SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA. (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 17]

 

21/01/2016
“NGUVU YA KUZAA VITU NJE YA KANUNI ZA KIBINADAMU (POWER TO BIRTH THINGS OUT OF HUMAN ORDER AND PRINCIPLES)”

elijah-prophet

“Mariamu akamwambia malaika, LITAKUWAJE NENO HILI, MAANA SIMJUI MME? Malaika akajibu akamwambia, ROHO MTAKATIFU atakujilia juu yako, NA NGUVU ZA ALIYE JUU ZITAKUFUNIKA KAMA KIVULI; kwahiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”
(Luka 1:34-35)
Huyu ni Mariamu, anapewa unabii wa KUZAA NJE YA KANUNI ZA KIBINADAMU… Haikumuingia akilini, haikueleweka, lilikuwa ni wazo la kijinga na la kipuuzi… Lakini MWISHO WA SIKU ALIZAA NJE YA KANUNI YA KIBINADAMU!!!

“Hata alipokwisha kunena (kufundisha na kuhubiri), alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, MKASHUSHE NYAVU ZENU MVUE SAMAKI. Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA, TUSIPATE KITU; lakini KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU. Basi walipofanya hivyo WALIPATA SAMAKI WENGI MNO, NYAVU ZAO ZIKAANZA KUKATIKA; Wakawapungia washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje wasaidiane; Wakaja wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama”
(Luka 5:4-7).
Huyu ni Petro na wenzake.
Walitumia KANUNI YA KIBINADAMU YA KUVUA SAMAKI USIKU KUCHA (Maana ndio muda mzuri wa kuvua na kupata samaki), lakini HAKIKUPATIKANA KITU.
Halafu Yesu anawapa agizo la KUVUA MCHANA WA JUA KALI yaani nje kabisa ya KANUNI ZA KIBINADAMU ZA KUZAA VITU.
Haiingii akilini, haiingii moyoni, haipokelewi na moyo wa kila mtu.
Lakini ashukuriwe Mungu kwa ajili ya Petro kwa sababu ya Ufunuo kuwa NENO LA YESU LINAWEZA KUZAA VITU NJE YA MFUMO NA KANUNI ZA KIBINADAMU.
Alipodaka huu ufunuo; Kilizaliwa kitu nje kabisa ya Utaratibu wa kibinadamu.
Hii ndiyo NGUVU YA KUZAA VITU NJE YA KANUNI ZA KIBINADAMU.

“Na siku ya tatu palikuwa na Arusi huko Kana, Mji wa Galilaya; naye mamake Yesu alikuwepo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pake pamoja na Wanafunzi wake.
Hata DIVAI ILIPOWATINDIKIA (Ilipowaishia), Mamaye Yesu akamwambia, HAWANA DIVAI. Yesu akamwambia, mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu bado haijawadia. Mamaye akawaambia watumishi, LOLOTE ATAKALOWAAMBIA FANYENI… Yesu AKAWAAMBIA, JAZENI MABALASI MAJI. NAO WAKAYAJALIZA HATA JUU. Akawaambia, sasa tekeni mkampelekee mkuu wa meza. WAKAPELEKA. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji kumbe yalikuwa DIVAI (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka maji)…”
(Yohana 2:1-9)
Kanuni ya kibinadamu ya kupata divai inahitaji UITENGENEZE.
Uwe na zabibu, maji na vitendea kazi vingine ili upate divai.
Lakini Yesu ALIITENGENEZA BILA HATA ZABIBU kwa kutumia maji tu na Neno lake.
Hii haikuwa kawaida, hii haikuwa njia ya kibinadamu ya kuzaa kitu, HII ILIKUWA NGUVU YA KIUNGU YA KUZAA VITU.

Ukisoma mifano mitatu yote hapo juu utajifunza siri itakayokupa matokeo hayohayo;

1. Neno la Mungu ndilo linaloumba na kuzaa vitu hata kama Kanuni za kibinadamu zinagoma.
i)Malaika Gabrieli alileta NENO LA UNABII ambalo LILIZAA KILICHOZALIWA.
Ndiyo maana Yesu anaitwa Neno la Mungu lililochukua mwili na kuja kwetu (Yohana 1:14, Mathayo 1:23).
ii) Petro alisema “KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU”
Aliamini Neno la Mungu kuliko KANUNI YA KIBINADAMU YA KUVUA SAMAKI USIKU.
Neno la Mungu linaweza kuzaa chochote likipewa nafasi.
iii) “Lolote ATAKALOWAAMBIA FANYENI…AKAWAAMBIA JAZENI MABALASI MAJI…AKAWAAMBIA MPELEKEENI MKUU WA MEZA…”
Divai haikupatikana nje ya Kanuni za Kibinadamu bila Neno kwanza.
Neno lilizaa divai toka kwenye maji matupu.
Neno ni muhimu mno ukitaka KUZIAIBISHA NA KUZIPINDA KANUNI ZA KIBINADAMU.

2. Lazima Mpokea Neno apokee:
Usipolipokea Neno kwa ujasiri na imani haliwezi kukufanyia kazi.
“Lile Neno halikuwafaa wao kwa maana halikuambatana na imani mioyoni mwao”
(Waebrania 4:2).
Unapotaka KUZAA VITU NJE YA KANUNI ZA KIBINADAMU LAZIMA NENO LA MUNGU ULILONALO ULICHANGANYE NA IMANI MOYONI MWAKO HATA KAMA AKILI YAKO INABISHA.
Kumbuka: “KWA MOYO MTU HUAMINI” na si “KWA AKILI HUAMINI”
Hata akili ikiwa inabisha kama ilivyobisha kwa Mariamu “Litawezekanaje neno hili?” Au kama Petro, “Tumefanya kazi usiku kucha na tusipate kitu”…vuka hapo AMINI NENO MOYONI NALO LITAKUPA KISICHOWEZEKANA KIBINADAMU!!
Mariamu aliamini moyoni akasema: “NA IWE KWANGU SAWASAWA NA NENO LAKO” (Luka 1:38).
Petro naye aliamini moyoni mbali ya mashaka kichwani akasema: “LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU” (Luka 5:5).

3. Dhihirisha nje imani yako kwa tendo la imani, maana imani yoyote iliyotokana na Neno itakupa tendo la imani la kufanya.
-Kwa Petro iliambatana na tendo la kushusha nyavu.
(Luka 5:5)
-Kwa wale wa Kana iliambatana na kuchota maji na kuyapeleka kwa mkuu wa meza.
(Yohana 2:7,8).
-Mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka 12, imani ilimpa tendo la kugusa pindo tu na akaponywa (Marko 5:25-28).
IMANI INAKUPA CHA KUFANYA KINACHOFANYA VITU VIZALIWE NJE YA KANUNI ZA KIBINADAMU.

Nakuombea uelewe siri hii, na uombe neema ya kutembea katika NGUVU HII YA KUZAA VITU NJE YA KANUNI ZA KIBINADAMU!

WEWE NI MTU MKUU, NI SHUJAA NA ULIYEBEBA HATMA ZA WENGI.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: