SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day 15]

https://i2.wp.com/thinklink.in/wp-content/uploads/2011/03/sun-sky-lg1.jpg

19/01/2016.

“UWEZO WA KUTAMKA VITU VIKADHIRIKA KATIKA UHALISI (THE POWER TO SPEAK THINGS INTO EXISTENCE)”

“Nawe UTAKUSUDIA NENO NALO LITATHIBITIKA, na mwanga utaziangazia njia zako”
(Ayubu 22:28).
Tafsiri ya Kiingereza ya Biblia ya KING JAMES andiko hili linasema; “THOU SHALL DECLARE A THING AND IT SHALL BE ESTABLISHED UNTO THEE…”
Yaani “UTATAMKA VITU NAVYO VITATOKEA KWAKO KAMA ULIVYOTAMKA…”
Siamini kama kuna mtu ambaye hataki kufika VIWANGO HIVI vya kufanya mambo aliyosema yatokee!
Naamini unatamani uwe ukimwambia Mgonjwa “Uwe mzima” hapohapo uzima utokee… Ukiiambia biashara ambayo inasuasua au inakaribia kufa “Biashara anza kutoa faida” mara moja faida ianze na isife tena… Ukiiambia ndoa inayosuasua “Ndoa heshima yako irejee” shuhuda zianze kuwa upendo na amani vimerudi.

Naamini kila mtu anatamani atembee kwenye NGUVU HII lakini ukweli unabaki palepale; NI WATU WACHACHE WANAOJUA KUHUSU UWEPO WA NGUVU HII NA WANAJUA KUITUMIA KUFANYA VITU VITOKEE!

Yesu alijua kuhusu nguvu hii ya KUSEMA VITU VIKATOKEA na alikuwa akiwashangaza watu wengine kwenye kizazi chake!

Siku moja alikuwa akivuka baharini na wanafunzi wake. Ikatokea kukawa na mawimbi, upepo na dhoruba, wakawa katika hatari ya kuzama.
Walipomuamsha HAKUCHUKUA CHOMBO KUCHOTA MAJI KAMA WAO.
Bali alitoka na KUYASEMESHA MAWIMBI, UPEPO NA BAHARI vikatii na kukawa na shwari kuu.
Walipoona ANASEMA VITU VINATOKEA… Walibaki midomo wazi, wakaanza kusema kwa hofu: “HUYU NI MTU WA NAMNA GANI HATA PEPO NA BAHARI ZAMTII?” (Mathayo 8:27).

Haya mambo hayajaisha; Ukipokea UWEZA HUU WA KUSEMA VITU VIKATOKEA, heshima yako itapanda mno. Watu wataulizana “HUYU NI MTU WA NAMNA GANI?”
Ni maombi yangu ukimaliza hili somo na kutendea kazi kanuni hizi watu waanze kuulizana “huyu ni mtu wa namna gani??”

JE MUNGU ANAPENDA TUSEME VITU NA VITOKEE??

Nakuhakikishia ndugu yangu unayesoma ujumbe huu, Mungu anataka uwe na UWEZO WA KUUMBA NA KUFANYA VITU VITOKEE KWA MANENO YAKO.

1.Mungu alipotuumba, alituumba kwa SURA NA MFANO WAKE (Mwanzo 1:26-27).
Kwa kiingereza maneno Sura (Likeness), na Mfano (Image) yana maana kubwa!!
Neno image lina maana ya ICON (Visible representation of invisible thing) kama ambavyo kwenye kompyuta tuna ICON ambayo inawakilisha SOFTWARE PROGRAM zisizoonekana, ndivyo Mungu alivyotuumba tukiwa na upande wa IMAGE/ICON (UPANDE UNAOONEKANA UNAOMWAKILISHA MUNGU ASIYEONEKANA)!!
Na Neno LIKENESS lina maana ya CHARACTER (Invisible attributes, altitudes, mindset and habits).
Ikiwa na maana ya kuwa Mungu ametuumba tukiwa na maeneo makuu mawili ambayo yote yanakusudiwa kumuwakilisha Mungu kwenye ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho.
Mfano (image) yaani mtu wa nje ni Uwakilishi wa Mungu katika ulimwengu wa mwili/ hapa duniani na Sura (Likeness) ni mtu wa ndani ambaye ana mawasiliano na ulimwengu wa roho!
Huyu mtu wa rohoni kazi yake ni;
-Kuona yasiyokuwepo nje (kupitia maono na ndoto, au neno la Mungu ulilosoma au kuhubiriwa/ kufundishwa)
-Kudaka mawazo (ideas) zinazoelea kwenye ulimwengu wa roho na kuzitafsiri nje.
-Kuchukua vitu nje (na kuviwasilisha rohoni)
-Kuyasema yasiyokuwepo nje ili yatokee nje.

Kutokana na uumbaji huu, Mungu ambaye ni Roho ametupa “sura yake (likeness)” ambayo inatupa UWEZO WA KUSEMA VITU TOKA ROHONI VIKAJA NJE!!
Ile tu kwamba umeumbwa na Mungu kwa sura na mfano wake, tayari una kiwango fulani cha kusema vitu na vikatokea!
Ndio maana Mzazi akitamka laana kwa mtoto inampata, haijalishi ana upako au la!
Mtu anayekiri magonjwa, kushindwa, kutoweza, lawama, manung’uniko YANATOKEA HAYO ALIYOSEMA.
Kila mtu anaweza kuumba vitu kwa kukusudia na hata kwa kutokusudia.
Ulimwengu wa roho umeshajipanga kuhakikisha vitu vitokee vikisemwa.
Tayari ndani yako kuna uwezo fulani wa kusema vitu vikatokea, utumie vizuri.
Usiache sura ya Mungu na mfano wake utumike kuumba matatizo kwako na kwa wengine, tumia ulimi na maneno yako kwa namna chanya!

2. Mtu akisikia NENO LA MUNGU na akalielewa ghafla kwenye ulimwengu wa roho anabadilika na kuwa MUUNGU kwenye kile ambacho amesikia na kuelewa.
Hii ni babkubwa… Ebu tusome kauli hii ya Yesu; “Ikiwa ALIWAITA MIUNGU wale WALIOJILIWA NA NENO LA MUNGU…” (Yohana 10:35).
Yaangalie tena hayo maneno tena rafiki!
Biblia inasema kwa kinywa cha Yesu, “Neno likimjia mtu na akalielewa na kulipokea anabadilika na kuwa muungu”
Sasa ukishakuwa “muungu” ukikisema kile ambacho umekipokea kifanya vitu viumbike na kutokea!
Lipende Neno la Mungu, lichimbe kwa kina, liamini bila kujiuliza, litumie kama sheria isiyopingwa, halafu UTAANZA KUSEMA VITU NA VITAANZA KUTOKEA.
Lipe heshima Neno la Mungu, LITAKUFANYA MUUNGU!

3. Unapookoka tu, inakupa haki ya kufanyika kuwa MTOTO WA MUNGU (Yohana 1:12).
Na Biblia inasema kuhusu sisi TULIOOKOKA ya kuwa TU WANA WA MUNGU hata kama ulimwengu (wasioamini) haututambui, bado hawageuzi ukweli kwamba sisi ni WANA WA MUNGU (1Yohana 3:1-2).
Sasa huwezi kuwa “mtoto wa mtu” na usiwe mtu!
Huwezi kuwa “mtoto wa mbwa” na usiwe mbwa!
Kama ambavyo mtoto wa mbuzi ni mbuzi… Mtoto wa nyoka ni nyoka… Vivyo hivyo MTOTO WA MUNGU NI MUUNGU!!
Na ukishajua wewe ni MUUNGU (Zaburi 82:6), utaanza KUUMBA VITU NA VITATOKEA kama ambavyo Baba yako wa mbinguni alifanya kwenye Mwanzo sura ya kwanza!!

KWANINI WALIOOKOKA WENGI HAWANA NGUVU HII YA KUUMBA VITU NA KUTAMKA VITU VITOKEE??

1. Kutojua kwamba tayari wameumbwa na sura na mfano wa Mungu ambao unakupa haki ya kuumba vitu na kutamka vitu vikawa kama alivyofanya Mungu.
(Mwanzo 1:26-27).

2. Hawaliheshimu Neno la Mungu na kulipa nafasi wakijua linaweza kuwafanya wawe miungu (Yohana 10:35).
Usipoliheshimu Neno, usipolipa muda, usipoliamini kama uhai wako, utatamka vitu havitatokea!

3. Kutojua siri ya Uungu ulionao ndani ya Yesu kwa kule “kuzaliwa mara ya pili kwa Roho” (Yohana 1:12-13, Yohana 3:6).

4. Kutoenenda katika upendo.
Imani hufanya vitu vitokee (Marko 9:23).
Lakini imani ina kizuizi kimoja endapo hakitazingatiwa haitoi matokeo, na kitu hicho ni UPENDO.
Biblia inasema IMANI hufanya kazi pamoja na Upendo (Wagalatia 5:6).
Ukikosa upendo, imani inagoma kufanya kazi.
Na imani ikigoma VITU HAVITATOKEA!
KAZANA PENDO LA MUNGU LILILO NDANI YAKO LIKUE (Warumi 5:5).
Kadri unavyokuwa deep katika upendo, imani itafanya kazi na kukupa matokeo; UTATAMKA VITU NA VITATOKEA!
Kumbuka: Upendo unamhusu Mungu na watu… Mpe Mungu upendo wote ulionao, na wape watu upendo kwa kile kidogo ulichonacho halafu utashangaa UKISEMA VITU VINATHIBITIKA.

5. Tunza uwepo wa Mungu maana huo ndio mtaji mkubwa wa kufanya uyasemayo yatukie.
Ukiwa na ushirika mzuri na Mungu, “…atalithibitisha neno lako kwa ishara zitakazofuatana nalo”
(Marko 16:20)

Natamani ufikie mahali uwe kama;
i) Samueli
” Samueli akakua, naye BWANA ALIKUWA PAMOJA NAYE, wala HAKULIACHA NENO LAKE LOLOTE LIANGUKE CHINI”
(1Samweli 3:19).

ii) Eliya
Huyu ndugu aliwahi kuitwa “mtaabishaji wa Israeli” kwa sababu alizuia mvua isinyeshe juu ya nchi kwa “neno lake” na akairuhusu inyeshe tena baada ya muda huo.
Hakusema “naizuia kwa miaka mitatu na nusu kwa neno la BWANA” hapana!
Alisema “kwa neno langu (mimi kama Eliya)” na ikawa hivyo.
Alichokisema ndicho kilichotokea.
(1Wafalme 17:1).
Si hilo pekee amewahi kuamuru moto ushuke toka mbinguni na kuwateketeza askari waliotumwa kumkamata.
Alipokuwa akisema kitu kama alivyoamuru ndivyo inakuwa.

Hawa ni baadhi ya watu waliotembea na uweza huu wa kutamka vitu na vikatokea.
Nakuombea utakapomtafuta BWANA akujibu na kuubadili mdomo wako, autakase ulimi wako, na ayape uhai na uzima maneno yako na yawe na uweza wa kuthibitika yakitamkwa!
Umebarikiwa,
WEWE NI SHUJAA, WEWE NI MTU MKUU MNO KWA DUNIA YAKO NA VIZAZI VINGI VIJAVYO!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: