically;
Yesu alisema sisi ni;
i) Nuru
Lazima tutoe nuru kwa wengine, haijalishi tuna nafasi za kiutawala au la.
Tuna kitu ambacho waliotuzunguka hawana.

ii) Chumvi
Yesu anatarajia tutie ladha kila mahali palipokosa ladha anapotupa nafasi ya kuwa.
Anataka tuwe watu wa kuzuia uharibifu usitokee pale tulipo (hii ni kazi ya chumvi kuhakikisha nyama na vyakula visiharibike. Ni PRESEVATIVE AGENT).
Ni wajibu wangu na wako kuhakikisha ubaya haupenyi tulipo.
HIZI NI NAFASI ZA KIUONGOZI.
Tena si nafasi za uongozi wa viwango vya chini.
Ni uongozi wa kiwango cha duniani.
Jesus has called us to lighten our World.
To influence the earth with Kingdom principles.

3. Uhitaji mkubwa wa watu waadilifu, wacha Mungu, watu wa haki na wakweli unapelekea kila aliyeokoka kuwa na nafasi ya kiuongozi maana ni wale walio katika Kristo Yesu kwelikweli wenye vigezo hivi.
Tumeona Mithali 29:2 ya kuwa watu hufurahi wenye haki wakitawala.
Haijalishi watu walioko duniani ni wabaya na watenda dhambi lakini hawako tayari kuongozwa na waovu wenzao.
Wanataka waadilifu, wasafi, wachapakazi, wasema kweli, wapinga rushwa na wateteaji wa haki zao.
Na hii inawafanya WALIOOKOKA wawe na soko kubwa kwenye eneo la uongozi.

MAJUKUMU YA KIONGOZI

Zaburi 32:8
“Nitakufundisha na kukuonyesha njia ya kuiendea, nitakushauri jicho langu likikutazama”

i) Kufundisha
Kila kiongozi wa kweli lazima awe na uwezo wa kufundisha walio chini yake.
Lakini huwezi kufundisha kama huna bidii kujifunza.
Paulo alimsisitiza Timotheo;
“Hata nitakapokuja, UFANYE BIDII katika kusoma, kuonya na kufundisha”
(1Timotheo 4:13)
Mtu yeyote anayesoma na kuongeza maarifa atajua vitu vingi na ataonya na kufundisha kwa ubora wale walioko chini yake!
TENGA MUDA KUSOMA VITABU, KUSOMA MAFUNDISHO, KUSIKILIZA AUDIO NA DVD ZA KUKUJENGA KWENYE MAENEO MBALIMBALI hasa kiroho, imani, uongozi, mahusiano, biashara na mengine mengi itakufanya uwe kiongozi mzuri sana!

ii) Kuonyesha njia sahihi ya kuiendea
Kiongozi lazima uwe na maono. Lazima uwe na uwezo wa kuona mwisho tangu mwanzo.
Na kutengeneza njia ya kukusaidia kufikia hiyo hatma uionayo.
Halafu ukimaliza unawashirikisha walioko chini yako maono yako na namna ya kufika huko (mikakati)!

iii) Kushauri
Kila kiongozi lazima awe na wigo mpana wa hekima, maarifa na ufahamu ambavyo vitamsaidia kuwashauri walioko chini yake.
Yesu ni kiongozi wetu (Mfalme) na anaitwa “Mshauri wa ajabu” (Isaya 9:6-7).
Huwezi kuwa Mfalme bila uwezo wa kushauri.
Kama kiongozi panua mipaka yako ya hekima, maarifa na ufahamu.

iv) Uangalizi
“…jicho langu likikutazama”
Kila kiongozi wa kweli lazima awe na uwezo wa kiungalizi na kiusimamizi.
Lazima uwe na muda wa kuangalia watu wana mambo yao.
Lazima uwe na uangalizi na usimamizi kwa rasilimali na vitu vilivyoko chini yako na mikononi mwako!

Msihi Mungu akupe Roho zake saba, ambazo zitakufanya uchomoze kwenye uongozi.
(Isaya 11:2).
Lakini jitambue kama kiongozi.
Uongozi si nafasi/ cheo, uongozi ni impact yako kwa watu wanaokuzunguka.
Uongozi ni vile unavyogusa na kugeuza maisha ya wengine.
Umebarikiwa,
WEWE NI SHUJAA, MTU MKUU NA MBARIKIWA.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA. (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 14 ]
  1. Minga stanton says:

    Mungu akubariki Sana kwa utumishi mwema

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: